Jukwaa la Wahariri(TEF),mnafanya kosa lile lile lililofanywa na Maaskofu wa KKKT na TEC

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
JUKWAA LA WAHARIRI (TEF), MNAFANYA KOSA LILELILE LILILOFANYWA NA MAASKOFU WA KKKT NA TEC

Aprili 5, 2018
Dar es Salaam.

Muda mfupi uliopita nimesikiliza Tamko la Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) kuhusu hali ya nchi yetu.

Kimsingi TEF walichokifanya hakina tofauti na kile walichokifanya Baraza la Maaskofu wa Kanisa la Kiinjilisti la Kilutheri Tanzania (KKKT) na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), ambacho ni kuendeleza wimbo wa ajenda za kisiasa zenye mlengo wa siasa za upinzani.

Huku ni kupotoka kwa hali ya juu sana.

Niliwahi kuhoji huko nyuma juu ya uhalali na uhalisia wa TEF ambao ni mabosi au viongozi wa waandishi wa habari nikiwemo mimi. Nilihoji hivi kwa sababu nikiwa mwandishi wa habari mpaka leo sijaelewa na wala sijaeleweshwa kuhusu Jukwaa la Wahariri ambalo naamini linapaswa kuwa na uhusiano wa karibu na waandishi wa habari hasa ikizingatiwa mara zote linazungumza masuala yanayowahusu waandishi wa habari kama lilivyofanya leo.

Nasema hivyo kwa sababu TEF inatoa matamko ambayo yanabeba sura kuwa ni matamko ya waandishi wa habari wakati kiuhalisia siamini kuwa huo ndio msimamo wa waandishi wa habari wa nchi hii.

Nilikuwa nafuatilia mkutano wa TEF, nimemuona Deodatus Balile na Neville Meena wakiendesha mkutano huu, wametoa hoja nyingi ambazo kimsingi na kwa ufupi hakuna tofauti na Waraka uliotolewa na Maaskofu wa KKKT na TEC kabla ya Pasaka.

Kwa bahati nzuri nilipata kusoma barua ya Prof. Kitila Mkumbo aliyomuandikia Askofu wake Fredrick Shoo. Na katika barua hii kwa usomi na unyenyekevu mkubwa Prof. Kitila Mkumbo alieleza namna maaskofu walivyojikwaa katika waraka wao na akatoa ushauri wake kwao.

Na mimi pia naomba nifanye hivyohivyo kwenye nyie Maaskofu wangu yaani Jukwaa la Wahariri na kwa kweli nikulenge wewe Kaimu Mwenyekiti wa TEF Deodatus Balile ambaye umelisoma tamko la TEF.

Ndugu Balile tamko lenu linatuletea maswali mengi kwenye jamii na hasa Serikali ambayo ni sehemu muhimu ya kazi zetu za kila siku. Mimi nikiwa mmoja wa waandishi wa habari ambao hawajashirikishwa na wala hawajawahi kushirikishwa kwenye masuala ya TEF limenikwaza kwa sababu wadau ambao nafanya nao kazi kwa karibu ni Serikali ambayo kimsingi tamko lenu linaituhumu kwa mambo mazito yenye vinasaba vya siasa za upinzani.

Nilitarajia kwa dhamana ambayo TEF imebeba ingefanya utafiti wa kutosha kabla ya kuandika tamko hili na kuja kulisoma kwa waandishi wa habari, nilitarajia waandishi wa habari tungejulishwa kupitia vyama vya waandishi wa habari wa mikoa (Press Clubs) ama kupitia Umoja wa Vyama vya Waandishi wa Habari (UTPC) ama ikishindikana kupitia vyombo vyetu vya habari, kuwa kuna tamko hili zito litatolewa kuhusu sisi.

Badala yake Balile na wenzako akina Neville Meena mmekaa na kwa mawazo yenu, hisia zenu na malengo yenu mkaamua kuandika mlichoandika na kisha kwenda kukisoma kwenye mkutano wa vyombo vya habari, mkibeba sura ya Tamko la Jukwaa la Wahariri wakati ndani yake mnazungumza kwa niaba ya waandishi wa habari.

Sasa twende hoja kwa hoja, mosi, mnasema kuna sintofahamu katika hali ya uchumi, mnazungumza hilo kwa kuzingatia nini? Maana takwimu zinaonesha hali ya uchumi wa nchi yetu ni nzuri? Takwimu za hivi karibuni zinaonesha kuwa uchumi wetu umepanda na sasa unakua kwa asilimi 7.1 kutoka 6.8, mfumuko wa bei umeshuka hadi asilimia 4.5, nchi yetu ni kati ya nchi 5 zenye kasi kubwa ya kukua kwa uchumi barani Afrika.

Takwimu za Benki Kuu (BOT) zinaonesha nchi ina akiba ya fedha za kigeni zaidi ya Bilioni 5 za kutosha kuagiza bidhaa na huduma kwa miezi 6 na Rais kasema fedha za kutekelezea miradi mikubwa ya reli, kununua ndege, barabara, maji, ujenzi wa viwanja vya ndege, elimu bure, kujenga flyover, kujenga bandari, kununua dawa za hospitali na mengine, zipo. Rais kasema Serikali ina fedha za kulipa mishahara wafanyakazi na haikopi katika mabenki ya biashara kama ilivyokuwa zamani. Sasa nyie mnazungumza sintofahamu ya kutoka wapi?

Balile na wenzako mnasema kuna sintofahamu ndani ya jamii kwa sababu uhuru wa kutoa maoni unaminywa ukiwemo uhuru wa vyombo vya habari, labda niulize wewe Balile gazeti lako la Jamhuri na mambo mazito linayoyaandika kila toleo ni mahali gani umeminywa uhuru wako? Au nimuulize Meena makala anazoandika kila siku kwenye magazeti mbalimbali likiwemo Mwananchi, na jinsi zinavyoikosoa Serikali ni lini uhuru wake umeminywa? Au Mwandishi wa habari mkongwe Jenerali Ulimwengu na vijana wake akina Ezekiel Kamwaga jinsi wanavyotumia gazeti lao la Raia Mwema kuandika mambo mazito ya kuikosoa Serikali ni wapi uhuru wao unaminywa? Chukua magazeti ya leo Mwananchi, Tanzania Daima, Nipashe, Mtanzania kwa kutaja machache soma na angalia kuna habari ngapi zinaikosoa Serikali, umesikia yameminywa? Ipo mifano mingi.

Nilitarajia wewe Balile kwa elimu yako ya sheria ungekuwa mwalimu pale ambapo waandishi wa habari wanadhani wana haki ya kuandika chochote tu bila kutambua kuwa wana wajibu wa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni mbalimbali zilizopo hapa nchini na pia kuzingatia weledi katika taaluma hii ya uandishi wa habari.

Ningeelewa zaidi kama TEF katika tamko lenu mngesema pia kuhusu makosa ya dhahiri ambayo vyombo vya habari vinayafanya na mara kwa mara tunasoma Mkurugenzi wa Maelezo Dk. Hassan Abbas anavionya na vinaomba radhi.

Balile na wenzako mnasema vyombo vya habari vinafungiwa na kutozwa faini. Sasa mlitaka vikikiuka sheria iwaje? Na kama hakutakuwa na adhabu hizo sheria zimetungwa za nini? Na hapa tuwe wakweli vyombo vya habari vilivyofungiwa vinafahamika na makosa yake hutajwa. Na kwa sisi waandishi wa habari tunajuana na tunajua uhalali wa vyombo hivyo kufungwa, kwa nini hatujiulizi kila wakati ni vyombo vilevile tu?

Hivi Balile na wenzako kwenye TEF mnataka kutuaminisha kuwa Magazeti ya Mwanahalisi na Mawio hayakustahili kufungiwa? Gazeti la Tanzania Daima ambalo limemaliza kifungo chake na ambalo Neville Meena aliwahi kuwa Mhariri wake halikustahili kufungiwa kwa makosa yale?

Hivi Ansibert Ngurumo aliyekuwa Mhariri mmojawapo wa Mwanahalisi na MAwio na ambaye kwa sasa ametengeneza drama ya kujifanya kakimbilia uhamishoni nchini Finland ndivyo mnataka waandishi wa habari wa Tanzania tuwe hivyo? Mnakiona anachokifanya Ansibert Ngurumo akiwa huko Finland au mmefumba macho hamsomi maandiko yake kwenye mitandao ya kijamii?

TEF mmebeba ajenda nyingine ya siasa za upinzani ambayo hata Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe kaisema tena jana wakati akitoka rumande Segerea kuwa demokrasia imezorota, mmepima wapi kuwa demokrasia imezorota? Kaizorotesha nani? Au mnamhoji nani kiasi cha kutaka Rais Magufuli akutane na hao mnaosema ni makundi mbalimbali?

Hoja hizi ni za wanasiasa wa upinzani kabisa ambao wanapambana kuingia Ikulu leo mnataka kuzibeba nyie TEF? Kama ni kukutana na makundi mbona Rais anakutana nayo? Amekutana na waandishi wa habari na wakauliza maswali hadi yakaisha, amekutana na wafanyabiashara wameuliza maswali mpaka yakaisha, hukuna na viongozi wa dini na huzungumza nao, hukutana na wanasiasa na huzungumza nao na taarifa za Ikulu zinakuja. Labda mseme mlitaka akutane na akina nani? Na kama ni hivyo basi muda bado upo, Rais ana miaka miwili na sasa kauanza wa tatu kati ya miaka mitano ya kuwa kwake madarakani.

Yaani ndugu zangu Wahariri mnatuvalisha joho ambalo waandishi wa habari hatustahili kabisa. Maanda haya mnayoyaandika ndio nyimbo za vyama vya siasa vya upinzani vinavyounda Umoja wa Katiba ya Watanzania (UKAWA), nyimbo za akina Mange Kimambi na Evarist Chahali. Yaani mnafikia mahali mnataka kutuweka waandishi wa habari wa nchi kwenye kundi moja na Mange Kimambi?

Kwenye tamko lenu mmechukua tukio la mwandishi wa habari kupokonywa simu na polisi huko Dodoma na Azory Gwanda kupotea kwamba sasa waandishi wa habari wote hatufanyi kazi kwa amani tumejawa na hofu. Mimi naomba kuuliza vitendo hivi vya waandishi wa habari kukutana na matukio ya kunyanyaswa vimeanza leo? Ni wakati gani waandishi wa habari hawakunyanyaswa? Ni Tanzania tu ndio haya yanatokea? Nadhani majibu mnayo.

Balile na wenzako TEF mnazungumza kuwa vyama vya siasa vinanyimwa haki ya kufanya mikutano. Hivi jamani ni mwandishi wa habari gani kawatuma mtoe tamko hili? Mimi hapa na mkutano wa chama cha siasa wapi na wapi? Ningeelewa zaidi kama Balile na wenzako mngetumia nguvu zenu kutoa somo kwa wanahabari namna ya kufanya kazi kwa weledi katika mikutano ya siasa iliyozuiliwa, sasa na nyinyi mmekuwa wanaharakati mnadai vyama vya siasa vinaminywa, mnataka vikafanye mikutano isiyoruhusiwa ili mtutume tukaandike habari halafu yatukute yaliyomkuta Daudi Mwangosi?

Balile na wenzako hapo TEF mnasema hali imekuwa mbaya kwamba vyombo vya habari sasa vinakosa matangazo ya biashara na mauzo ya magazeti yameshuka chini. Nilitarajia nyie ndio mngekuja na suluhisho la namna ya kukabiliana na hali ambapo fedha za matangazo ambazo vyombo vya habari vilitegemea kupata Serikalini hazipo. Nilitarajia mje mseme sasa magazeti yetu yatapatikana kwenye App ama katika mfumo ambao wasomaji watalazimika kulipia ndipo wasome, nilitarajia nyie mtakuja na msaada wa namna gani matangazo ya televisheni na redio yahamie kwenye kulipia kama ilivyo kwa Azam Media ili kuwe na kipato cha kuwalipa waandishi wa habari vizuri?

Mnataka kulazimisha Serikali itoe hela za matangazo? Hivi TEF hamjifunzi vyombo vya habari vya nchi za wenzetu vinaendeshwaje? Hivi taaluma yetu si ndio inatufundisha juu ya mgongano wa maslahi, sasa mnapotaka vyombo vya habari viendeshwe kwa kutegemea Serikali hivyo vyombo vitakuwa na uhuru gani wa kuikosoa? Labda hili la vyombo vya habari kuidai Serikali linaweza kueleweka lakini pia sidhani kama ilikuwa sawa kuja kulimwaga kwenye mkutano na waandishi wa habari kwa sababu wanaoidai Serikali ni wengi na inawezekana hiki kinachodaiwa na vyombo vya habari ikawa ni kidogo. Na pia ningetarajia jambo hili litolewe tamko na wamiliki wa vyombo vya habari sio nyinyi TEF.

Ndugu zangu njooni na solution sio kuja kulalamika. Halafu hebu kuweni wakweli hata kabla ya nyakati hizi ni wakati gani waandishi wa habari walikuwa na malipo mazuri na hali nzuri kazini? Tena nyie wenyewe wahariri ndio mmekuwa wa kwanza kuwashawishi wamiliki wa vyombo vya habari wawalipe waandishi shilingi 1,750/= kwa habari inayotumwa gazetini, yaani mwandishi wa habari anaitafuta habari tena kwa kusafiri kwa gharama kubwa na mwisho wa siku malipo yake ni shilingi 1,750/=, nyinyi wenyewe wahariri ndio ambao mnapokea habari kutoka kwa waandishi wa habari ambao hawana mishahara, hawana ajira, hawana mikataba ya kazi na hata hawana mafao yoyote. Na haya mambo hayajaanza leo.

Waandishi wa habari wanafariki dunia, tunaishia kuchangisha fedha ili kununua hadi chakula cha watu waliopo msibani. Lakini nyie TEF hata siku moja hatujawaona mkiwabana hao wamiliki wabebe majukumu ya kuhudumia wafanyakazi wao wanapoumwa ama kifo.

Na niwe mkweli hii tabia ya TEF kukurupuka acheni. Mlikurupuka wakati wa mgogoro wa Ruge Mutahaba wa Clouds Media na Paul Makonda – Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na mwisho wake ukawa ni aibu na leo mmekurupuka tena hivyohivyo.

Kwenye mgogoro wa Ruge na Makonda mlipokuruka, na kama kawaida yenu tukawaona mnaungwa mkono na wanasiasa wa UKAWA na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na leo tena mnapita humo, mnatufanya waandishi wa habari wa nchi hii tuonekane ni wapinzani wa Serikali wakati haya ni mambo yenu nyinyi. Hata habari mnazozipa umuhimu kwenye nyombo vyenu zinakuwa na mwelekeo huo huo wa kuunga mkono UKAWA, ndio maana leo mmesababisha waandishi wa habari tunakuwa wanyonge mbele ya Serikali, hatuaminiki kwa sababu yenu.

Najua baada ya kuandika maoni yangu haya mtakuja kusema sijui katiba ya TEF na nimeandika takataka lakini nataka niwaambie turudi kwenye misingi yetu, acheni kutupeleka kwenye mwelekeo unaoharibu taswira ya tasnia hii ya habari. Msituingize kwenye siasa, hii ni taaluma inayoheshimika duniani kote. Inawezekana nyie mna maslahi yenu lakini ndani ya tasnia hii tumo ambao tunategemea kalamu na weledi wetu, msituyumbishe na msitugombanishe na Serikali.

Na ifike mahali vyombo hivi vinavyowahusu waandishi vipate sura mpya. Nampongeza sana Mkongwe Teophil Makunga kwa uamuzi wake wa kujiuzulu uenyekiti wa TEF, inawezekana kuna sababu lakini nadhani ni muhimu tansia hii ianze kuona demokrasia ya kuwa na sura mpya kwenye vyombo vinavyosimamia, hapa nina maana ya TEF, Baraza la Habari (MCT), Umoja wa vyama vya waandishi wa habari (UTPC) na vingine. Sio kila siku ni wale wale tu akina Meena, Balile na wenzenu. Tunao watu wengine wazuri.

Mwisho nawaomba viongozi wa Serikali mtambue kuwa tamko lilisomwa na TEF ni la wahariri wanaounda uongozi wa TEF, halituhusu waandishi wa habari tulio wengi na ambao tunaendelea kufanya kazi zetu kama kawaida. Tuendelee kushirikiana kama kawaida kuijenga Tanzania yetu ambayo kwa sasa duniani kote inasifika kwa kuwa na kiongozi Mhe. Rais John Pombe Magufuli ambaye ni mfano bora wa kuigwa barani Afrika kwa juhudi zake za kutetea wanyonge, kupigania rasilimali za nchi, kupiga vita rushwa, kubana matumizi yasiyo ya lazima, kujenga viwanda na kujenga uchumi imara wa kutupeleka katika kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.

Mwandishi wa habari niliyetoa maoni haya naishi Dar es Salaam na nimekuwa katika uandishi wa habari kwa miaka 18 sasa. Sijataka kutaja jina langu kwa sababu sitaki ninyooshewe kidole na yeyote hasa ikizingatiwa hulka za jamaa zangu akina Balile, Meena na wenzake nazijua.

Soma: Jukwaa la wahariri(TEF) walia juu ya kuminywa uhuru wa habari, utekaji na mauaji nchini
 
Sawa tuache siasa za upinzani pembeni. Nini msimamo/tamko lako juu ya kupotea mwanahabari Azory ? Au kutekwa kwa yule mwandishi wa Makambako, unaelezeaje ? Maana wewe kama Kitila mnakosoa tu njia inayotumika bila kugusia maudhui ya matamko husika
 
The List huita "rubish"empty set. Ameshindwa kuunganisha wajibu wa waandishi kwa jamii na kwao binafsi tumsamehe anaogopa kutukanwa na wakulu ili ajitetee yeye hayumo.Unaona jinsi andiko lilivyojaa mashaka.Kwake kila asiyekubaliana na serikali ni ukawa.Uvivu wa kufikiri utaua kizazi hiki.
 
Kama kweli ni mwandishi wa habari na si polepole aliyeandika unafiki huo basi atakuwa mwandishi wa Uhuru!!na ndiyo maana hata waandishi wenzake wa TEF walimkwepa maana ni nuksi!! Sasa umewalaumu wao kwa kumkosoa magufuli(serikali) halafu huyu jinga amemsifia!! That means hapo wote mnafanya siasa!

Tofauti ni kuwa wenzake wanafanya siasa pana na yeye anafanya siasa tumbo!! Vyama vya upinzani vimekatazwa kufanya mikutano halali ila ccm na vibaraka wake wanaruhusiwa kufanya mikutano na makongamano nchi nzima! Eti leo wafuasi na wanachama wa upinzani wanasakwa na dola hadi misibani!!

Ukiuliza kosa lao hupati jibu! Tafsiri yake ni kuwa Wanaonewa!! Anasema uchumi unakuwa kwa 7.1% lakini anakiri kuwa biashara imeshuka(ikiwemo ya magazeti) hatuambii huo uchumi unakuwa kwenye angle ipi ila anachojua ni ku talk the talk of his breadwinners!!

Yaani mwenzako anasema kwa kuonyesha dhahiri mapungufu halafu wewe unamkemea kuwa anaingilia siasa, kisha wewe unakisifia kilekile alichokiponda mwenzako na hujishtukii kuwa na wewe umetumbukia humohumo!! Sijui serikali ina maadui wangapi hadi sasa! Maana kila siku wanaongezeka.
 
Hii ndio changamoto mojawapo ya huku JF.Ingekua ni shule ningesema tumechanganywa wanafunzi wa sekondari na msingi kwenye darasa moja na kwa pamoja tunatumia syllabus ya sekondari.

Una haki ya kutoa mawazo yako ila siafikiani nawe.
 
JUKWAA LA WAHARIRI (TEF), MNAFANYA KOSA LILELILE LILILOFANYWA NA MAASKOFU WA KKKT NA TEC

Aprili 5, 2018
Dar es Salaam.

Muda mfupi uliopita nimesikiliza Tamko la Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) kuhusu hali ya nchi yetu.

Kimsingi TEF walichokifanya hakina tofauti na kile walichokifanya Baraza la Maaskofu wa Kanisa la Kiinjilisti la Kilutheri Tanzania (KKKT) na Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), ambacho ni kuendeleza wimbo wa ajenda za kisiasa zenye mlengo wa siasa za upinzani.

Huku ni kupotoka kwa hali ya juu sana.

Niliwahi kuhoji huko nyuma juu ya uhalali na uhalisia wa TEF ambao ni mabosi au viongozi wa waandishi wa habari nikiwemo mimi. Nilihoji hivi kwa sababu nikiwa mwandishi wa habari mpaka leo sijaelewa na wala sijaeleweshwa kuhusu Jukwaa la Wahariri ambalo naamini linapaswa kuwa na uhusiano wa karibu na waandishi wa habari hasa ikizingatiwa mara zote linazungumza masuala yanayowahusu waandishi wa habari kama lilivyofanya leo.

Nasema hivyo kwa sababu TEF inatoa matamko ambayo yanabeba sura kuwa ni matamko ya waandishi wa habari wakati kiuhalisia siamini kuwa huo ndio msimamo wa waandishi wa habari wa nchi hii.

Nilikuwa nafuatilia mkutano wa TEF, nimemuona Deodatus Balile na Neville Meena wakiendesha mkutano huu, wametoa hoja nyingi ambazo kimsingi na kwa ufupi hakuna tofauti na Waraka uliotolewa na Maaskofu wa KKKT na TEC kabla ya Pasaka.

Kwa bahati nzuri nilipata kusoma barua ya Prof. Kitila Mkumbo aliyomuandikia Askofu wake Fredrick Shoo. Na katika barua hii kwa usomi na unyenyekevu mkubwa Prof. Kitila Mkumbo alieleza namna maaskofu walivyojikwaa katika waraka wao na akatoa ushauri wake kwao.

Na mimi pia naomba nifanye hivyohivyo kwenye nyie Maaskofu wangu yaani Jukwaa la Wahariri na kwa kweli nikulenge wewe Kaimu Mwenyekiti wa TEF Deodatus Balile ambaye umelisoma tamko la TEF.

Ndugu Balile tamko lenu linatuletea maswali mengi kwenye jamii na hasa Serikali ambayo ni sehemu muhimu ya kazi zetu za kila siku. Mimi nikiwa mmoja wa waandishi wa habari ambao hawajashirikishwa na wala hawajawahi kushirikishwa kwenye masuala ya TEF limenikwaza kwa sababu wadau ambao nafanya nao kazi kwa karibu ni Serikali ambayo kimsingi tamko lenu linaituhumu kwa mambo mazito yenye vinasaba vya siasa za upinzani.

Nilitarajia kwa dhamana ambayo TEF imebeba ingefanya utafiti wa kutosha kabla ya kuandika tamko hili na kuja kulisoma kwa waandishi wa habari, nilitarajia waandishi wa habari tungejulishwa kupitia vyama vya waandishi wa habari wa mikoa (Press Clubs) ama kupitia Umoja wa Vyama vya Waandishi wa Habari (UTPC) ama ikishindikana kupitia vyombo vyetu vya habari, kuwa kuna tamko hili zito litatolewa kuhusu sisi.

Badala yake Balile na wenzako akina Neville Meena mmekaa na kwa mawazo yenu, hisia zenu na malengo yenu mkaamua kuandika mlichoandika na kisha kwenda kukisoma kwenye mkutano wa vyombo vya habari, mkibeba sura ya Tamko la Jukwaa la Wahariri wakati ndani yake mnazungumza kwa niaba ya waandishi wa habari.

Sasa twende hoja kwa hoja, mosi, mnasema kuna sintofahamu katika hali ya uchumi, mnazungumza hilo kwa kuzingatia nini? Maana takwimu zinaonesha hali ya uchumi wa nchi yetu ni nzuri? Takwimu za hivi karibuni zinaonesha kuwa uchumi wetu umepanda na sasa unakua kwa asilimi 7.1 kutoka 6.8, mfumuko wa bei umeshuka hadi asilimia 4.5, nchi yetu ni kati ya nchi 5 zenye kasi kubwa ya kukua kwa uchumi barani Afrika.

Takwimu za Benki Kuu (BOT) zinaonesha nchi ina akiba ya fedha za kigeni zaidi ya Bilioni 5 za kutosha kuagiza bidhaa na huduma kwa miezi 6 na Rais kasema fedha za kutekelezea miradi mikubwa ya reli, kununua ndege, barabara, maji, ujenzi wa viwanja vya ndege, elimu bure, kujenga flyover, kujenga bandari, kununua dawa za hospitali na mengine, zipo. Rais kasema Serikali ina fedha za kulipa mishahara wafanyakazi na haikopi katika mabenki ya biashara kama ilivyokuwa zamani. Sasa nyie mnazungumza sintofahamu ya kutoka wapi?

Balile na wenzako mnasema kuna sintofahamu ndani ya jamii kwa sababu uhuru wa kutoa maoni unaminywa ukiwemo uhuru wa vyombo vya habari, labda niulize wewe Balile gazeti lako la Jamhuri na mambo mazito linayoyaandika kila toleo ni mahali gani umeminywa uhuru wako? Au nimuulize Meena makala anazoandika kila siku kwenye magazeti mbalimbali likiwemo Mwananchi, na jinsi zinavyoikosoa Serikali ni lini uhuru wake umeminywa? Au Mwandishi wa habari mkongwe Jenerali Ulimwengu na vijana wake akina Ezekiel Kamwaga jinsi wanavyotumia gazeti lao la Raia Mwema kuandika mambo mazito ya kuikosoa Serikali ni wapi uhuru wao unaminywa? Chukua magazeti ya leo Mwananchi, Tanzania Daima, Nipashe, Mtanzania kwa kutaja machache soma na angalia kuna habari ngapi zinaikosoa Serikali, umesikia yameminywa? Ipo mifano mingi.

Nilitarajia wewe Balile kwa elimu yako ya sheria ungekuwa mwalimu pale ambapo waandishi wa habari wanadhani wana haki ya kuandika chochote tu bila kutambua kuwa wana wajibu wa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni mbalimbali zilizopo hapa nchini na pia kuzingatia weledi katika taaluma hii ya uandishi wa habari.

Ningeelewa zaidi kama TEF katika tamko lenu mngesema pia kuhusu makosa ya dhahiri ambayo vyombo vya habari vinayafanya na mara kwa mara tunasoma Mkurugenzi wa Maelezo Dk. Hassan Abbas anavionya na vinaomba radhi.

Balile na wenzako mnasema vyombo vya habari vinafungiwa na kutozwa faini. Sasa mlitaka vikikiuka sheria iwaje? Na kama hakutakuwa na adhabu hizo sheria zimetungwa za nini? Na hapa tuwe wakweli vyombo vya habari vilivyofungiwa vinafahamika na makosa yake hutajwa. Na kwa sisi waandishi wa habari tunajuana na tunajua uhalali wa vyombo hivyo kufungwa, kwa nini hatujiulizi kila wakati ni vyombo vilevile tu?

Hivi Balile na wenzako kwenye TEF mnataka kutuaminisha kuwa Magazeti ya Mwanahalisi na Mawio hayakustahili kufungiwa? Gazeti la Tanzania Daima ambalo limemaliza kifungo chake na ambalo Neville Meena aliwahi kuwa Mhariri wake halikustahili kufungiwa kwa makosa yale?

Hivi Ansibert Ngurumo aliyekuwa Mhariri mmojawapo wa Mwanahalisi na MAwio na ambaye kwa sasa ametengeneza drama ya kujifanya kakimbilia uhamishoni nchini Finland ndivyo mnataka waandishi wa habari wa Tanzania tuwe hivyo? Mnakiona anachokifanya Ansibert Ngurumo akiwa huko Finland au mmefumba macho hamsomi maandiko yake kwenye mitandao ya kijamii?

TEF mmebeba ajenda nyingine ya siasa za upinzani ambayo hata Mwenyekiti wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe kaisema tena jana wakati akitoka rumande Segerea kuwa demokrasia imezorota, mmepima wapi kuwa demokrasia imezorota? Kaizorotesha nani? Au mnamhoji nani kiasi cha kutaka Rais Magufuli akutane na hao mnaosema ni makundi mbalimbali?

Hoja hizi ni za wanasiasa wa upinzani kabisa ambao wanapambana kuingia Ikulu leo mnataka kuzibeba nyie TEF? Kama ni kukutana na makundi mbona Rais anakutana nayo? Amekutana na waandishi wa habari na wakauliza maswali hadi yakaisha, amekutana na wafanyabiashara wameuliza maswali mpaka yakaisha, hukuna na viongozi wa dini na huzungumza nao, hukutana na wanasiasa na huzungumza nao na taarifa za Ikulu zinakuja. Labda mseme mlitaka akutane na akina nani? Na kama ni hivyo basi muda bado upo, Rais ana miaka miwili na sasa kauanza wa tatu kati ya miaka mitano ya kuwa kwake madarakani.

Yaani ndugu zangu Wahariri mnatuvalisha joho ambalo waandishi wa habari hatustahili kabisa. Maanda haya mnayoyaandika ndio nyimbo za vyama vya siasa vya upinzani vinavyounda Umoja wa Katiba ya Watanzania (UKAWA), nyimbo za akina Mange Kimambi na Evarist Chahali. Yaani mnafikia mahali mnataka kutuweka waandishi wa habari wa nchi kwenye kundi moja na Mange Kimambi?

Kwenye tamko lenu mmechukua tukio la mwandishi wa habari kupokonywa simu na polisi huko Dodoma na Azory Gwanda kupotea kwamba sasa waandishi wa habari wote hatufanyi kazi kwa amani tumejawa na hofu. Mimi naomba kuuliza vitendo hivi vya waandishi wa habari kukutana na matukio ya kunyanyaswa vimeanza leo? Ni wakati gani waandishi wa habari hawakunyanyaswa? Ni Tanzania tu ndio haya yanatokea? Nadhani majibu mnayo.

Balile na wenzako TEF mnazungumza kuwa vyama vya siasa vinanyimwa haki ya kufanya mikutano. Hivi jamani ni mwandishi wa habari gani kawatuma mtoe tamko hili? Mimi hapa na mkutano wa chama cha siasa wapi na wapi? Ningeelewa zaidi kama Balile na wenzako mngetumia nguvu zenu kutoa somo kwa wanahabari namna ya kufanya kazi kwa weledi katika mikutano ya siasa iliyozuiliwa, sasa na nyinyi mmekuwa wanaharakati mnadai vyama vya siasa vinaminywa, mnataka vikafanye mikutano isiyoruhusiwa ili mtutume tukaandike habari halafu yatukute yaliyomkuta Daudi Mwangosi?

Balile na wenzako hapo TEF mnasema hali imekuwa mbaya kwamba vyombo vya habari sasa vinakosa matangazo ya biashara na mauzo ya magazeti yameshuka chini. Nilitarajia nyie ndio mngekuja na suluhisho la namna ya kukabiliana na hali ambapo fedha za matangazo ambazo vyombo vya habari vilitegemea kupata Serikalini hazipo. Nilitarajia mje mseme sasa magazeti yetu yatapatikana kwenye App ama katika mfumo ambao wasomaji watalazimika kulipia ndipo wasome, nilitarajia nyie mtakuja na msaada wa namna gani matangazo ya televisheni na redio yahamie kwenye kulipia kama ilivyo kwa Azam Media ili kuwe na kipato cha kuwalipa waandishi wa habari vizuri?

Mnataka kulazimisha Serikali itoe hela za matangazo? Hivi TEF hamjifunzi vyombo vya habari vya nchi za wenzetu vinaendeshwaje? Hivi taaluma yetu si ndio inatufundisha juu ya mgongano wa maslahi, sasa mnapotaka vyombo vya habari viendeshwe kwa kutegemea Serikali hivyo vyombo vitakuwa na uhuru gani wa kuikosoa? Labda hili la vyombo vya habari kuidai Serikali linaweza kueleweka lakini pia sidhani kama ilikuwa sawa kuja kulimwaga kwenye mkutano na waandishi wa habari kwa sababu wanaoidai Serikali ni wengi na inawezekana hiki kinachodaiwa na vyombo vya habari ikawa ni kidogo. Na pia ningetarajia jambo hili litolewe tamko na wamiliki wa vyombo vya habari sio nyinyi TEF.

Ndugu zangu njooni na solution sio kuja kulalamika. Halafu hebu kuweni wakweli hata kabla ya nyakati hizi ni wakati gani waandishi wa habari walikuwa na malipo mazuri na hali nzuri kazini? Tena nyie wenyewe wahariri ndio mmekuwa wa kwanza kuwashawishi wamiliki wa vyombo vya habari wawalipe waandishi shilingi 1,750/= kwa habari inayotumwa gazetini, yaani mwandishi wa habari anaitafuta habari tena kwa kusafiri kwa gharama kubwa na mwisho wa siku malipo yake ni shilingi 1,750/=, nyinyi wenyewe wahariri ndio ambao mnapokea habari kutoka kwa waandishi wa habari ambao hawana mishahara, hawana ajira, hawana mikataba ya kazi na hata hawana mafao yoyote. Na haya mambo hayajaanza leo.

Waandishi wa habari wanafariki dunia, tunaishia kuchangisha fedha ili kununua hadi chakula cha watu waliopo msibani. Lakini nyie TEF hata siku moja hatujawaona mkiwabana hao wamiliki wabebe majukumu ya kuhudumia wafanyakazi wao wanapoumwa ama kifo.

Na niwe mkweli hii tabia ya TEF kukurupuka acheni. Mlikurupuka wakati wa mgogoro wa Ruge Mutahaba wa Clouds Media na Paul Makonda – Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na mwisho wake ukawa ni aibu na leo mmekurupuka tena hivyohivyo.

Kwenye mgogoro wa Ruge na Makonda mlipokuruka, na kama kawaida yenu tukawaona mnaungwa mkono na wanasiasa wa UKAWA na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na leo tena mnapita humo, mnatufanya waandishi wa habari wa nchi hii tuonekane ni wapinzani wa Serikali wakati haya ni mambo yenu nyinyi. Hata habari mnazozipa umuhimu kwenye nyombo vyenu zinakuwa na mwelekeo huo huo wa kuunga mkono UKAWA, ndio maana leo mmesababisha waandishi wa habari tunakuwa wanyonge mbele ya Serikali, hatuaminiki kwa sababu yenu.

Najua baada ya kuandika maoni yangu haya mtakuja kusema sijui katiba ya TEF na nimeandika takataka lakini nataka niwaambie turudi kwenye misingi yetu, acheni kutupeleka kwenye mwelekeo unaoharibu taswira ya tasnia hii ya habari. Msituingize kwenye siasa, hii ni taaluma inayoheshimika duniani kote. Inawezekana nyie mna maslahi yenu lakini ndani ya tasnia hii tumo ambao tunategemea kalamu na weledi wetu, msituyumbishe na msitugombanishe na Serikali.

Na ifike mahali vyombo hivi vinavyowahusu waandishi vipate sura mpya. Nampongeza sana Mkongwe Teophil Makunga kwa uamuzi wake wa kujiuzulu uenyekiti wa TEF, inawezekana kuna sababu lakini nadhani ni muhimu tansia hii ianze kuona demokrasia ya kuwa na sura mpya kwenye vyombo vinavyosimamia, hapa nina maana ya TEF, Baraza la Habari (MCT), Umoja wa vyama vya waandishi wa habari (UTPC) na vingine. Sio kila siku ni wale wale tu akina Meena, Balile na wenzenu. Tunao watu wengine wazuri.

Mwisho nawaomba viongozi wa Serikali mtambue kuwa tamko lilisomwa na TEF ni la wahariri wanaounda uongozi wa TEF, halituhusu waandishi wa habari tulio wengi na ambao tunaendelea kufanya kazi zetu kama kawaida. Tuendelee kushirikiana kama kawaida kuijenga Tanzania yetu ambayo kwa sasa duniani kote inasifika kwa kuwa na kiongozi Mhe. Rais John Pombe Magufuli ambaye ni mfano bora wa kuigwa barani Afrika kwa juhudi zake za kutetea wanyonge, kupigania rasilimali za nchi, kupiga vita rushwa, kubana matumizi yasiyo ya lazima, kujenga viwanda na kujenga uchumi imara wa kutupeleka katika kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.

Mwandishi wa habari niliyetoa maoni haya naishi Dar es Salaam na nimekuwa katika uandishi wa habari kwa miaka 18 sasa. Sijataka kutaja jina langu kwa sababu sitaki ninyooshewe kidole na yeyote hasa ikizingatiwa hulka za jamaa zangu akina Balile, Meena na wenzake nazijua.

Hizi profffesional boards za Tanzania zote crap.
Wamesahau kazi zao wanasiasa wamewatawala.
Ukiwa na mayegemeo flani akili yote inachanganyikiwa ukikosa.
 
Sijasoma andiko lako lote but am so sorry to say this.... LIMEJAA UPUUZI NA UPUMBAVU MWINGI.. ningekuwa na muda wa kulisoma lote ningelijibu kwa kirefu lakini kwa machache niliyoyasoma bandiko lako linajiakisi wazi muktadha wake... Tumika upate kula yako lakini Kumbuka madhila ya wengine na dhima ya kalamu yako.... Kesho ipo..!!! Usisahau
 
Back
Top Bottom