Julius Mtatiro: Muongo asiye na Kumbukumbu

Julius Mtatiro: Muongo asiye na Kumbukumbu

COMMENT YA MCHANGIAJI







Lakini na wewe Mtatiro kwenye msiba wa Wilson Kabwe,ulilaani kitendo cha mtoto wa marehemu kutompa mkono Paul Makonda,ukasema si uungwana,unakumbuka?

Nilikukosoa na nikakuambia, kwangu mimi yule dada ni shujaa kwakuwa hakuwa na chembe ya unafiki kwa kile alichofanyiwa marehemu wakati wa uhai wake.

Leo naona majibu umeyapata,watu wanafiki haina haja ya kuwaficha,ukweli utakuweka huru,hapo SEIF kaonesha wazi kwamba moyo wake haupo na wanafiki wa CCM waliomuweka mzee Jumbe kizuizini miaka yote 32,pia wanafiki wanaowakamata na kiwatesa wafuasi wa CUF Znz.

Huo ndio ukweli na unapaswa kuwa wazi,ukweli uliojificha ni unafiki.




JIBU LA JULIUS MTATIRO


↓↓↓↓↓↓
Kuna tofauti kubwa sana kati ya tukio la Makonda na Mtoto wa Kabwe na hili. Kifo cha Kabwe hakikusababishwa Makonda. Kitendo cha Makonda kueleza tuhuma za Kabwe hadharani kilikuwa ni wajibu. Unafananisha suala hilo na hili la Shein kupora ushindi wa Wazanzibari waziwazi na kwa kutumia mabavu mwaka jana? Makonda is innocent, Shein will never be innocent kwa dhambi ya mwaka jana. Sikuwa mnafiki brother.
Sijui dhamira ya Mtatiro ni ipi? lakini akumbukwe Maalim ndiye aliyesababisha Jumbe kutimuliwa kazi baada ya kupeleka unafiki kwa Mwalimu, nashangaa hata hapo msibani alifuata nini? katika uhai wa Jumbe sikuwahi msikia maalim akimwongelea, kawa makamu wa Rais alishindwa nini kupeleka hoja ya kumwachia huru? halafu leo analeta unafiki msibani.
 
Fikiria tu,umefika sehemu ukasalimia watu lakini mtu mmoja akakataa kusalimiana na wewe ungejisikia vipi..!


Sasa huyo ni mkuu wa nchi amenyimwa mkono mbele ya wananchi wake unafikiri inaumiza kidogo??
Mwenye akili ataumia nini Shein kunyimwa mkono ?? sema Seif alikuwa na aibu angemtemea mate !!
 
Sasa ndio tumejua sura halisi ya Maalim, hivi anamnunia shain kwa lipi? umakamu wa Rais haukumtosha basi hakuna cha kumtosha, mtoto ukimpa bakuli la uji akalipiga teke kinachofuata huwa ni makofi bila kujali ana njaa.
Umakamu gani huo ??!! Makamu boya ya kusimangwa ?! Ya kupangiwa ?!. Yeye Shein mbona hajaukubali huo umakamu ?! BORA KUKOSWA
 
Mtatiro ni mchumia tumbo.
Wanasiasa vijana wa kizazi hiki hawana msimamo.
 
Mtatiro nae bhana! Kosa la Siasa ni kuwa wajinga wako kwenye siasa werevu wamebaki wanawashangilia. Mtu usiokuwa na msimamo na majibu mepesi unataka wananchi wakuamini?
 
hivi mtatiro si. ndo aliyekiua chama cha. wananchi kule bara mpaka wakamtoa
 
'...utawaombeaje waliokufa ikiwa una chuki na walio hai?' Huyo ni Mtatiro kwenye msiba wa W.Kabwe. Hiyo sentensi haiwezi kutumika kwa Maalim? Labda hasira yake ingekuwa kwa Jecha,mshika kipenga.
Kiongozi mkuu wa nchi kainama kumsalimia raia, lakini raia anazira. Tawala zote hutoka kwa Mungu,ni baraka kusalimiwa na mkuu wako.
 
Kwani kwenye msiba wa Jumbe aliyefiwa ni Sheni? Sheni ndie muhusika mkuu wa Msiba wa Jumbe?
 
'...utawaombeaje waliokufa ikiwa una chuki na walio hai?' Huyo ni Mtatiro kwenye msiba wa W.Kabwe. Hiyo sentensi haiwezi kutumika kwa Maalim? Labda hasira yake ingekuwa kwa Jecha,mshika kipenga.
Kiongozi mkuu wa nchi kainama kumsalimia raia, lakini raia anazira. Tawala zote hutoka kwa Mungu,ni baraka kusalimiwa na mkuu wako.
Mkuu umeaza vizuri akamalizia vibaya. Sio kweli kwamba tawala zote hutoka kwa Mungu, asikudanganye mtu! Watu wengi husema hivyo bila kutafakari.
 
Shein haoni hat aibu!!! Kweli madaraka matamu!! Ila naamini ni shinikizo la bara kuwa Shein akomae tu kwa marudio nchi isiende kwa CuF! Ila rohoni inamuuma sana maana anajua ushindi sio wake!!!
 
Inasikitisha, ukiwa mnafiki wa kiwango cha changarawe katika ujana wako utakuja kuwa mchawi wa kiwango cha lami uzeeni.
 
11203156_10155430241345198_8819449306200691384_n.jpg
Mkono unasema.
 
Back
Top Bottom