Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,866
- 4,252
Habari za Jumatatu
Moja kwa moja kwenye mada ni kwamba nimekuwa nafuatilia tamthilia hii bila kufuata mtiririko. Ila siku za karibuni nimeifuatilia bila kupenda kwa kuwa nilikuwa nabembelezwa nitoe remote na kubadili chaneli. Hivyo wakati nasubiria tamthilia iishe, ilibidi kutazama ndipo niendelee na program zangu.
Changamoto ni kwamba ni tamthilia iliyojaa ufuska mno, tena wa wazi. Kila tukio ni stori za ngono. Wanahamasisha usaliti bila hofu. Hata kama mwisho ungekuwa tofauti na matarajiio, kwamba hao mafuska wamepata juakali, bado wameshatenveneza dameji. Wameshafundisha watu, haswa wanawake zetu mbinu za kuchepuka. Na kwamba hakuna baya kwenye usaliti. Ni ujanja wako tu kuhakikisha unakuwa janja janja kukwepa kushikwa.
Sasa mbaya zaidi ni juzi hapa wale wazinzi wawili walipopata kiota cha kufanyia uchafu wao, yule dogo alifanya ishara ya msalaba kushukuru kwamba anafanikisha kumla mke wa mtu. Yani alimshukuru Mungu kumsaidia kufanikiwa. Ukweli niliona na nilifadhaika. Ni kufuru ya hali ya juu dhidi ya Ukatoliki na Ukristu.
Sasa Jumapili naangalia program zangu, nakumbushwa kuwa inaanza. Wakachukua remote. Kuangalia stesheni, tanthilia haipo muda huo na badala yake kuna kipindi kingine. Kama wameisimamisha ni jambo la heri. Wenzao wazungu hutangaza kabisa kuwa hii kitu ni utazame kwa uamuzi wako. Napenda kuona wanaipiga pini kabisa.
cc waziri Dr. Dorothy Gwajima