Joshua Nassari apata ajali ya chopa

Joshua Nassari apata ajali ya chopa

CHADEMA anadaeni maandamano ya kupinga NASSARY kupata ajali.
 
Suala hapo ni kwamba akome kutumia hizo chopa maana sio size zake kila kukicha tunasikia yuko na chopa mara huku mara kule sasa kwanini asiachane nazo tu maana zitakuja kumuua bure!

Hizi sasa nadhani labda ni chuki zako mkuu tu na hakuna kigezo kingine unachokitumia. Pointi yangu ni kwamba hata kama akiacha kutumia chopa na akapanda gari, bado nalo linaweza kupata ajali vie vile!! Naamini tutakuwa tumeelewana hapo.
 
hizi habari ni za ukweli kamanda nassari amepata ajali ya helkopita leo wakati akitoka kwenye kampeni za kuhamasisha watu kujiandikisha taarifa ambazo hajithibitishwa nassari ameumia ambulance ipo njiani ndo inampeleka katika hospital selian arusha
may day may day choper down!
 
wanabodi nawasalimu sana.

Nimepewa taarifa muda huu kuwa mbunge wa arumeru mashariki, ndugu joshua nassari, amepata ajali muda huu akiwa maeneo ya leguruki.

Mosi, inasemekana amenusurika na amepata majeraha madogo lakini mmoja wa abiria wake kavunjika mguu.

Nitazidi kuwajuza kadri nitakavyopokea taarifa.

Nawasilisha.

******** updates *********

mbunge amekimbizwa katika hospitali ya selian na kwa mujibu wa katibu wa mbunge hajaumia sana, ila abiria wawili mmoja anajulikana kwa jina la eve ambaye ni mmoja wa viongozi wa bawacha jimboni kaumia mbavu na mwingine kavunjika mguu.

Tupo jimboni na tunawatoa hofu wananchi wote waliopata taharuki jimboni kuwa mbunge ni mzima amepatwa na majeraha kidogo!!

Tunamshukuru mungu kwa rehema zake.

View attachment 266469
nataka kujua historia fupi ya huyo rubani......
Pia nataka kujua nani manufacturer wa hiyo chopa imesajiliwa ''nji'' gani...kwa kumbukumbu zangu za kizee hii ni chopa ya pili( kwa kipindi kifupi)kuanguka ikufuatiwa na ile iliyoanguka kipunguni.
 
bila ujuzi wa GIS ingekuwa balaa hongera rubani hali ya hewa Arusha kwa sasa angani inahitaji ujasiri. yote hayo ni kwasababu kuhakikisha kila Mtanzania anapata mlo maratatu kwa siku.

mafisadi yalaaniwe

We boya kweli! kwani wameitungua hiyo chopa mbovu!?
 
We boya kweli! kwani wameitungua hiyo chopa mbovu!?

...Huwa najibu kwa vitendo only 4 gt !!!

Dog-fight-to-death.jpg
 
Wakati Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari akisema anashindwa kuamini kilichotokea na kunusurika katika ajali ya helikopta juzi,mmiliki wa chopa hiyo, Philemon Ndesamburo amesema atanunua nyingine haraka kabla ya kuanza kampeni za Uchaguzi Mkuu.

Kauli hizo zilitolewa jana ikiwa ni siku moja baada ya helikopta hiyo inayomilikiwa na Ndesamburo kupitia kampuni yake ya Keys Aviation kupata ajali wakati ikitumiwa na Nassari na baadhi ya viongozi wa CHADEMA.

Wakati ikipata ajali, ilikuwa imekodishwa na Kampuni ya General Aviation Services (T) Ltd inayomilikiwa na Kapteni William Slaa.

Katibu wa Ndesamburo, Basil Lema alisema ilipata ajali baada ya kupigwa na kimbunga wakati anga likiwa limefunikiwa na wingu zito.¡°Mheshimiwa Ndesamburo amemshukuru Mungu kwa kuwanusuru watu waliokuwa kwenye ndege hiyo ambao ni pamoja na Mbunge Joshua Nassari.¡°Ameweka wazi kwamba atalazimika kununua nyingine mapema kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka huu,¡± alisema Lema akimnukuu Ndesamburo.

Lema alisema rubani aliyekuwa akiendesha helikopta hiyo alifanikiwa kuielekeza juu ya miti alioutumia kupunguza kasi ya kushuka chini na kusaidia abiria kutoka salama.¡°Imeharibika lakini abiria wote ni wazima. Walikuwamo wanne,¡± alisema na kuongeza kuwa helikopta hiyo ndiyo iliyotumiwa na CHADEMA katika Uchaguzi Mkuu wa 2010 na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka jana na chama hicho kilitegemea kuitumia katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Pia, imewahi kutumiwa na makada mbalimbali wa CCM akiwamo Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba na kada maarufu wa Moshi mjini, Buni Ramole.

Kauli ya Nassari Akizungumza na waandishi wa habari katika wodi alikolazwa kwenye Hospitaliya Seliani ¨C Arusha, Nassari alisema waliporuka kutoka Leguruki, hakukuwa na dalili zozote za kuchafuka kwa hali ya hewa, lakini dakika chache baada ya kuruka angani wingu zito lililoambatanana upepo mkali liliwafunika ghafla.¡°Wingu lile na upepo ule sijawahi kuona katika maisha yangu yote zaidi ya kusoma kwenye vitabu vya simulizi vya mambo ya ushirikina.

Namshukuru Mungu wote tuko salama kwani hatukuwa na matumaini ya kupona ajali ile,¡± alisema Nassari.

Mbunge huyo aliyekuwa katika ziara ya kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwenye Daftari la Wapigakura, alimwagia sifa rubani Slaa kwa uwezo na ustadi aliouonyesha hadi wakanusurika.¡°Kama siyo ustadi wake, naamini watu wangeokota vipande vya nyama tu kwenye eneo la ajali, ila Mungu ni mkuu leo tuko hai wote licha ya madhara madogo,¡± alisema.

Nassari alisema muda mfupi kabla ya kuruka saa kumi na moja jioni, wakati akihutubia mkutano huko Leguruki, alipokea simu kutoka kwa mchungaji mmoja akimtaarifu kupata maono kuwa anakabiliwa na hatari ya kukutwa na jambo kubwa na baya akimtaka adumu katika sala.¡°Dakika 15 baadaye nikaruka na kupataajali.

Naamini kilichotuokoa ni nguvu yasala niliyosali baada ya kupokea ujumbe wa mchungaji na maombi ya wachungaji wangu wanaoniombea kila siku,¡± alidai Nassari.

Rubani Slaa alisema alishangaa lilipotokea wingu na upepo uliosababisha ndege kuanguka ikiwa njiani kuelekea Ndoombo na Ngureserosambu.¡°Kabla ya kurusha ndege nilijiridhisha na hali ya hewa.

Hakukuwa na kiashiria chochote cha hali ya hatari kama maeneo mengine ambako tulishindwa kutua kutokana na mvua zilizokuwa zikinyesha.

Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Seliani, Dk Paul Kisanga alisema hali za majeruhi si mbaya, isipokuwa Eva Kayaha aliyevunjika mbavu mbili.


Chanzo:
Mwananchi
 
Khali ya hewa kubadilika ghafla sio uchawi. Pia inaonyesha dhahiri ni msimu wa mvua mvua kwa hiyo kusema ni uchawi inakuwa too presumptive. Haya mambo ya mabadiliko ya ghafla huwa yapo
 
Hapo na siasa imeingizwa, eti uchawi! 'nilipokea cm toka kwa mchungaji mmoja' mbona hamtaji jina?! siasa siasa siasa! credit to oct 25! ni maoni yangu tu!
 
Back
Top Bottom