Nadhani tatizo si kukemea au kutokumea bali kuwa na serikali iliyoko madarakani ikiundwa na watu wasio na maadili. Siku hizi Tanzania imekuwa dampo la kila uchafu hasa miigizo. Tuna vituo vya TV vyenye kutoa huduma chafu kwa wateja. Tuna vipindi vya kisagaji kama Mikasi na utitiri wa magazeti ya udaku. Kenya hawana magazeti ya udaku, matangazo machafu wala vipindi vya hovyo kama Tzania. Nadhani tatizo ni jamii ya kitanzania kupenda vitu vya hovyo na kuchukia vitu muhimu. Iwapo rais mwenyewe hana maadili hadi kuwaambiwa wanafunzi wanaopata mimba eti ni kutokana na kiherehere chake huku wabunge wake wengi wakiwa wavuta bangi na walevi unategemea nini? Hili si tatizo la upinzani bali CCM.