Yaani huwa najiuliza waliomchagua walitarajia nini kutoka kwake, ila anachofanya ndio kilicho ndani ya uwezo wake.
Huo uwaziri kivuli wenyewe sijui kama anajua majukumu yake zaidi ya kuendesha mapambano na clouds kwa kutumia wasanii.
Kwenye filamu sioni mapambano yoyote, Wasanii wana vilio mpaka makoo yamekauka, matatizo ya usambazaji, Mikoani hakuna cha maana kinaendelea kuhusu filamu kila msanii analazimika kukimbilia Dar ndio aonekane anafanya kitu.
Ni mikoa mingapi ameshatembelea na kukutana na wasanii wa filamu kusikiliza matatizo yao ?
Hiyo bongo fleva anaonekana kuishupalia ili tu atekeleze mapambano yake na clouds kama mlivyoona kwenye msiba wa Ngwair.
Kesho na keshokutwa chadomo wanatarajia huyu ndio awe waziri wa utamaduni vijana na michezo.....ee Mungu tunusuru waja wako.
KUNA WABUNGE WAKISIMAMA BUNGENI UTAWASIKIA TU...KUDADADEKI......Deus Kibamba