Uchaguzi 2020 Joseph Selasini, aviangukia vyama kuwasamehe vijana walioshindwa kura za maoni baada ya kuvihama vyama vyao

Mbunge wa Rombo aliyemaliza muda wake Joseph Selasini, ameviomba vyama vyote nchini kuhakikisha vinawapokea vijana wote waliohama vyao vyao na kuhamia vyama vingine lakini wakashindwa kwenye kura za maoni kwa kuwa walishaonesha wanao uwezo wa kufanya kazi.

Selasini ametoa kauli hiyo hii leo Agosti 7, 2020, Jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza kwenye mkutano Mkuu wa chama cha NCCR-Mageuzi na kuongeza kuwa vijana hao wanapashwa kuwapokea na kisha kuwalea na kuwarekebisha kwenye makosa yao na kuwapa nafasi za uongozi.

"Naviomba vyama vyote, chama changu cha NCCR-Mageuzi, CCM, CHADEMA tusiwatupe vijana, hata vijana ambao walihama kutoka CHADEMA kwenda CCM wakaenda kushindwa kwenye kura za maoni, tunajua vijana wanavyotangatanga hata katika kutafuta uchumba, wanatafuta fursa fungueni milango hao vijana warudi waweze, kufanya kazi ya Watanzania" amesema Selasini.

CC: Lijualikali.
Kwani wameanza kutapatapa? Wafanye hata biashara si huwa wanahamasisha vijana wengine wajiajiri? Kwa nini inakuwa ngumu kwao kujiajiri?
 
Wajifunze kutokana na Lipumba na Mrema. “Hawakuniachia hata Kiraracha yungu” Ndivyo alivyosema Mrema alivyogundua wakati wa local Gov elections kuwa hata kijiji chake ccm wamekichukua! Hahaha!Ndivyo walivyo wajanja hao! Propesa ameachwa kwenye mataa.
 
Nasikitika dalalali wa accacia wa mabeberu kwenye madini yetu eti nae mgombea uraisi kwa tiketi ya chadema
 
Kwahiyo ni rasmi sasa siasa ndio kila kitu..tulikosea sana tulipoipa siasa thamani kubwa kuliko taaluma ..
Badala washauriwe kutumikia fani zao kuna mtu anawaombea wasitupwe
Na Hasa Silinde anajifanya yeye eti Mchumi Mahiri...si aanze sasa kutoa mihadhara kwenye Vyuo Vikuu mbalimbali duniani?😀

Na yule mtoto wa mjini naye aingie na manati yake mjini aanze kupora bodaboda😀
 
Huyu mzee ni mpumbavu aliyepindukia. Mods nisameheni. Kwa iyo siasa zinazobeba hatma ya maisha yetu watanzania yeye anataka tuzichukulie kama fursa za kimaisha?????

Huyu mtu bora aliondoka Chama makini chadema. Kwa akili hizi anastahili kuwepo huko NCCR au CCM ambako watu wanachukulia hatma za maisha zetu kama fursa zao za kiuchumi.

Kanipa hasira sana. Ndo mana nchi hii hatuendelei kwa kweli. Akili kama hizi hazitakiwi kabisa kuwepo kwenye kada ya uongozi
yaani zamani nilikuwa na heshimu watu wa kasikazini kwa kuwa na akili na misimamo ya maana lakini utawala wa Magufuli umesaidia kujuwa watu kwa uhalisia wao. na kwasababu hiyo nimegunduwa ujinga hauna kabila. hata kasikazini tumeona Magufuli na polepole wakirubuni wajinga kibao kwa ahadi hewa.
 
Mbunge wa Rombo aliyemaliza muda wake Joseph Selasini, ameviomba vyama vyote nchini kuhakikisha vinawapokea vijana wote waliohama vyao vyao na kuhamia vyama vingine lakini wakashindwa kwenye kura za maoni kwa kuwa walishaonesha wanao uwezo wa kufanya kazi.

Selasini ametoa kauli hiyo hii leo Agosti 7, 2020, Jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza kwenye mkutano Mkuu wa chama cha NCCR-Mageuzi na kuongeza kuwa vijana hao wanapashwa kuwapokea na kisha kuwalea na kuwarekebisha kwenye makosa yao na kuwapa nafasi za uongozi.

"Naviomba vyama vyote, chama changu cha NCCR-Mageuzi, CCM, CHADEMA tusiwatupe vijana, hata vijana ambao walihama kutoka CHADEMA kwenda CCM wakaenda kushindwa kwenye kura za maoni, tunajua vijana wanavyotangatanga hata katika kutafuta uchumba, wanatafuta fursa fungueni milango hao vijana warudi waweze, kufanya kazi ya Watanzania" amesema Selasini.

CC: Lijualikali.
Huko walikohamia kuna waliowakuta ambao wametumikia Vyama vyao Kwa Mapenzi, Utii, Shida na Raha na Uvumilivu. Waliokutwa ndio Wanàstahili Uongozi . Leo Wageni wasiojua ABC za Vyama walivyohamia Wapewe Uongozi Kwa Lipi? au Pongezi ya Kusaliti Vyama vilivyotoka? Kama wamehamia huko Kwa Mapenzi ya dhati wapimwe Kwa Kunyimwa Uongozi/ Madaraka Kwa 5 Years.
 
Mbunge wa Rombo aliyemaliza muda wake Joseph Selasini, ameviomba vyama vyote nchini kuhakikisha vinawapokea vijana wote waliohama vyao vyao na kuhamia vyama vingine lakini wakashindwa kwenye kura za maoni kwa kuwa walishaonesha wanao uwezo wa kufanya kazi.

Selasini ametoa kauli hiyo hii leo Agosti 7, 2020, Jijini Dar es Salaam, wakati akizungumza kwenye mkutano Mkuu wa chama cha NCCR-Mageuzi na kuongeza kuwa vijana hao wanapashwa kuwapokea na kisha kuwalea na kuwarekebisha kwenye makosa yao na kuwapa nafasi za uongozi.

"Naviomba vyama vyote, chama changu cha NCCR-Mageuzi, CCM, CHADEMA tusiwatupe vijana, hata vijana ambao walihama kutoka CHADEMA kwenda CCM wakaenda kushindwa kwenye kura za maoni, tunajua vijana wanavyotangatanga hata katika kutafuta uchumba, wanatafuta fursa fungueni milango hao vijana warudi waweze, kufanya kazi ya Watanzania" amesema Selasini.

CC: Lijualikali.
Yeye mwenyewe aombe msamaha
 
Kwa namna moja au nyingine kuna pointi.
Mtu hujifunza zaidi pale anapofanya makosa.
Tusishindwe na ccm imewapokea walio wao hadi Lowasa.
Nasi tuwapokee lakini wakae karantini...chini ya uangalizi kwa muda wa kutosha
Hahahaaa....... Ngumu kumeza
 
Back
Top Bottom