Dume la Mende
JF-Expert Member
- Mar 23, 2011
- 423
- 64
Na Flora Amon
MCHUMBA wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Willibrod Slaa, Bi. Josephine Mushumbusi, amekiri kumtumia ujumbe mfupi wa simu (SMS) Mbunge wa viti Maalumu Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Stella Manyanya, huku akikanusha kumtukana.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, Bi.Mashumbusi alisema kabla ya mbunge huyo kumtuhumu kuwa ametumiwa ujumbe wa matusi angefafanua kwanza kwa kusoma ujumbe aliotumiwa.
Alisema hawezi kukataa kumtumia mbunge huyo sms lakini haukuwa wa matusi kama alivyodai.
"Ujumbe wangu niliandika kuwa 'aache kuwa mshabiki bali aongelee uhalisia na nadharia kwa sababu wananchi walipo kijijini kwake ni masikini na wana maisha magumu,' hilo ni tusi?" alihoji Bi.Mushumbusi.
Alisema yeye alishaenda kijijini alikotokea Mwandisi Manyanya ambapo wananchi wake wana maisha magumu hali ambayo yeye ilimtia uchungu.
Alisema mbunge huyo akisimama kuchangia hoja achangii kama mtu mwenye wananchi walio na maisha magumu bali yeye ni mshabiki hali ambayo inamshgaza.
"Ninavyoelewa wanawake wasomi wanajadili mambo ya kisomi, lakini yeye akiwa katika kujadili hoja hajadili kama mwenye uchungu na wananchi wake bali anajadili ushabiki kitu ambacho kwa sasa kimepitwa na hakileti maendeleo," alisema.
Aliongeza kuwa jinsi anavyomjua mbunge huyo laiti kama angekuwa amemtukana basi angemfikisha katika vyombo vya sheria.
Akichangia bajeti ya waziri mkuu 2011/2012 Mwandisi Manyanya alisema alipokea ujumbe mfupi wa matusi kupitia simu yake ya mkononi kutoka kwa Bi.Mshumbusi.
Source: Majira