Samahani Mzee Mwanakijiji pamoja na heshima nyingi natanguliza kwanza, lakini naomba kutofautiana sana nawewe katika hili> Mh. Nassar yuko sahii kabisa katika matamshi na hata kwa wafuasi wake hawawezi kutofautiana naye kwa udogo wake ambao ni wazi hawezi kumzuia mkuu wa nchi kufanya jambo lolote ikiwemo kutembelea ndani au nje ya nchi.Amesema jambo ambalo kwa haraka linaonekana lina mantiki lakini linapuuzia uzito wa alichokisema. Kama ni mtu mdogo hivyo aligombea ubunge wa nini? Kama anakosa hekima ya kupima madhara ya maneno yake - watu wanaweza kuumia kwa kauli moja tu ya mtu mwenye ushawishi - kwa sababu yeye ni 'mtu mdogo' ananitisha. Yeye anaweza kuwa na umri mdogo lakini nguvu ya ushawishi wake inashinda baruti na siyo watu wote wanaomsikiiliza wanamchukulia kuwa ni mtu 'mdogo'. grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
ni mapema mno ku doubt uwezo wake, mpe muda wa kujifunza. kuna watu wazima wengi wenye akili na uzoefu mkubwa katika siasa waliokwishwa wahi kubwatuka kuliko huyu dogo, na hawajajifinza mpaka leo. Mimi nina imani huyu dogo ameelewa kosa lake na ataendelea kujifuza kadri anavyokua kisiasa. Tumwombee kheri kijana wetu!Naanza kudoubt uwezo wa huyu kijana umbile la mtu haligawi nchi bali maneno ya mtu.Mimi naona bora anyamaze mambo ya poe kwanza.Mbowe mwambie afyate mdomo huyu kijana.
Amesema jambo ambalo kwa haraka linaonekana lina mantiki lakini linapuuzia uzito wa alichokisema. Kama ni mtu mdogo hivyo aligombea ubunge wa nini? Kama anakosa hekima ya kupima madhara ya maneno yake - watu wanaweza kuumia kwa kauli moja tu ya mtu mwenye ushawishi - kwa sababu yeye ni 'mtu mdogo' ananitisha. Yeye anaweza kuwa na umri mdogo lakini nguvu ya ushawishi wake inashinda baruti na siyo watu wote wanaomsikiiliza wanamchukulia kuwa ni mtu 'mdogo'. grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
Huyu mtoto anaongea sana jamani si anyamaze????????????????? Mdomo ulimponza ulimi. Mbowe amemwambia bora akae kimya. Kama kukosea alishakosea.
Hapa mimi sikubaliani na wewe kabisa. Udogo anaomaanisha Nassari ni wa yeye kuigawa nchi. Najua hata wewe unajua Nassari hana uwezo wa kuigawa nchi kwa sasa. Na hana maana kwamba kila siku atakuwa mdogo. Haya maneno kayatamka leo lakini haina maana kwamba atakuwa mdogo na kesho pia
Leo baada ya mahojiano na polisi Arusha mjini zaidi ya masaa sita,Nassari akiongea na waandishi wa habari alisema "Mimi ni mdogo,kama ninauwezo wa kuigawa nchi hii basi nchi hii haikupaswa kuwepo"
Source;ITV News 2000hrs*
Hawakamatwi kwani wao wachache sana, kama wanamaanisha kweli basi hakuna Muungano kabisa.Na wale wa zanzibari
wanaotaka kujitenga vp?
Tena wanaendesha miha
dhara kila siku nao vp?
mmetoa Beretta bungeni mmeingiza SMG - By mh. lema.
Mzinga umeielewa kauli ya Nassari kweli? sidhani kama kalimaanisha udogo wa umbileNaanza kudoubt uwezo wa huyu kijana umbile la mtu haligawi nchi bali maneno ya mtu.Mimi naona bora anyamaze mambo ya poe kwanza.Mbowe mwambie afyate mdomo huyu kijana.
amejibu kifalsafa kabisaLeo baada ya mahojiano na polisi Arusha mjini zaidi ya masaa sita,Nassari akiongea na waandishi wa habari alisema "Mimi ni mdogo,kama ninauwezo wa kuigawa nchi hii basi nchi hii haikupaswa kuwepo"
Source;ITV News 2000hrs*
matusi ya lusinde ni laana kwa ccm long live nassary
Ndiyo maana hata yeye anashangaa hakujua kuwa ana nguvu ya ushawishi kiasi hicho.Amesema jambo ambalo kwa haraka linaonekana lina mantiki lakini linapuuzia uzito wa alichokisema. Kama ni mtu mdogo hivyo aligombea ubunge wa nini? Kama anakosa hekima ya kupima madhara ya maneno yake - watu wanaweza kuumia kwa kauli moja tu ya mtu mwenye ushawishi - kwa sababu yeye ni 'mtu mdogo' ananitisha. Yeye anaweza kuwa na umri mdogo lakini nguvu ya ushawishi wake inashinda baruti na siyo watu wote wanaomsikiiliza wanamchukulia kuwa ni mtu 'mdogo'. grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr
Ngoja niweke wazi kabisa; sina tatizo na kauli ya 'kujitenga'. Ni kauli ya kisiasa na imeshawahi kutolewa mara nyingi na watu wa Kigoma, watu wa Mtwara/Lindi, na hata watu wa Pemba.Binafsi hilo halinisumbui sana. Na mtu yeyote anajua aliitoa kauli hiyo kwa maana ya kuweka point ya utani ndio maana alisema "kama Sudan". Haina maana nzito ya kihivyo kwani na wengine wameshatoa kauli kama hizo.
Lakini huwezi kutoa kauli yenye kumtishia Rais na ukabakia hivihivi. Mtagundua kwamba kauli zenye kutishia maisha au usalama wa kiongozi yeyote wa umma huwa hatuzivumilii hapa kwa sababu moja kubwa - siyo watu wote wana akili zilizotulia na huwezi kujua nani akisikia anasukumwa vipi.
Nassari ni kiongozi maarufu sana sasa hivi na ameshinda kwa kishindo kikubwa sana. Kule Arusha ana mvuto mkubwa sana na ni mvuto wa watu kukesha na kumlinda hadi dakika ya mwisho. Chuki dhidi ya CCM ni chuki ya kweli (real hate) na siyo watu wote wanaweza kudumu kwenye chuki hiyo na wakiacha kwenye mambo ya kisiasa tu. Sasa, mbunge maarufu, tena kijana anaposimama na kusema anaweza kumpiga mkwara rais asikanyage Arusha siyo jambo dogo kwa sababu siyo wasikilizaji wake wote wanamuona 'mdogo hivyo'. Nassari ana ushawishi na anamvuto.
Labda watu wengi hawajui historia. Martin Luther King hakuwa na cheo chochote cha kisiasa zaidi ya kuwa mhamasishi mwanaharakati. Lakini mauaji yake yalisababisha miji ya Wamarekani kuingia katika machafuko makali sana. Ni kwa sababu watu walijua ameuawa na mikono ya watu wenye nguvu. Hata Nassari pamoja na "udogo" wake wote hakuna mtu Arusha atapenda anatendewa vibaya au kuonewa na wapo watu wanaoweza kufanya lolote kwa ajili ya utii wao. Nadhani watu wengi wameshasahu kuwa mauaji ya Arusha ya 2011 kwa kiasi kikubwa yalisababishwa na polisi kutumia nguvu dhidi ya watu ambao waliona wanaonewa.
Sasa mbunge anaposimama na kutoa kauli ambayo vyombo vya usalama vinaiona ni ya vitisho dhidi ya Rais ni kutokuwa makini kudhania tu ni jambo dogo. Alichotakiwa kusema Nassari ni hiyo kauli yake ya kwanza tu kuwa hakumaanisha ubaya wowote na kama mtu yeyote amekwazwa anaomba radhi. Lakini siyo kusema kuwa ati yeye ni mtu mdogo na asingeweza kugawa nchi; well hilil ni zaidi ya kugawa nchi. Hivi akisema kuwa Rais asikanyage na Kikwete akaamua kukanyaga na mwehu mmoja akaamua kufanya kitu kibaya kwa msafara wa rais watu watamlaumu mwehu kwa vile ni mwehu siyo? Lakini, yule mwehu ukimuuliza atasema "rais wetu" alitoa amri Kikwete asikanyage Arusha na akakanyaga!
Hii ni sababu moja ambayo inanifanya miye nisiwe shabiki sana ya hoja ya 'uongozi bora ni ujana' kwani tayari tumeshaona mengi yasiyo ya lazima ambayo vijana wameyafanya na kuthibitisha ukosefu mkubwa wa hekima na utulivu unaotokana na busara. Siyo lazima useme kila kinachoingia kichwani hata kama unaamini ni sahiihi. Kuna vingine unaweza kuvisema ila kwa namna tofauti. Hili huwezi kufundishwa shuleni au chuoni!
Ni matumaini yangu Polisi hawatoliendeleza hili na Nassari atakuwa amegundua (sidhani kwa sababu arrogance ya madaraka nayo nimbaya sana!) makosa yake. Sitaki ajisikie ameonewa bali ajue genuinely hakupaswa kutoa kauli hiyo na ni unfortunate. Kwa mfano Lema angekuwa makini na kauli zake wala asingevuliwa Ubunge! HEKIMA, HEKIMA, HEKIMA!!