Joshua Nassari apitishwa kura za maoni ya mkutano mkuu wa CHADEMA - Arumeru

chachana

Member
Aug 4, 2011
57
92
Joshua Nassari ameshinda kura za maoni za ndani ya chama na hivyo kuwa amepitishwa na mkutano mkuu wa wilaya kuwa mgombea wa ubunge jimbo la Arumeru mashariki kupitia chadema.

Nassari amepata kura 805, akifuatiwa na Anna Mgwira kura 23, Godlove Temba kura 18, Rebeca Magwisha kura 12, Samweli shami kura 10, Anthony musani kura 8 na yihane kimuto kura 6.

Taarifa ni kuwa wagombea wengine wameridhika sana na matokeo hayo, uchaguzi ulikuwa wa uwazi sana na uliendeshwa vizuri sana. Mzee Mtei Edwin ndiye aliyefungua mkutano huo.

Hivi sasa kuna shamra shamra na nderemo kubwa.

Updated 3/March/2012
[FONT=Tahoma, Calibri, Verdana, Geneva, sans-serif]
Wakuu salaam

Kamati Kuu ya CHADEMA inayokutana USA River, Meru, Arusha, katika kikao chake cha kawaida kujadili ajenda mbalimbali, leo imemteua Ndugu Joshua Samwel Nassari kuwa mgombea ubunge wa CHADEMA Jimbo la Arumeru Mashariki.

Aluta continua...mapambano yanaendelea
[/FONT]
 
sisi tumewapa Wameru chaguo lao, Majizi-CCM yanajiandaa na pingamizi, kitanuka sana safari hii na ole wenu mtakaotumia mali za umma kwenye kampeni......
 
Kamanda Joshua Nassary amewabwaga wenzake ktk kura za maoni.amepata kura 800 kati ya kura 880. ushindi huu ni wa asilimia 90.8.Tunampongeza kamanda Nassary. PEOPLESSSSSS POWERRRRRRRRR DAIMA
 
Hongera Joshua Nassary......!Hongera wagombea wote mliokuwa kwenye kinyang'anyiro!
 
Joshua Nassari ameshinda kura za maoni za ndani ya chama na hivyo kuwa amepitishwa na mkutano mkuu wa wilaya kuwa mgombea wa ubunge jimbo la Arumeru mashariki kupitia chadema.
Nassari amepata kura 805, akifuatiwa na Anna Mgwira kura 23, Godlove Temba kura 18, Rebeca Magwisha kura 12, Samweli shami kura 10, Anthony musani kura 8 na yihane kimuto kura 6.

Taarifa ni kuwa wagombea wengine wameridhika sana na matokeo hayo, uchaguzi ulikuwa wa uwazi sana na uliendeshwa vizuri sana. Mzee Mtei Edwin ndiye aliyefungua mkutano huo.

Hivi sasa kuna shamra shamra na nderemo kubwa.

Bravo cdm demokrasia iwe ndio nguzo ya chaguzi zenu. Mizengwe kama ya ccm isiwanyemelee
 
Joshua Nassari ameshinda kura za maoni za ndani ya chama na hivyo kuwa amepitishwa na mkutano mkuu wa wilaya kuwa mgombea wa ubunge jimbo la Arumeru mashariki kupitia chadema.
Nassari amepata kura 805, akifuatiwa na Anna Mgwira kura 23, Godlove Temba kura 18, Rebeca Magwisha kura 12, Samweli shami kura 10, Anthony musani kura 8 na yihane kimuto kura 6.

Taarifa ni kuwa wagombea wengine wameridhika sana na matokeo hayo, uchaguzi ulikuwa wa uwazi sana na uliendeshwa vizuri sana. Mzee Mtei Edwin ndiye aliyefungua mkutano huo.

Hivi sasa kuna shamra shamra na nderemo kubwa.

tunashukuru hakuna alionesha dalili za kutumika na Magamba, hope wangemchinjia baharini..taratibu mpinga posho mwingine ndani ya mjengo
 
Bwana mdogo sina wasiwasi naye ni mpiganaji haswa kwani ni wakazi wachache wa hapa Arusha wasiofahamu jinsi alivyochangia katika siasa za kimageuzi akiwa na Lema si arumeru tu bali hata hapa Arusha mjini. amekuwa na wakazi wa Arusha mjini nyakati zote za harakati za kuleta mabadiliko na ninaweza sema ni mwana mapinduzi wa kizazi kipya. Arumeru kazi kwao kwani ni imani yangu hawatamwangusha kwani alikuwa tayari kuwatumikia mwaka 2010 na sasa fursa imepatikana na Chadema imewarejeshea kijana wao. Tumpe ushirikiano ili alitwae jimbo kwa kishindo kwani ni dhahiri hapa CCM hawatashinda hata kama watakuja na helkopta 100
 
Ndugu Wanabodi

Kijana Joshua Nassari Amepita Kura Za Maoni Kwa Asilimia Zaidi Ya Tisini, Kuiwakilisha Chadema katika uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Arumeru mashariki.

Kura Zilizopigwa zilikuwa 888, Na Nassari Kapata 800 anaemfuatia ni Anna Mgwira 26.

Jumla wagombeaji walikuwa saba, Kwa Majina Ni;

1. Joshua Nassari
2. Anna Mgwira
3.Anthony Msami
4. Godlove Temba
5. Yohhane Kimuto
6. Samweli Shami
7. Rebbeca

Kura hizi zimepigwa leo katika ukumbi Meru Garden maeneo ya Kwa Aloisi Maji ya Chai, wagombeaji wote waloshindwa wamekubali matokeo na wana furaha tu kumuunga mkono kijana wetu Nassar

na sasa kinachoendelea ni katibu mkuu Dr. Wilbrod Slaa anaendelea kuhutubia nyomi ya wafuasi wa Chadema walofurika hapa.

habari hizi Source yake ni mimi mwenyewe niko tukioni. Picha baadae au kesho tukializa hizi pilika
 
Joshua Nassari ameshinda kura za maoni za ndani ya chama na hivyo kuwa amepitishwa na mkutano mkuu wa wilaya kuwa mgombea wa ubunge jimbo la Arumeru mashariki kupitia chadema.
Nassari amepata kura 805, akifuatiwa na Anna Mgwira kura 23, Godlove Temba kura 18, Rebeca Magwisha kura 12, Samweli shami kura 10, Anthony musani kura 8 na yihane kimuto kura 6.

Taarifa ni kuwa wagombea wengine wameridhika sana na matokeo hayo, uchaguzi ulikuwa wa uwazi sana na uliendeshwa vizuri sana. Mzee Mtei Edwin ndiye aliyefungua mkutano huo.

Hivi sasa kuna shamra shamra na nderemo kubwa.

mwanzo mzuri kama hakuna malalamiko. Kazi moja mbele ya kusambaratisha magamba kwa sera, nguvu za hoja, uwazi na ukweli wa mambo.
 
wapiga kura walikua wachache sana...

Hao ndio wanachama waliopiga kura.Ukisema wachache una maana gani?
Wameru wanakwenda shambani kulima,kukata majani ya ng'ombe na kuchanja kuni.
They were busy in other words.
 
Peoplesss power. All the best CDM. Campaign ziwe za busara sana jamani. Bwana Nassary, mwaga sera, epuka mipasho. Please make sure the victory is ours. Kila heri kamanda!!
 
Back
Top Bottom