Jukwaa la Wahariri(TEF),mnafanya kosa lile lile lililofanywa na Maaskofu wa KKKT na TEC

Wanazungumza kitu sahihi kama hakuna utu mtathamini madaraja na Reli mnayohenga ikiwa watu kuuawa mnataka iwe kawaida...Popote pale binadamu ndio anathaminiwa kuliko vitu maana vitu vipo na vinapatikana...
 
Egnecious
1. Sasa wewe umeandika hili "tamko" ukimwakilisha nani ? Kama unajiwakilisha mwenyewe, kwa maana maoni yako binafsi, then uko sahihi kwa sbb hayo ni maoni yako binafsi, ni vionjo vya hisia zako!!

2. Unasema walishokisema kinashabihiana na kisemwacho na vyama vya upinzani, waraka wa KKKT na TEC.

Sasa kama huo ndiyo uhalisia wa mambo ktk jamii ? Hivi unaweza kuona tikiti maji jeusi pale ukasema hilo ni "tako la nyani" mbele za watu na watu hao wakakuelewa na kukuamini ?

Je, si kwamba watakuona wewe ni mwendawazimu fulani hivi ? Sasa hii ndiyo maana yako hapa kwa hawa watu. Ulitaka waseme tofauti na uhalisia huo wauonao ili kufurahisha nafsi na unaowaunga mkono....

Nadhani unachopaswa kufanya wewe ni aidha ni ukubaliane nao au upingane nao jambo ambalo ni la kawaidà miongoni mwa binadamu wenye maono na mitazamo tofauti.

Ndiyo maana wewe unaamini matamko na takwimu za Magufuli na serikali yake bila kihoji.

Matamko na takwimu ambazo hazi reflect hali halisi miongoni mwa wananchi, miongoni mwa jamii wanaoingoza....


3. Kutofautiana kimaono na kimitazamo juu ya mambo ama jambo fulani sio dhambi. Ni kawaida kabisa na ni afya. Ni mitazamo tofauti tofauti inayokinzana ndiyo hutupeleka kwenye hatua za mbele za kimaendeleo....

Wapinzani kama ulivyowaita wewe ni watu. KKKT na TEC na TEFF nao ni watu. Wanayatazama mambo ktk namna tofauti na unavyoyatazama wewe ama anavyoyatazama Magufuli na serikali. Hili sio kosa.

Lililo muhimu jiulizeni kwa nini hawa hawaoni mambo yako sawa sawa na serikali ama hata John Pombe Magufuli aonavyo... ? Baada ya hapo ni sharti kufanya mambo kwa utofauti ili watu waone na kuwashawishi kuwaunga mkono.

Kinyume chake, hatutaona na tutawakosoa na kusema tu. Sasa kama mtawalazimisha watu kwa kutumia bunduki na risasi za moto kukubaliana na serikali, na iwe hivyo ili tuone tutafika wapi....

Jamii ndiyo inayoweza kuamua ni nani mkweli na ni nani is Just making up things na itaamua ili hakuna sheria iliyovunjwa ktk kutoa mawazo ama maoni yoyote.....!!
 
Hizi ndizo zile kelele ambazo Mwalimu Nyerere aliongelea kwa namna ya unabii.

Kwamba watakuwa wanasema huyoo huyoo huyoo, wewe usigeuke nyuma chapa mwendo kwa kwenda mbele.

JPM anachapa kazi, anapiga mzigo wa kufa wa mtu, hawa kina Balile na Meena ni binadamu tu, ambao pengine wanayo bei inayofahamika kwa matajiri fulani wachache.
 
Kwamba maaskofu walikosea ni maoni ya kujihami kwa vitendo dhalimu. Maaskofu hukemea matendo yanayoenda kinyume na ubinadamu au mapenzi ya Mungu kwa mwanadamu.
 
Umesema kweli, walichosahau TEF ni kuwa wao ni marefarii wanapaswa kuwa katikati.

Hatutaki kujua maoni yao tunataka habari toka kwao.

Kama basi kwamfano limepata ajari limeua watu 12 tuambie limeua watu 12 hicho ndicho tunachotaka. Sio useme kwanamna ajari ilivyokuwa ilipaswa kuua watu 100 lkn nashangaa imeuakidogo tu no hilo silo tunalotaka.

Baada ya msimamo wenu hatutegemei zuri la serikali lisemwe na nyie wenye mtizamo mbaya juu ya nchi yenu wenyewe.
 
Kwamba maaskofu wanafanya makosa kukemea dhambi za viongozi hadharani, wakati huohuo wanapokemea dhambi za waumini hadharani hawakosei kwani injili haiwahusu viongozi? Kuminya demokrasia, mauaji na utekaji siyo dhambi zinazopaswa kukemewa na maaskofu? Barua za kichungaji kama huo waraka wa maaskofu zichukuliwe kama sehemu ya injili na mahubiri. Mtume Paulo aliziandika nyingi sana na zilikuwa na maudhui mengi ya namna hiyo.
 
Kuna mtu alikuzuia usiende shule? Si uliamua mwenyewe! Wenzako waliweka makalio yao kwenye viti ndiyo maana wanakula milo mitatu kwa siku na kuweza kusoma walaka huu mrefu.
kwa uandishi huo Kati yake na wewe nani hajaenda shule? jaribu kuficha ujinga wako japo kwa dakika
 
Sasa nimefarijika kumbe kuna waandishi wanaojitambua.
Nashukuru umejibu kwa hoja tena zilizoshiba. Kuna kitu kiko wazi, hawa wahariri walizoea kupewa bahasha na serikali kwa awamu zilizopita. Ndiyo yalikuwa maisha yao. Angalieni mfano wa tukio la aibu la hivi karibuni walivyopewa bahasha na TFF ili wafunike na kupindisha suala la Wambura.
Badala ya kutumia akili kukabiliana na hali iliyopo, wanakimbilia kumshambulia Mh Rais, haisaidii.
Trauma mwingine ktk taifa
 
Egnecious Kwa nini ufikirie ni kupotoka, badala ya kufikiria kujadiriana ili kuondoa kasoro zisemwazo hatimaye tufikie Muafaka kwa manufaa ya Taifa letu, sidhani kumuona kila anayesema kinyume au kukosoa ni msaliti, ni mkosaji na anastahili adhabu, wasikilizwe badala ya kufikiria kuwanyamazisha kwa namna yeyote hilo litakuwa kosa kubwa kuliko wanavyoonekena wao na matokeo yake si mazuri. Tuipende nchi yetu, kwa kukosoana na kusahihishana kwa upendo
 
Je, Prof. Kitila Mkumbo alipotoa ushauri wake kuhusu Waraka wa Maaskofu, alificha jina lake ?
Huyu ni Musiba mrithi wa Muro na Mtikila na gazeti lake .nimejua kutokana na inayo sema( sisi wengine tunafanya kazi na serikali )hii ni kauli ya musiba yeye afanyiagi umma kazi kupata habari bali serikali .huyu sio mzima kabisa
 
Mwisho nawaomba viongozi wa Serikali mtambue kuwa tamko lilisomwa na TEF ni la wahariri wanaounda uongozi wa TEF, halituhusu waandishi wa habari tulio wengi na ambao tunaendelea kufanya kazi zetu kama kawaida.
Hutaki wahariri WAKUSEMEE lakini wewe unataka UWASEMEE waandishi wengine. U great thinker uko wapi hapo? Kwa nini usiombe watanzania watambue bali unawaomba serikali itambue?
 
Back
Top Bottom