Jukwaa la Wahariri(TEF),mnafanya kosa lile lile lililofanywa na Maaskofu wa KKKT na TEC

Tumsamehe tu... sasa tufanyeje? hamna cha kumsaidia.... Lost child!!! Hahahaha
 
Kila mtu waraka waraka. Kutoa waraka halafu haufanyiwi kazi sawa sawa kupotezeana muda tu.
 
Wewe unadai ni muandishi na si mhariri,kwanini ushirikishwe katika mambo yasiyokuhusu. Umeamua kujitoa ufahamu na kutaka kulazimisha mtizamo ambao ungekufurahisha? Try to be realistic japo kwa mara moja. Pole kwa kubaini kuwa kuna makundi mengi yanye mtizamo unaokinzana na wa kwako.
 
Tusichanganye kusema ukweli na kile kinachoitwa kukosoa, huku lugha inayotumika ni ya kejeli, kebehi, na matusi. Ukweli kusemwa au kukosoa serikali ni kwa kutumia majukwaa ya kikatiba na siyo kwa kutoa matamko na nyaraka.

Majukwaa hayo ni vikao vya Serikali za vijiji, Mitaa, Hamashauri, Bunge na Mahakama. Lakini pamoja na majukwaa hayo, wastarabu, kupitia vyama vyao vya kiataaluma au kijamii, wana nafasi ya kujadiliana na Serikali yanayogusa mambo yao, km mikutano ya Rais na wawekezaji, wafanya biashara na hata waandishi wa habari.

Kuhararisha mikutano ya hadhara ili viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani kupanda majukwaani kupandikiza sumu ya chuki baina yetu, siyo demokrasia katu.
Jaribu kutumia akili japo kidogo,mambo ya kuendeza tumbo at times itakulazimu kujidhalilisha ili mkono uende kinywani.
 
kwa urefu wa andiko hili huna sifa ya kuwa mwandishi wa habari, maana unatumia nguv nyingi saana ili ueleweke,
 
Nyaraka ndio imekuwa habari ya mjini, kila kundi na waraka wake, hadi zinapoteza hata maana.
Watu wanatafuta kick kupitia nyaraka siku hizi.

Wengine wanakuja....
 
Huyu mwandishi sijamwelewa,ana msinamo gani,hebu na wewe andika waraka uwape hao unaosema hawakukushirikisha
 
Sasa nimefarijika kumbe kuna waandishi wanaojitambua.
Nashukuru umejibu kwa hoja tena zilizoshiba. Kuna kitu kiko wazi, hawa wahariri walizoea kupewa bahasha na serikali kwa awamu zilizopita. Ndiyo yalikuwa maisha yao. Angalieni mfano wa tukio la aibu la hivi karibuni walivyopewa bahasha na TFF ili wafunike na kupindisha suala la Wambura.
Badala ya kutumia akili kukabiliana na hali iliyopo, wanakimbilia kumshambulia Mh Rais, haisaidii.
 
Story yako kwanza inachosha ! Mungu ipo siku atawafanya munene kwa lugha moja
 
Tunataka uhuru wa kujieleza lakini hata humu hatu practice uhuru wa maoni, halafu tunaisema serikali inaminya.

Hawa ndo wangekuwa wanaongoza serikali, hali ingekuwa mbaya sana.

Ili tuwe viongozi bora wa baadaye, tujifunze kuheshimu maoni ya watu wengine. mnataka wote tuunge mkono hizo waraka zinazotokewa kwa nini.
 
Na wewe una maslahi binafsi kama kitila kitila analinda tumbo lake kwa sasa na anafanya kila awezalo apandishwe cheo.sasa wewe ni mhariri wakuite ama unatafuta kiki
Je unashiliki vikao wewe si wandishi wa kawaida ukatafute nini kwa wahariri usifikilie kwa kutumia tumbo lako tumia akili uokoe kizazi kijacho pole kwa familia na wazazi waliolusomesha wakazani utaleta jambo jipya elimu yako haikusaiidii na pia siamini kama ni mwandishi wewe
 
Egnecious Maaskofu wa katoliki wamesema, na kushauri, haujajibu hoja zao kama zina ukweli au hazina ukweli, umeishia kuwalaumu kuwa hoja zao zinafanana na hoja za Ukawa.

Maaskofu wa KKKT wameshauri na kuonya, haujajibu kile walichokisemea kina ukweli au ni uongo, umeishia kuwalaumu kuwa hoja zao zinafanana na zile za Ukawa.

Jukwaa la wahariri limetoa maoni juu ya kinachoendelea nchini, na kushauri hatua za kuchukua ili kuepuka hatari tuiendeayo, unasema hoja zao zinafanana na hoja za ukawa.

Nadhani wewe unachotaka ni kusikia unachokipenda hata kama hakina ukweli, kwa sababu ya kweli yote kwa sababu tu yamesemwa na hao Ukawa hutaki kuyasikia,(kuna unachokitafuta au unachokilinda).

Kwa mazingira ya sasa ni muhimu ukajua kwamba, kinachiwapata wengine kinaweza pia kukupata wewe, kama kweli wewe ni mwandishi wa habari, huwezi kutetea kupotea kwa mwandishi mwenzako, tena katika mazingira yaliyoelezwa na mkewe, huwezi kunyamazia kilichompata Masoud kipanya, kwa sababu tu ya kujitafutia kupendwa na unaowatumikia, kuwa mkweli.

Amini nakwambia, itafika wakati, utakapofikiwa wewe hautakuwa na wa kukusemea, kwa sababu wote watakaopaswa kukusemea, watakuwa wameshughulikiwa, hivyo itakuwa rahisi zaidi kukushughulikia wewe kwa kuwa utakuwa peke yako!
Ni swala la wakati tu, kila la kheri katika upofu wa fikra zako.
 
Of course hapa ni vita ya nuru dhidi ya giza. Wema dhidi ya uovu. Upande wa uovu pia unawatetezi. Hawa hawaogopi hata viongozi wa dini
Wa kumwogopa ni MUNGU tu. Hao viongozi ni binadamu kama wewe. Wengine wana mapungufu makubwa kuliko wewe
 
Back
Top Bottom