Josephine akanusha madai ya Mbunge

Status
Not open for further replies.

Dume la Mende

JF-Expert Member
Mar 23, 2011
423
64
Na Flora Amon

MCHUMBA wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Willibrod Slaa, Bi. Josephine Mushumbusi, amekiri kumtumia ujumbe mfupi wa simu (SMS) Mbunge wa viti Maalumu Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Stella Manyanya, huku akikanusha kumtukana.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, Bi.Mashumbusi alisema kabla ya mbunge huyo kumtuhumu kuwa ametumiwa ujumbe wa matusi angefafanua kwanza kwa kusoma ujumbe aliotumiwa.

Alisema hawezi kukataa kumtumia mbunge huyo sms lakini haukuwa wa matusi kama alivyodai.

"Ujumbe wangu niliandika kuwa 'aache kuwa mshabiki bali aongelee uhalisia na nadharia kwa sababu wananchi walipo kijijini kwake ni masikini na wana maisha magumu,' hilo ni tusi?" alihoji Bi.Mushumbusi.

Alisema yeye alishaenda kijijini alikotokea Mwandisi Manyanya ambapo wananchi wake wana maisha magumu hali ambayo yeye ilimtia uchungu.

Alisema mbunge huyo akisimama kuchangia hoja achangii kama mtu mwenye wananchi walio na maisha magumu bali yeye ni mshabiki hali ambayo inamshgaza.

"Ninavyoelewa wanawake wasomi wanajadili mambo ya kisomi, lakini yeye akiwa katika kujadili hoja hajadili kama mwenye uchungu na wananchi wake bali anajadili ushabiki kitu ambacho kwa sasa kimepitwa na hakileti maendeleo," alisema.

Aliongeza kuwa jinsi anavyomjua mbunge huyo laiti kama angekuwa amemtukana basi angemfikisha katika vyombo vya sheria.

Akichangia bajeti ya waziri mkuu 2011/2012 Mwandisi Manyanya alisema alipokea ujumbe mfupi wa matusi kupitia simu yake ya mkononi kutoka kwa Bi.Mshumbusi.

Source: Majira
 
Kama hiyo ndio message basi Eng Manyanya ni nyanya kweli; kwa magamba yule sasa amekomaa na anaona kumkumbusha umaskini ni kosa
 
Hivi kumbe hata kupashana kwenye siasa kupo? nivizuri kwamaendeleo ya taifa! na wengine wenye tabia za kutojali kama wao ni kina mama tunaowategemea kuionea Huruma nchi endelea kuwapa vijembe hivyo mama, usimsahau Makinda
 
Josephine hakuwa na sababu ya kumtumia sms hiyo kwani anamjui vema nimuongea hovyoo.
 
MCHUMBA wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Willibrod Slaa, Bi. Josephine Mashumbusi, amekiri kumtumia ujumbe mfupi wa simu (SMS) Mbunge wa viti Maalumu Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Stella Manyanya, huku akikanusha kumtukana.

Alisema hawezi kukataa kumtumia mbunge huyo sms lakini haukuwa wa matusi kama alivyodai.

"Ujumbe wangu niliandika kuwa "aache kuwa mshabiki bali aongelee uhalisia na nadharia kwa sababu wananchi walipo kijijini kwake ni masikini na wana maisha magumu,"hilo ni tusi? alihoji Bi.Mashumbusi.
Ushauri wa bure kwa Dr.
Reign in your better-half before she gets out of hand.
Stella Manyanya ni mbunge na mheshimiwa whether unamheshimu or not.
Aidha nampa chngamoto Josephine ambaye ni member humu , amuandikie na Mama Salma , naye anatoka sehemu si mbali na huko.Kwa vile Mumewe ni Rais, wanavijiji wote Tanzania ni watu wake , masikini na tajiri.
Na hapo ndo anaweza kushangaa nyani kula mahindi bichi.
 
Manyanya pumba sana nilimheshimu ila sasa ameliwa; kumbe hata katika tume ya mwakiembe alikuwa bendera fuata upepo
 
Hivi slaa ametajwa wapi kwenye thread hii? anayezungumzwa ni Josephine, mjadala unaelekezwa kwa Dr.!!!!! hivi can't we stick to the focus alone? acha 'president' wetu atulie.....acheni hizo. we unayemponda kuhusu usafi wake kwenye ndoa, unadhani kwa kufunga ndoa tu ndio ticket ya mbinguni? No Jesus, No heaven! (life -Jesus = O).
 
Kama vipi Manyanya na yeye atoe ujumbe aliotumiwa na Josephine, kinyume chake ujumbe wa mama yetu Josephine unasimama kama ulivyo na kumuacha wazi Manyanya kuwa ana hoja nyepesi za kujadili watu na sio uwezo!
 
Naombeni namba ya Makinda Jaman, nina ujumbe maalum kwake.
 
Huyu nae kumbe kumsaliti mumewe kote huko alikuwa anataka umaarufu.
si alidhani mchumbake ataukwaa urais..dah fistlady na kuropokaropoka wapi na wapi.Nilichoka siku tunajibishana naye humu akatuambia dawa yetu iko motoni ole wetu wakishika nchi..nikajua huyu mmama siyo.
 
Kwenye mahakama hayo aliyoyaandika huyu Josephine yanaweza kabisa yakawa ni matusi.
 
Halafu hapa ndio josephine kalikoroga kabisaa, naona kiswahili kinampiga chenga, hii ni contradiction ya hali ya juu: "aongelee uhalisia na nadharia",

halisi adjective
1 exact, accurate, definite, precise, literal
2 genuine, true, positive

nadharia , pl nadharia { English: theory }
 
Na Flora Amon

MCHUMBA wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Willibrod Slaa, Bi. Josephine Mushumbusi, amekiri kumtumia ujumbe mfupi wa simu (SMS) Mbunge wa viti Maalumu Mkoa wa Ruvuma Mhandisi Stella Manyanya, huku akikanusha kumtukana.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, Bi.Mashumbusi alisema kabla ya mbunge huyo kumtuhumu kuwa ametumiwa ujumbe wa matusi angefafanua kwanza kwa kusoma ujumbe aliotumiwa.

Alisema hawezi kukataa kumtumia mbunge huyo sms lakini haukuwa wa matusi kama alivyodai.

"Ujumbe wangu niliandika kuwa 'aache kuwa mshabiki bali aongelee uhalisia na nadharia kwa sababu wananchi walipo kijijini kwake ni masikini na wana maisha magumu,' hilo ni tusi?" alihoji Bi.Mushumbusi.

Alisema yeye alishaenda kijijini alikotokea Mwandisi Manyanya ambapo wananchi wake wana maisha magumu hali ambayo yeye ilimtia uchungu.

Alisema mbunge huyo akisimama kuchangia hoja achangii kama mtu mwenye wananchi walio na maisha magumu bali yeye ni mshabiki hali ambayo inamshgaza.

"Ninavyoelewa wanawake wasomi wanajadili mambo ya kisomi, lakini yeye akiwa katika kujadili hoja hajadili kama mwenye uchungu na wananchi wake bali anajadili ushabiki kitu ambacho kwa sasa kimepitwa na hakileti maendeleo," alisema.

Aliongeza kuwa jinsi anavyomjua mbunge huyo laiti kama angekuwa amemtukana basi angemfikisha katika vyombo vya sheria.

Akichangia bajeti ya waziri mkuu 2011/2012 Mwandisi Manyanya alisema alipokea ujumbe mfupi wa matusi kupitia simu yake ya mkononi kutoka kwa Bi.Mshumbusi.

Source: Majira

huyu mama ni mpiganaji mzuri sana ilikuwaje akakosa viti maalumu? maana anajituma sana kuliko hata wale wabunge wa viti maalumu. hivi hakuna nafasi ilibaki apewe huyu?
 
Mimi nashauri siku nyingine mkitaka kuandika habari za huyu mwanamke muandike kabisa Josephine Kimada wa Slaa badala ya kusema tu josephine, wengine tunadhani ni wachumba zetu. Pia na tabia ya magezeti kuandika mchumba wa Slaa mimi naona kama yanalenga kumharibia mzee huyu, maana hadi leo jamani awe na mchumba? Josephine ni Kimada wa Slaa sio mchumba jamani acheni kumdharau mbunge mstaafu.
 
huyu mama ni mpiganaji mzuri sana ilikuwaje akakosa viti maalumu? maana anajituma sana kuliko hata wale wabunge wa viti maalumu. hivi hakuna nafasi ilibaki apewe huyu?

Yeye na Rose Kamili wote wapewe? na mwenyekiti naye angeleta wa pili.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom