Jokate Mwegelo: Siku hizi wazazi wanawaogopa Watoto

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,462
Akizungumza na Wanahabari, leo Ijumaa Oktoba 27, 2023, Jokate Mwegelo Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) amesema viongozi bora wanatakiwa kutengenezwa kuanzia ngazi ya chini.

Amesema “Hatuwezi kuwa na viongozi bora bila kutengenezwa, viongozi bora wanatoka kwenye familia, wanatoka kwa wazazi na walezi, jukumu hilo haliwezi kukwepeka.

“Suala la kukemea ukatili wa kijinsia hasa kwa Watoto ni jukumu la jamii pia.

“Kuna sehemu mtoto analawitiwa au anabakwa lakini mzazi ndio anakuwa kikwazo cha mtoto kupata haki.

“Wazazi wanatakiwa kushika nafasi zao za ulezi na kuongoza watoto na kuwasaidia, kipindi hiki tunaona Wazazi wanawaogopa watoto kuliko Watoto wanavyowaogopa.

“Kipindi cha nyuma ilikuwa mtoto akifanya jambo anaogopa mzazi wake lakini leo ni kinyume chake, hiyo inachangia kudhorotesha maadili, hiyo imechangia Watoto kutokaa kwenye mstari.”
 
Muongozo mh supika,hivi yeye kabla ya kuibuliwa na ccm alikuwaje? Na jeh anayo moral authority ya kuzungumza hayo? Naomba muongozo wako
 
Back
Top Bottom