Joshua Nassari aiombe radhi CHADEMA

Joshua Nassari aiombe radhi CHADEMA

Wanaotaka kumlaumu nasari wanakosea na ni wageni kwenye siasa,je kama alipata nafasi ya kukutana na magufuli mnajuaje hakumweleza yanayoendelea kule Dar na moro?
 
Kama ni hivyo hata Magufuli ni rais wa watanzania hata sisi ambao hatukumpa kura tumeshamkubali.. Magufuli kaenda Arusha kama kiongozi wa serikali na si mwanachama wa CCM...

Mlaumu Nassari kama CDM haiitambui serikali lakini as long as wanaitambua basi hana kosa lolote. Kuna mchangiaji hapo kasema na Meya wa Arusha na viongozi wengine wa CDM walioenda mbona hujawa'address ??
Muwe mnamshauri huyo Ngosha akiwa kwenye ziara kama Rais aache mipasho ya vyama. Shida naiona imeanza kwa kuingiza UCCM.
 
Kwanza Marandu inabidi uombe radhi kwa kuongezea maneno ya uwongo.Magufuli hakusema ndani ni ccm,alisema ndani mpenda maendeleo. Lakini tuulizane hapa,Nassari alikuwa pekee mtu wa chadema pale kwenye mapokezi? Kwa nini asakamwe yeye tu.
Kulikuwa na Mh Meya wa jiji la Arusha,kulikuwa watu wengi tu wa chadema. Pili Mh Msigwa alimpokea waziri mkuu Mjaliwa lakini hayajasemwa. Tatu Mbunge Mh prof Jay juzi alikuwa na waziri wa mifugo jimboni kwake kutatua mgigoro wa wakulima wa miwa,mbona haulizwi chochote?
Umeona eeh? naniliona mwigulu akifurahia na profesa Jay wakiwa na nyuso za tabasamu kabisa labda kama kuna Jambo liko nyuma ya pazia kuhusu Joshua sioni sababu yakufikia watu kua na chuki kiasi hicho wakati hii nchi ya kwetu sote.
 
Fukuzeni msaliti huyo anataka kuwa kama Zitto Kabwe alivyokuwa anaambatana na Kikwete.
 
Unaleta siasa za maji taka humu wakati maendeleo ndio kipaumbele cha taifa na ustawi wa Taifa letu.mawazo yako ni mgando kabisa mleta uzi tena wewe ni mnafiki na mzandiki mkubwa.kwa hiyo kama kamsifia ulitaka amshike mashati palepale au?ile ni issue ya kitaifa ww umekalia siasa tu.kama unaona ukawa ndio wenye uchungu na hii nchi mbona posho na ruzuku zao wanaweka mfukoni hawakugawii japo ulipie vitoto vyako shule au kwa nini hawazikuanyi kwa pamoja wakasaidia jamii iliyowazunguka!acha porojo zako
 
Msichoelewa Kila Jambo Lina wakati wake, Sioni Ubaya Kuungana na Rais Katika Ziara za Maendeleo. Au Kumsifia akifanya Mema. Alichokosea Nassari Ni Timing, Kila Kitu Kina wakati wake. Wakati Wabunge wengine wa Chadema wakihangaika Kuwawekea Dhamana Wenzako, wewe Unazungusha matako yako na Anayehusika Kuwahujumu, Na Palepale anakutumia kuwalamba Vijembe wenzako. Na Unachekelea sio Wazimu huo!
 
Msichoelewa Kila Jambo Lina wakati wake, Sioni Ubaya Kuungana na Rais Katika Ziara za Maendeleo. Au Kumsifia akifanya Mema. Alichokosea Nassari Ni Timing, Kila Kitu Kina wakati wake. Wakati Wabunge wengine wa Chadema wakihangaika Kuwawekea Dhamana Wenzako, wewe Unazungusha matako yako na Anayehusika Kuwahujumu, Na Palepale anakutumia kuwalamba Vijembe wenzako. Na Unachekelea sio Wazimu huo!
Mkuu unakosea unaonyesha unasiasa za chuki sana mpaka basi sasa Rais yuko eneo lake afanyaje?
 
Point yako hasa ni nini!? Nasari aombe msamaha kwa kosa la unafiki la kumpokea raisi? Au Nasari aombe msamaha kwa kosa la unafiki sababu amesifiwa na raisi?
 
Acha chokochoka marandu..Siasa sio Uadui...Nasari is doing a great Job...Lema anatakiwa aige...maendeleo ya wananchi kwanza
 
Siasa siyo uadui nani kakwambia?.
Yanayofanyika zenji,umeye dar na morosiyo uadui?.
Mwenye mada ni kama kaongea ukweli vile.
 
Nasary ameanza kuwa na akili sana amejua kuwa Ccm ndio chama kilichomlea na kumsomesha bure.
 
Kapo ni Kweli Naamini mara nyingi thiredi za Namna hii zInaaziishwa Na Maadui wa

Chadema Na Ukawa ili kuchonganisha
 
mbona unatumia maneno yenye ukakasi naunaonekana unamchukia sana nassari. nimesoma nikaona ukiacha tukio lenyewe ni kuwa wewe unamchukia sana joshua nassari. sijui sababu. unadhan ilikuwa busara nassari amjibu magufuli pale mkutanoni? come on... mbali na mambo mengine dr magufuli ni kama mzazi wa joshua nassari na yale maneno aliyosema dr magufuli ni utani tu ambapo angeweza kusema mshabiki wa yanga akimzungumzia wa simba. siasa si chuki na uadui. unadhani mkiishi kiadui inawasaidia nini wananchi?
ccm wakifanya vizuri watasifiwa na wakifanya vibaya tutawaponda sna tu. ila siasa unazozitaka wewe ndo za MIAFRIKA MIJINGA AMBAYO WAKATI WA UCHAGUZI INAWAKAMATA WAPINZANI NA KUWAFUNGA AU KUWABAMBIKIA KESI. HUU NI UJINGA WA MIAFRIKA MINGI SANA.

nassari ahana cha kuomba radhi, kama mbunge yupo kwa maslah ya watu wake na kuna kpindi habari za kipuuzi mtu unatakiwa kuachana nazo. suala la maendeleo ya jimbo na wageni wanaofika kwenye jimbo kama mbunge anapaswa kushiriki vyema pasipo kujipendekeza. habari za kusema joshua hakupaswa kukutana na Mh Magufuli ni za kijinga maana pengine kwa kukutana huko ndo anaweza sasa kuongea naye na pengine kumwambia abt wat yu re saying. otherwise tuache siasa za karne ya 10 wakati tupo karne ya 21.



Someni Kabla Hamjajibu, Mimi Joshua simjui Kiundani wala Sina Chuki naye, Nimetathmini yaliyotokea na Haivumiliki. Kama anajitambua alitakiwa Amponde Magufuli, Huwezi Kukubali Kutumiwa kama, "Condom" Kuwatukana wenzako waliokufikisha ulipo. Na Pia kwa yaliyokuwa yakiendelea Huko Dar es salaam na Kilombero, Joshua Nassari hakupaswa kukutana na Magufuli. Ingekuwa Halima Mdee Ni dada yake Nassari angeenda Kukutana na aliyemweka Rumande kwa sababu za Kishenzi? Sasa hilo ndio naona lilikuwa Kosa Kubwa na Ujinga wa Nassari.
 
Mfano ukiwa unatembea barabarani ukiwa na familia yako ,mtu akamsifia meo kuwa kapendeza,is this a crime ee? Sasa mimi naona kwanza you Ukawa are favoured highly,mkuu wa nchi mpaka akuone na kukusifia si jambo dogo,huyu mtoto mnataka kumkatisha tamaa ili apunguze kasi ya utndaji,shame on you, wewe ndo uende utakako,mkmbizi mkubwa, hapa sasa hivi tunaangalia utendaji sio siasa tena, wabunge waliokamatwa wataface chombo husika ili kiwape haki , na haki hiyo inaweza kuwa positive au negative, by the way nani alikuambia eti mtu afanye makosa halafu kwa kuwa ni nani sijui wa chama gani ,asguswe, there is no body tall enough kuzidi sheria, sasa Nasari asimashe shughuli za jimbo kwa sababu waitara na halima mdoo wako rumande, inahusu, tena mna bahati hata
 
Niliona tetesi Jana, za habari ya Magufuli akimsifia Joshua Nassari, Kuwa Ni Kijana safi, ambaye Usoni ni Chadema lakini Ndani ni CCM. Haya yalikuwa Ni matusi ya Magufuli kwa Chadema kumtumia Nassari. Ni aibu sana na ni Unafiki Kusema ati mtu safi anayefanya Mema na anayetenda haki Ndani Ni CCM. Ni CCM ipi? Iliyoiba Ushindi wa Urais Bara? Iliyofuta Ushindi wa Zanzibar? Inayohaha Kila Mahali Kuiba Nafasi za Umeya? Iliyowarudisha wezi wote wa Escrow kwenye madaraka? Iliyokalia Uchafu wa Muhimbili, badari, TRA etc? CCM ipi ambayo huyu anazungumzia?

Najua Siku za Nyuma, Mwenyekiti Mbowe alishahudhuria na Kumsifia Kikwete na Magufuli katika Ufuunguzi wa Barabara. Lakini hakufanya hivyo wakati Wabunge na Madiwani wa Chadema wakiwa wamekamatwa na Kufuunguliwa Kesi za Kishenzi. Alichokosea Nassari ni Timing, Kuwepo kwake Ziara za Magufuli kama Kimalaya fulani, Kumemfanya Magufuli amtumie sawia kujihalalisha na Kutukana Vyama.

Joshua Nassari bwana mdogo, Nikuambie Kuwa alichokupa Magufuli sio Sifa Ni Matusi, Nimekuona Kwenye Gazeti Ukichekelea kama juha, kwa sababu hutumii akili. Wakati akina Halima Mdee, Wabunge na Madiwani wa Chadema wakiwa Rumande wewe unapeleka maninii kwenye Ziara za anayetuma unyama huu.

Na Kama Ulilazamika Kwenda, Ulitakiwa Palepale baada ya Kikao Ukanushe, "Sifa" Zile na Useme wewe Upo pale Kama mbunge wa UKAWA na Huoni sawa Kufananishwa na CCM.

Mwisho Nikuambie Nassari Mwanangu, Ulichofanya Ni sawa na Kuwapiga Mateke ya Puani na Masikio, watu mmoja mmoja wa Chadema waliopigwa na Polisi, waliowekwe jela, waliokesha waliotoa fedha, waliokupigania kuwa Mbunge. Ukitaka Kujua CCM hawana Maslahi Na wewe Mwangalie Ole Sendeka! And you are very light weight compered to many! Hata Nikikusikiliza Bungeni Joshua Wewe bado Kabisa Kukua, angalia Usijinyonge Kisiasa.

Na Kwa Ukawa Kama Josua Hatatubu, Mvumilieni amalize Muda wake, lakini akimaliza aende atakako. Msimpe tena Tiketi ya Kugombea Ubunge Arumeru. Ni bora jimbo lipotee Kuliko kuwa na Mbunge anayesaliti Wenzake waliompigania
Umesema ni tetesi,wacha mimi nipite sina muda.
 
Noted mimi natokea Meru ni muda tu haujafika he has to quit! No compromise na anayemzika mazima ni mkuu wa Wilaya huyu ametokea kuwa karibu sana na wana Meru kuliko hata mbunge na mkuu huyu wa wilaya ana tengeneza njia nyeupe kwa mgombea wa ccm atakayekuja. Nasari haonekani ibadani wala kwingineko. .....anyway mambo yake ni complicated sana. CDM bado tunaipenda SANA
Haonekani ibadani,hiyo ni hoja dhaifu sana, kazi ya mbunge siyo kuhudhuria ibada
 
Back
Top Bottom