Joshua Nassari apata ajali ya chopa

Joshua Nassari apata ajali ya chopa

mmaranguoriginal.

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2014
Posts
4,060
Reaction score
460
Wanabodi nawasalimu sana.

Nimepewa taarifa muda huu kuwa mbunge Wa Arumeru Mashariki, ndugu Joshua Nassari, amepata ajali muda huu akiwa maeneo ya Leguruki.

Mosi, inasemekana amenusurika na amepata majeraha madogo lakini mmoja Wa abiria wake kavunjika mguu.

Nitazidi kuwajuza kadri nitakavyopokea taarifa.

Nawasilisha.

******** Updates *********

Mbunge amekimbizwa katika Hospitali ya Selian na kwa mujibu wa Katibu wa mbunge hajaumia sana, ila abiria wawili mmoja anajulikana kwa jina la Eve ambaye ni mmoja wa viongozi wa BAWACHA jimboni kaumia mbavu na mwingine kavunjika mguu.

Tupo jimboni na tunawatoa hofu wananchi wote waliopata taharuki jimboni kuwa Mbunge ni mzima amepatwa na majeraha kidogo!!

Tunamshukuru Mungu kwa rehema zake.

Nassari.jpeg

Mbunge Nassari azungumzia ajali, Ndesamburo kununua chopa mpya!
Wakati Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari akisema anashindwa kuamini kilichotokea na kunusurika katika ajali ya helikopta juzi, mmiliki wa chopa hiyo, Philemon Ndesamburo amesema atanunua nyingine haraka kabla ya kuanza kampeni za Uchaguzi Mkuu.

Kauli hizo zilitolewa jana ikiwa ni siku moja baada ya helikopta hiyo inayomilikiwa na Ndesamburo kupitia kampuni yake ya Keys Aviation kupata ajali wakati ikitumiwa na Nassari na baadhi ya viongozi wa CHADEMA.

Wakati ikipata ajali, ilikuwa imekodishwa na Kampuni ya General Aviation Services (T) Ltd inayomilikiwa na Kapteni William Silaa.

Katibu wa Ndesamburo, Basil Lema alisema ilipata ajali baada ya kupigwa na kimbunga wakati anga likiwa limefunikiwa na wingu zito.

"Mheshimiwa Ndesamburo amemshukuru Mungu kwa kuwanusuru watu waliokuwa kwenye ndege hiyo ambao ni pamoja na Mbunge Joshua Nassari.

"Ameweka wazi kwamba atalazimika kununua nyingine mapema kwa ajili ya kuongeza nguvu kwenye kampeni za Uchaguzi Mkuu mwaka huu," alisema Lema akimnukuu Ndesamburo.

Lema alisema rubani aliyekuwa akiendesha helikopta hiyo alifanikiwa kuielekeza juu ya miti alioutumia kupunguza kasi ya kushuka chini na kusaidia abiria kutoka salama.

"Imeharibika lakini abiria wote ni wazima. Walikuwamo wanne" alisema na kuongeza kuwa helikopta hiyo ndiyo iliyotumiwa na CHADEMA katika Uchaguzi Mkuu wa 2010 na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka jana na chama hicho kilitegemea kuitumia katika Uchaguzi Mkuu ujao.

Pia, imewahi kutumiwa na makada mbalimbali wa CCM akiwamo Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Mwigulu Nchemba na kada maarufu wa Moshi mjini, Buni Ramole.

Kauli ya Nassari Akizungumza na waandishi wa habari katika wodi alikolazwa kwenye Hospitaliya Seliani C Arusha, Nassari alisema waliporuka kutoka Leguruki, hakukuwa na dalili zozote za kuchafuka kwa hali ya hewa, lakini dakika chache baada ya kuruka angani wingu zito lililoambatanana upepo mkali liliwafunika ghafla.

"Wingu lile na upepo ule sijawahi kuona katika maisha yangu yote zaidi ya kusoma kwenye vitabu vya simulizi vya mambo ya ushirikina.

Namshukuru Mungu wote tuko salama kwani hatukuwa na matumaini ya kupona ajali ile," alisema Nassari.

Mbunge huyo aliyekuwa katika ziara ya kuhamasisha wananchi kujiandikisha kwenye Daftari la Wapigakura, alimwagia sifa rubani Silaa kwa uwezo na ustadi aliouonyesha hadi wakanusurika.

"Kama siyo ustadi wake, naamini watu wangeokota vipande vya nyama tu kwenye eneo la ajali, ila Mungu ni mkuu leo tuko hai wote licha ya madhara madogo," alisema.

Nassari alisema muda mfupi kabla ya kuruka saa kumi na moja jioni, wakati akihutubia mkutano huko Leguruki, alipokea simu kutoka kwa mchungaji mmoja akimtaarifu kupata maono kuwa anakabiliwa na hatari ya kukutwa na jambo kubwa na baya akimtaka adumu katika sala.

"Dakika 15 baadaye nikaruka na kupata ajali.

Naamini kilichotuokoa ni nguvu yasala niliyosali baada ya kupokea ujumbe wa mchungaji na maombi ya wachungaji wangu wanaoniombea kila siku," alidai Nassari.

Rubani Slaa alisema alishangaa lilipotokea wingu na upepo uliosababisha ndege kuanguka ikiwa njiani kuelekea Ndoombo na Ngureserosambu.

"Kabla ya kurusha ndege nilijiridhisha na hali ya hewa.

Hakukuwa na kiashiria chochote cha hali ya hatari kama maeneo mengine ambako tulishindwa kutua kutokana na mvua zilizokuwa zikinyesha.

Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Seliani, Dk Paul Kisanga alisema hali za majeruhi si mbaya, isipokuwa Eva Kayaha aliyevunjika mbavu mbili.


Chanzo:
Mwananchi
 
Hizi habari ni za ukweli kamanda Nassari amepata ajali ya helkopita leo wakati akitoka kwenye kampeni za kuhamasisha watu kujiandikisha taarifa ambazo hajithibitishwa Nassari ameumia ambulance ipo njiani ndo inampeleka katika hospital selian Arusha
 
Mbunge amekimbizwa ktk Hosptal ya Selian na kwa mujibu wa Katibu wa mbunge hajaumia sana ila abiria wawili mmoja anajulikana kwa jina la Eve ambaye ni mmoja wa viongozi wa BAWACHA jimboni kaumia mbavu na mwingine kavunjika mguu.

Tupo jimboni na tunawatoa hofu wananchi wote waliopata taaruki jimboni kuwa Mbunge ni mzima amepatwa na majeraha kidogo!!

Tunamshukuru Mungu kwa rehema zake.
 
twashukuru sanaaa ndg.kwa taarifaa hizoo unapopata zingine just expose
 
Taarifa kutoka kwa Ndote Katibu wa Mbunge Mbowe juu ya ajali Hii hapa
í-½í±‡í-½í±‡í-½í±‡

Chopper imepigwa na storm kwa takriban dk 2. Pilot amefanikiwa kufanya landing manouvre lakini kimbungaa kilikuwa kikali sana. Ndege imecrash abiria wameumia kiasi tu. Wamepelekwa Selian Hospital.

Ndege imebaki vipande. Nimeongea na pilot akiwa na tune nzuri tu. Wenzake walikuwa wametangulia hospitalini. Tuwaombee wapate nafuu haraka.
 
Eti,kapata vijeraha vidogo?na pia kavunjika mguu mmoja wapo?
sidhani!!!
 
Nasari kwa nn anatumia chopa kipindi hiki?
 
Pole kwake dogo janja na wenzake!!!Mungu awape ahueni haraka
 
Hizi habari ni za ukweli kamanda Nassari amepata ajali ya helkopita leo wakati akitoka kwenye kampeni za kuhamasisha watu kujiandikisha taarifa ambazo hajithibitishwa Nassari ameumia ambulance ipo njiani ndo inampeleka katika hospital selian Arusha

Mkuu thanks,
 
Ni kwamba anashindwa kuzungukia jimbo kwa gari? Juzi tu hapa nimepost kuhitaji kujua umuhimu na ulazima wa Nassari kutumia chopa ndani ya jimbo kama sio ufujaji wa pesa... but pole kwake
 
Mungu awaponye makamanda wote walihusishwa na ajali hiyo.Mapambano yanaendelea
 
Haya ndiyo madhara ya kupuuza utabiri wa hali ya hewa, mbona jana TMA walitoa tahadhari ya weather today.Poleni wajeruhiwa mnatakiwa mheshimu utaalamu
 
Ni kwamba anashindwa kuzungukia jimbo kwa gari? Juzi tu hapa, nimepost kuhitaji kujua umuhimu na ulazima wa Nassari kutumia chopa ndani ya jimbo kama sio ufujaji wa pesa... but pole kwake

Hiyo pesa anatoa wapi kukodi chopa?
 
Haya ndiyo madhara ya kupuuza utabiri wa hali ya hewa, mbona jana TMA walitoa tahadhari ya weather today.Poleni wajeruhiwa mnatakiwa mheshimu utaalamu

Mkuu hao ni wapinzani, kila amri itokayo kwa watendaji wa serikali wameagizwa kuipinga tu, na hii ya hali ya hewa nayo watadai aliyeitoa kaajiriwa na ccm hivyo sio rahisi kutii amri hiyo. Poleni majeruhi.
 
Back
Top Bottom