Martin Maranja Masese apinga uteuzi wa Joshua Nassari

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,371
Hivi ndivyo watu walivyochambua na kupinga uteuzi wa Joshua Nassari kuwa Mkuu wa Wilaya.

===

Mnazikumbuka sababu ya NASSARI kuvuliwa ubunge? Nchi zenye vetting system, kwa sababu zile za Nassari kutelekeza shughuli za Bunge na akaenda kula maisha Beverly Hills, USA, akashindwa kuheshimu kanuni za bunge, asingeweza kuwa kiongozi wa serikali Lakini, ni misa ya shukrani

Spika wa bunge Job Ndugai ameandika barua kwenda kwa mwenyekiti wa NEC Jaji Semistocles Kaijage kumtaarifu jimbo la Arumeru Mashariki lipo wazi kutokana mbunge wake Joshua Nassari (CHADEMA) kupoteza sifa kuendelea kuwa mbunge. Amekosa vikao vya mikutano mitatu ya bunge mfululizo

Kwenye hilo la Nassari kufutiwa ubunge wake simlaumu Spika (kwanza-labda baadae) isipokuwa lawama naziweka hapa;

1. Ofisi ya Katibu mkuu CHADEMA
2. Josh Massari mwenyewe kama mbunge
3. Mnadhimu wa KUB (kambi ya upinzani bungeni)

Sitaki kuamini kwamba Josh Nassari alikuwa Vasco Da Gama pasi-na kutoa taarifa na kuomba ruhusa. Kama alifanya vyote basi Spika atapewa furushi la lawama.

Hilo ni kosa la kiufundi kufanywa na mbunge mzoefu aliyeingia bungeni kwa mbinde (2012) na labda alifanya makusudi (sifikiri hivyo) ili ang'olewe ubunge wake.

Kwamba Nassari Joshua hajui matakwa ya katiba ya Tanzania ibara ya 71(1)(c) au kanuni za kudumu za bunge kanuni ya 146(1)(2)

Ofisi ya katibu mkuu wa CHADEMA inapaswa kuhakikisha nidhamu ya wabunge wake inakuwa kwenye 'standards' kusimamia maadili na taratibu za kisheria kwa wabunge wake. Hii inatupa picha ya ofisi ya katibu mkuu wa CDM.

Hata kama unauguza mkeo au mzazi wako.. kuna taratibu za kibunge na katiba lazima zifuatwe kwako mbunge. Kanuni za kudumu za bunge ndio zinaongoza shughuli za bunge na wabunge. Katiba ya nchi pia. Utetezi wa Nassari ni dhaifu.

Hii ni "blunder" ambayo inatuonesha tulivyo na wabunge wasiojali uwakilishi wetu fedha zetu na kadhalika. Labda tu kama Spika atakuwa ameupotosha umma kwa kumuonea Joshua Nassari..

Lakini hadi hapa kwa taarifa hii ya bunge ikituonesha NEC kujuzwa jimbo la Arumeru Mashariki kuwa wazi, ni uzembe wa CHADEMA na KUB kushindwa kusimamia maadili na kanuni kwa wabunge wake. Wanajiendesha tu juu ya taasisi iliyowapa dhamana.

But what do i know??
#MMM

====

Unahitaji roho ya chuma kumtetea Nassari. Unakosa vipi vikao vyote vya mikutano 3 ya bunge ukiwa na afya timamu? Hii ni sawa na MWAKA MZIMA. Atleast angelikosa mikutano 2 na ule mmoja unahudhuria. Unaenda siku moja, unatia saini unaenda zako Seattle huko. Hawakupati popote. Sasa huyu mwaka mzima hajakanyaga Dodoma. Eti mimba. Unalea mimba? Wana Arumeru walichagua mbunge au Vasco Da Gama? Wanasiasa wengine chapa fimbo nyingi hadharani."

====

Documents. Documents. Documents. Documents.
Nassari anasema aliomba e-mail (aliomba) ya Spika na kupewa. Maana yake hakuwa na njia rasmi za mawasiliano na ofisi ya Spika.
Kwamba, mbunge mzoefu kama Nassari hajui kabisa miaka saba (7) amekuwa akiwasiliana vipi na ofisi ya spika?? Hajui kabisa?
Afadhali hata angelituma barua yake 'hard copy' kwa njia ya FedEx au DHL kuliko hizi porojo zingine alozoleta leo.
Jana Freeman aliposema 'Nassari awaeleze mwenyewe kilichotokea' watu wazima tulielewa. Tukajua hii 'blunder' Freeman anairuka. Hataki kushiriki huu "utoto" wa Josh.
Nilifikiri kama Nassari ameonewa, basi atakuwa na vielelezo. HANA. anatupiga kamba tu. Alipaswa kuwaonesha waandishi wa habari "alivyoonewa kwa vielelezo"
Halafu Nassari, kwani lazima uwasiliane 'direct' na Spika? Ofisi ya naibu spika ipo.. ofisi ya katibu wa bunge ipo. Kwanini hukutuma e-mail huko?
Twende hapa. CDM wanazo idara zenye kushughulika na masuala ya bunge. Kwamba Nassari hakuna taarifa zake hapo? Zipo wapi?
Ofisi ya KUB haina taarifa hizo? Zipo wapi sasa? Mnadhimu wa KUB hana taarifa za kimaandishi? Zipo wapi? Ok.. katibu mkuu wa CDM hana taarifa za mbunge wake kuwa nje ya nchi kwa ruhusa?
Kuna maswali mengi najiuliza hapa. Sipati majibu. Press ya Nassari ina mapengo mengi sana. Inahitaji kujazwa nyama nyingi.
Ushauri wangu kwako Nassari. Nenda sasa mahakama za kikatiba. Nenda kwenye bunge la jumuiya ya madola. Peleka vielelezo. Kama unavyo, vitumie. Lasivyo itakuwa kazi bure.

=====

Mwisho kabisa.

Suala la Nassari limenifanya nibaini kuna mstari mdogo sana unaoweza kuwatofautisha vijana wa upinzani na MATAGA. kwa aina hii vijana, tutaendelea kuwa na taasisi za hovyo za kisiasa. Vijana hawa wanatetea lolote linalofanywa na viongozi wao na kukosoa la upande mwingine.

Nimemsikiliza Joshua Nassari A~Z na kubaini kwamba hajauza jimbo, isipokuwa kwa uzembe na makosa yake ya kiufundi "amevuliwa ubunge" CDM wamelipoteza jimbo. Nyakati hizi sikutegemea mbunge wa upinzani afanye makosa ya kizembe na upumbavu wa bei rahisi. Costly mistakes. Blunders.

Fikiria, Ofisi ya katibu mkuu CDM imeonesha uzembe mkubwa. Ile idara inayohusika na masuala bunge nayo haina taarifa za mbunge wake kuwa nje ya nchi kwa ruhusa. Ofisi ya KUB pia haina vielelezo.. nimefika wakati nikajiaminisha, bado ipo safari ndefu sana kufika mbele tuendako.

Taasisi imara sana ni ile iliyofanikiwa kwenye nidhamu ya wabunge na viongozi wa idara za HQ na hata KUB. Sasa mambo yapo shaghalabaghala sana. Mtu aina ya Nassari kwa uzembe huu alipaswa kuwajibishwa na taasisi yake kabla ya bunge. Lakini what happened? Tunamtetea 'mbunge mtoro' kwa faida ya nani?? Tumekuwa waswahili sana.

Tabia za kiswahili ni kati ya tabia za hovyo tu. Na tukiendelea na uswahili huu hata wachache hao wanaotuamini sasa wataacha kutuamini na watajitenga mbali nasi. Tutabaki yatima kama makinda ya ndege kwenye mbuyu mkubwa.

Kwa upande mwimgine, haya ni Matokeo ya bunge kutokuwa 'MUBASHARA' ndio matokeo ya wabunge kuwa watoro na kutochangia bungeni... wananchi wanashtukizwa maana hawana sehemu ya kuwaona wawakilishi wao hata pale wanapokuwa hawapo bungeni. Nape na Magufuli engineered that skirmish,

Anyways, tuendelee kujadili masuala mengine yanayotukabili
#MMM
20210621_131049.jpg

20210621_131043.jpg

20210621_131039.jpg

20210621_131033.jpg
 
Narudia tena sina imani na huyo Maza. Naona anakurupuka tu na teuzi zake. Sijui hata kama anauliza maswali ya kina kwa hao wanaofanya vetting. Na hao wanaofanya vetting ni watu makini kweli wanaoweka mbele maslahi ya Nchi au WANADEMKA tu ili siku iingie? Kuna OMBWE kubwa sana la uongozi nchini.
 
Narudia tena sina imani na huyo Maza. Naona anakurupuka tu na teuzi zake. Sijui hata kama anaulizwa maswali ya kina kwa hao wanaofanya vetting. Na hao wanaofanya vetting ni watu makini kweli wanaoweka mbele maslahi ya Nchi au WANADEMKA tu ili siku iingie? Kuna OMBWE kubwa sana la uongozi nchini.
Huyu Mama ni tatizo na ameamua kurithi na kuyaenzi baadhi ya mambo ya yasiyofaa ya Mwendazake yaliyotuharibia hii nchi.

Kwa kifupi, hatoshi na bora muda wake uishe aondoke.

Hata Katiba Mpya sidhani kama itakuwa ni moja ya vipaumbele vyake kwani inaonekana ameanza kufurahia hii katiba mbovu inayompa mamlaka makubwa ya kufanya atakavyo.
 
Narudia tena sina imani na huyo Maza. Naona anakurupuka tu na teuzi zake. Sijui hata kama anauliza maswali ya kina kwa hao wanaofanya vetting. Na hao wanaofanya vetting ni watu makini kweli wanaoweka mbele maslahi ya Nchi au WANADEMKA tu ili siku iingie? Kuna OMBWE kubwa sana la uongozi nchini.
Maza yuko vizuri tatizo analemewa na kelele ndani ya ccm...ishu ya sabaya imeleta mgawanyiko mkubwa sana.. Kwakuwa ilionekana ni ushindi kwa CHADEMA na mwenyekiti...! Hili la kuwateua kina Nasari ni kama kuwapoza machungu mataga
 
Maza yuko vizuri tatizo analemewa na kelele ndani ya ccm...ishu ya sabaya imeleta mgawanyiko mkubwa sana.. Kwakuwa ilionekana ni ushindi kwa CDM na mwenyekiti...! Hili la kuwateua kina Nasari ni kama kuwapoza machungu mataga
Anazidi kuharibu tu kwani hizo nafasi MATAGA ndio walikuwa wanazitaka hivyo anazidi kuharibu pande zote.

Anatakiwa aachane na mambo ya kijinga aliyoyaasisi Mwendazake.
 
Kuna wanaodai tumpe muda lakini kuna mengi tu ambayo angekuwa ana nia nzuri ya kuweka maslahi ya nchi mbele basi angeshayafanyia kazi au at least kutwambia Watanzania ni vipi atayashughulikia tena kwa haraka lakini yupo yupo tu na mikutano yake na makundi ya Watanzania ambayo haina tija huku akiendelea kukwepa kukutana na Wapinzani wa kweli nchini. Sioni jipya na hilo la Katiba huru na Tume mpya ya uchaguzi kupatikana kabla ya uchaguzi mkuu October 26, 2025 tusahau tu.

Huyu Mama hafai na amerithi mambo ya hovyo ya Mwendazake yaliyotuharibia hii nchi...
 
Nyinyi huwa hamna jema wala shukran.

Jiwe ndio aliwajua vyema na ndio maana akawafanyia alivyowafanyia. JK aliwaeka karibu na kuamini kwamba Tanzania ni yetu sote lakini shukran yenu ni matusi kwake.

Hata mfanyiwe nini nyinyi hamtokaa mshukuru kwamba angalau mmepata rais anaeskiliza maoni na kujali kwamba sote ni Watanzania. Mmekalia lawama juu ya lawama juu ya lawama.

Muwe na staha na busara na muache huu ujinga wenu dhidi ya rais.

Yaani tatizo ni kuteuliwa Nassari???? Huku hampo na kule hampo
 
Maza yuko vizuri tatizo analemewa na kelele ndani ya ccm...ishu ya sabaya imeleta mgawanyiko mkubwa sana.. Kwakuwa ilionekana ni ushindi kwa CDM na mwenyekiti...! Hili la kuwateua kina Nasari ni kama kuwapoza machungu mataga

Issue ya Sabaya ni ushindi kwa Chadema? Kila kitu Sio siasa mjinga kweli wewe what about:

  • Watoto waliobakwa na kula witiwa?
  • wanavyuo waliobakwa na kulawitiwa?
  • walioteswa?
  • waliozulumiwa?

Nyie CCM hamna akili kabisa! Na huu ubinafai wenu unafika mwisho si Mda mrefu!
 
Kama ndani ya maccm kuna wanaomtetea yule jambazi na muuaji basi chama hicho hakistahili kuwepo madarakani kwani sasa ni genge la majambazi na wauaji ambao wako tayari kufanya maovu ya kila aina ili kujikusanyia utajiri haramu na kuua ili kuendelea kung’ang’ania madaraka.
Maza yuko vizuri tatizo analemewa na kelele ndani ya ccm...ishu ya sabaya imeleta mgawanyiko mkubwa sana.. Kwakuwa ilionekana ni ushindi kwa CDM na mwenyekiti...! Hili la kuwateua kina Nasari ni kama kuwapoza machungu mataga
 
Nyinyi huwa hamna jema wala shukran.

Jiwe ndio aliwajua vyema na ndio maana akawafanyia alivyowafanyia. JK aliwaeka karibu na kuamini kwamba Tanzania ni yetu sote lakini shukran yenu ni matusi kwake....
Huyo Jiwe ndio hopeless kabisa.

Hatuhitaji kubembeleza mtu kutimiza wajibu wake kwani hii kazi waliomba wenyewe na wanalipwa vizuri sana kufanya hii kazi hivyo ni wajibu wao kufanya wanachotakiwa kukifanya.

Hizo ni kodi zetu hatuwezi kukaa kimya kuona zinatumika vibaya.
 
Very well said Mkuu. Hawatufanyii hisani ni pesa zetu walipa kodi ambazo wanaishia kufanya madudu miaka nenda miaka rudi. Miaka 60 ya uhuru katika nchi iliyo na utajiri mkubwa sana lakini hakuna chochote cha kujivunia huku kundi lao la wachache wakiwa mamilionea na mabilionea kupitia kodi zetu wakati huo sekta zote muhimu nchini Elimu, Afya, usafiri, maji, umeme, ajira, uchumi, vyombo vya dola ni HOVYO KABISA.
Huyo Jiwe ndio hopeless kabisa.

Hatuhitaji kubembeleza mtu kutimiza wajibu wake kwani hii kazi waliomba wenyewe na wanalipwa vizuri sana kufanya hii kazi hivyo ni wajibu wao kufanya wanachotakiwa kukifanya.

Hizo ni kodi zetu hatuwezi kukaa kimya kuona zinatumika vibaya.
 
Issue ya Sabaya ni ushindi kwa Chadema? Kila kitu Sio siasa mjinga kweli wewe what about:
  • Watoto waliobakwa na kula witiwa?
  • wanavyuo waliobakwa na kulawitiwa?....
Pole nadhani hukuelewa nilichoandika pengine na kwa vile umetoka usingizini.. Nadhani kuna nyuzi zisizopungua 30 hapa jukwaani za kumtetea sabaya na wanaofanya hivyo wanajulikana
 
Huyo Jiwe ndio hopeless kabisa.

Hatuhitaji kubembeleza mtu kutimiza wajibu wake kwani hii kazi waliomba wenyewe na wanalipwa vizuri sana kufanya hii kazi hivyo ni wajibu wao kufanya wanachotakiwa kukifanya.

Hizo ni kodi zetu hatuwezi kukaa kimya kuona zinatumika vibaya.
Hamna lolote mkuu, hamnaga hoja wala agenda iliyo na malengo ya kitaifa. Nyinyi ni kupinga tu kila lifanywalo.

Hamuwezi kukaa kimya mbona kipindi cha jiwe mliufyata?? Shukuruni kwamba Marais waislam wana hekma na busara.

Kwa kutumia hizo hizo kodi zenu jiwe alifanya anavyotaka na mliufyata kimyaaaa hakuna cha kodi zenu wala nini.

Muwe na staha na busara na muache huu ujinga wenu dhidi ya Rais.
 
Huwa mnashangaza Sana yaani mnataka katiba kwa sababu ya uchaguzi? Mozambique ya Samora, ANC ya Mandela na wenzake, Mugabe na wenzake, Museveni na wenzake , Kagame , etc walishinda na waliingia madarakani bila katiba mpya, hawakupiga kelele za kimama mama kama zenu.

Siasa zenu na mikakati yenu ni kitoto kitoto , Kila siku mlalilia kupata biscuits ambazo hamna uwezo nazo ili Hali mnasubiriwa kupewa na baba yenu.

Pambaneni kama wenzenu badala kukaa na kuandika Kama umelewa pombe za ofa.
Kuna wanaodai tumpe muda lakini kuna mengi tu ambayo angekuwa ana nia nzuri ya kuweka maslahi ya nchi mbele basi angeshayafanyia kazi au at least kutwambia Watanzania ni vipi atayashughulikia tena kwa haraka lakini yupo yupo tu na mikutano yake na makundi ya Watanzania ambayo haina tija huku akiendelea kukwepa kukutana na Wapinzani wa kweli nchini. Sioni jipya na hilo la Katiba huru na Tume mpya ya uchaguzi kupatikana kabla ya uchaguzi mkuu October 26, 2025 tusahau tMMlevi

Kuna wanaodai tumpe muda lakini kuna mengi tu ambayo angekuwa ana nia nzuri ya kuweka maslahi ya nchi mbele basi angeshayafanyia kazi au at least kutwambia Watanzania ni vipi atayashughulikia tena kwa haraka lakini yupo yupo tu na mikutano yake na makundi ya Watanzania ambayo haina tija huku akiendelea kukwepa kukutana na Wapinzani wa kweli nchini. Sioni jipya na hilo la Katiba huru na Tume mpya ya uchaguzi kupatikana kabla ya uchaguzi mkuu October 26, 2025 tusahau tu.
 
Kuna wanaodai tumpe muda lakini kuna mengi tu ambayo angekuwa ana nia nzuri ya kuweka maslahi ya nchi mbele basi angeshayafanyia kazi au at least kutwambia Watanzania ni vipi atayashughulikia tena kwa haraka lakini yupo yupo tu na mikutano yake na makundi ya Watanzania ambayo haina tija huku akiendelea kukwepa kukutana na Wapinzani wa kweli nchini. Sioni jipya na hilo la Katiba huru na Tume mpya ya uchaguzi kupatikana kabla ya uchaguzi mkuu October 26, 2025 tusahau tu.
Na mkiendelea hivi hiyo habari ya mikutano na the so called wapinzani wa kweli itapotelea hewani. Haina hata haja ya kuwakaribisha.

Sisi tutamkumbusha aachane na hizo habari maana Mheshimiwa Kikwete alifanya hivyo na hakuna tija yoyote iliyopatikana law kukutana na hao wanaojiita wapinzani wa kweli. Zaidi zaidi walikwenda tu kunywa chai ikulu na kuongeza gharama zisizo za msingi.

Kwa tabia zenu hizi Wallahi haya mambo ya katiba mpya na tume huru pia yanaweza yakapeperuka na to be honest my friend hamna mtakaloweza kumfanya mama. Ni hisani na busara zake tu. Ni mapenzi yake kwa taifa lake tu, hivyo musitake kumvuruga.

Eti anatoka mtu na kusema hatuwezi kumbembeleza na tutapaza sauti. You are not being realistic.

Muwe na staha wakuu
 
Back
Top Bottom