Johnson Mashaka na mbio za Ubunge Ukonga

FMES,

..sasa Mashaka si CCM mwenzako halafu unamrushia tuhuma za Ukenya tena?

..huyu kijana na hizi idea zake kama unavyoona ktk speech yake hapo atawapeni shida sana humo CCM.
 
Whoever spends US$ 350,000 to become a candidate for CCM for a constituency MP is, kwa mawazo yangu, chimbuko la ufisadi. Huyu atategemea kurudisha fedha zake kwa hiyo lazima atatumia UFISADI kuzirudisha. Hakuna lingimnne hapa hawa wataongeza UFISADI. Itakuwa Kasi mpya na Ufisadi zaidi - simple nothing else.
 
Kudi Shauri,

..lakini bado haijathibitishwa kwamba Mashaka anatumia kiasi hicho cha fedha.

..inawezekana watu wanajaribu kumchafua kwa kum-link na mafisadi.
 
FMES,

..sasa Mashaka si CCM mwenzako halafu unamrushia tuhuma za Ukenya tena?

..huyu kijana na hizi idea zake kama unavyoona ktk speech yake hapo atawapeni shida sana humo CCM.

- Mkuu umeanza tena? Si majuzi tu ulisema ya personal huyataki tena vipi? Ni wapi nimemrushia tuhuma za ukenya? Mashaka ni mkazi mwenzangu mkuu wa Kinyerezi na familia yake yote ninaifahamu, ndio maana nikasema hivi anahitaji kuiweka wazi sasa ya connection yake na Kenya kifamilia,

- Ili kuepusha yaliyomkuta Mungai, kwenye kugombea NEC au umesahau mkuu?

Respect.

FMEs!
 
Mashaka haipendi Tanzania na hawapendi Watanzania .Mashaka nadhani ana nia ya madaraka zaidi kulisaidia Taifa.Mashaka kuja kwa gear hizi na kudhani kwamba kuingia CCM ndiyo atapambana na upuuzi wa CCM anapoteza muda na atachoka sana .Au labda aseme ameamua kuungana nao kutukamua sawa lakini si kwa nia ya kuleta changes huwezi kuusema ufisadi ukiwa ndani ya CCM .
 
FMES,

..sasa Mashaka si CCM mwenzako halafu unamrushia tuhuma za Ukenya tena?

..huyu kijana na hizi idea zake kama unavyoona ktk speech yake hapo atawapeni shida sana humo CCM.




CV ya John Mashaka


32 Years Old

MBA- Univesrsity of North Carolina Chapel Hill 2006
Jurist Doctrate Duke University 2004

He is an investment Banker
 
FMES,

..inawezekana kabisa sikuisoma vizuri posting yako, kwa hiyo nikateleza ktk majibu yangu.

..nimejaribu kurejea nyuma kusoma tena ulichoandika lakini sijui posting yako imepotelea wapi.

..kama unavyosema mkuu heshima mbele, tuendelee kumkoma nyani mchana kweupe,..
 
The John Mashaka Charitable Foundation is a 501 (c) (3) entity established and funded by John Mashaka, in order to fulfill his dream and desire to use the fruits of his blessings, to help people living under massive poverty, get clean water, and also provide assistance to those living with HIV/AIDS virus get free medical attention they would not otherwise obtain.
http://powerofhearing.com/mashaka/index.html

mashaka1bc.jpg
 
- Mkuu kila unapofungua kinywa unazidi kuonyesha uwezo wako wa kufikiri ulipoanzia na kuishia, kila siku unalia lia hapa kwamba Kyela unaibiwa na kuongozwa na mafisadi, hivi kweli unaweza kulinganisha maendeleo ya jimbo la Ukonga na Kyela?

- Mkuu jimbo la Ukonga lina kata nyingi zikiwemo za Kinyerezi, Kipunguni, Kitunda, Ukonga Magereza, Majumba Sita, Sitaki Shari, Segerea, Airwing na zinginezo, sasa hebu nitajie kata moja tu kati ya hizi unayoweza kulinganisha na hata jimbo zima la Kyela kimaendeleo?

- Ndio kwanza tumefungua bara bara mpya ya lami, kutoka getini Airwing yaani njia panda ya Airport mpaka gerezani Segerea kufikia Tabata unaunganisha mpaka Kimara. Mahanga sio siri ni kiongozi mchovu, lakini Ukonga sio Mahanga ambaye amekaa bungeni kwa miaka minne tu so far, hili jimbo ni bomba kabla hata yeye kuhamia Ukonga.
- Eti mkuu jimbo lenye vitega uchumi na kutoa ajira kwa wananchi jimboni kama Julius Nyerere International Airport, FFU HQ, JWTZ-Airwing HQ, JWTZ-Mizinga Squad, Gereza Kuu la Ukonga, Gereza Kuu la Segerea, Viwanda vya nguo Kiltex na Sungura tex, Kiwanda maalum cha kutotota vifaranga vya kuku, Segerea Catholic Seminary, unasema unaweza kulinganisha hili jimbo na Kyela? Hivi unajua hili jimbo lina secondary ngapi mkuu? Hebu nitajie jimbo moja tu Tanzania nzima linaloweza kulifikia jimbo hili la Ukonga kwa maendeleo?

- Na pia jimbo hili tunajivunia sana kwa kuwa na kata ninayotoka ya Kinyerezi/Sitakishari ambayo ni a home for national celebrities kama the sitting national leaders Waziri Wasirra, Mkuu wa Itifaki Balozi Itatiro, RC wa sasa Mbeya Mwakipesile, Mbunge wa Kawe Rita Mlaki, Managing Director Azania Bank Charles, Managing Director Wananchi Bank Mzee Mkwawa, pia tuna wastaafu wa taifa kama familia ya waziri wa zamani wa afya Mzee Sterling, Mzee Apiyo, familia ya marehemu Waziri Itatiro, familia ya marehemu makamu wa mwenyekiti wa kwanza wa Chadema Mzee Ngwilulupi, familia ya Balozi wetu wa zamani Nigeria Marehemu Mwasakafyuka, Wakuu watatu wa zamani wa Magereza Mzee Mwanguku, Mzee Mwaijande na Mzee Mwaipopo, familia ya mkuu wa polisi zamani marehemu Mzee Liani, Pia tuna wafanya biashara maarufu kama kina Mujuluzi, majority owner wa Imma, Dr. Mwaijande owner wa pharmacy maarufu pale Muhimbili hospital, kampuni kubwa ya mabasi na malori ya Mahende, Club maarufu sana Dar ya Hill-teck, pia ni a home for a former Simba player/national team Idd Pazi "Father" na pia ni a home for mimi mwenyewe Mukulu Field Marshall Es, yaani wazee wa sauti ya umeme! na Mkulu Mashaka John.

- Engineeer, hili jimbo haliwezi kuwa chovu kama lako huko Kyela not even close mkuu, msiwe mnakurupuka kurupuka jamani ulizeni kwanza, infact hili jimbo la Ukonga linaweza kuwa numero uno kwa maendeleo bongo nzima, sasa hivi kiwanja cha kujenga nyumba cha eka moja tu Ukonga kitakugharimu atleast Shillingi Millioni 20-30, sasa Engineer unasema nikitaka kununua kiwanja kama hicho Kyela kweli bei itakuwa sawa na hii ya Ukonga? Bwa! ha! ha! mkuu karibu sana Ukonga, usingoje ya kusimuliwa mkuu!

Wakuu Malafyale, Sinkala na Mkandara huuu ni wakati wa kuhamishia hii elimu tunayoipata hapa JF, katika jimbo letu badala ya kurushiana maneno machafu yasiyo na mshiko kwa masilahi ya taifa kama hao wa Kyela, na ni lazima tujihusishe sana na hii process ya kutafuta mbunge anayefaa kwa jimbo letu yaani wa kuendeleza aliyoyakuta, mimi toka jana nilipoiona hii habari ya Mashaka, nimekua nikiwasiliana na wazee wa jimbo kujua kinachoendelea na soon tutaweka msimamo hapa. Mkuu Engineer karibu sana jimboni kwetu ujifunze elimu ya maendeleo ya jimbo mkuu.

Respect.

Field Marshall Es!
mkuu mda si mrefu namimi ntakua jirani yako lakini bwa ha,ha,haa,inaonekana umetoka hill teck resort mda si mrefu mkuu kutafuna yale maji ya dhahabu.tuko pamoja mkuu
 
The John Mashaka Charitable Foundation is a 501 (c) (3) entity established and funded by John Mashaka, in order to fulfill his dream and desire to use the fruits of his blessings, to help people living under massive poverty, get clean water, and also provide assistance to those living with HIV/AIDS virus get free medical attention they would not otherwise obtain.
http://powerofhearing.com/mashaka/index.html

mashaka1bc.jpg
kama kweli nilijua huyu panya atakuja na story kama hizi mwishoni,jamani naomba niulize hivi nyinyi wabongo hasa mliosoma nje hamuwezi kufanya kitu ingine zaidi ya kuwadanganya watu na hivyo visenti vyenu vya pipi kuwaibia?we john mashaka huna biashara nyingine ya kufanya na hizo vx zako 4 na dola 350,000 zaidi ya kununua ubunge?si lazima wote muwe wanasiasa,halafu chama chenyewe ccm unahitaji nini cha zaidi humo?si ufungue hata travel agency au jenga hotel basi kama hela zinakuwasha,e bwana mi sina mjadala mrefu watu washamba kama hawa anaona kukaa marekani basi we ndio mungu utafanya lolote unalotaka,kama muda wa kupiga box umeisha rudi home tu anzisha biashara ya matikiti maji na matango basi kama obama wa urusi.
 
Kwa Hisani ya Bongo Celebrity Blog naweka Mahojiano ya Bwana Mashaka aliyoyafanya na Blog hiyo tarehe 2/Aprili/2008;

Ingawa vyombo vya habari mbalimbali,katika nyakati tofauti tofauti,vimekuwa vikiandika habari zake na yeye kualikwa katika mihadhara mbalimbali kuzungumzia masuala ya kujitolea, umasikini,maradhi na mambo mbalimbali yahusuyo ubinaadamu,yawezekana kabisa ukawa hujawahi kulisikia jina lake wala kuiona sura yake.


John Mashaka ni kijana mdogo wa miaka 30 ambaye kama walivyo watanzania wengine wengi, anakerwa na hali za umasikini,ujinga na maradhi zinazowakabili mamilioni ya watanzania hivi leo.Tofauti yake na watanzania wengine wengi ni kwamba yeye ameamua kujitoa mhanga kusema na pia kusaidia kwa hali na mali anapoweza.Kwa maana nyingine,John Mashaka ni kijana ambaye anajaribu kuamsha upya hali ya kujitolea bila kujali sana hali ya utajiri aliyo nayo.Anasisitiza kile ambacho tumekuwa tukiambiwa tangu enzi na enzi;Kutoa ni moyo na wala sio utajiri.


Pamoja na hayo,hivi karibuni, habari zake zilipotolewa kwenye blog maarufu ya Issa Michuzi, mjadala mkubwa ulizuka kuhusu anachojaribu au alichowahi kukifanya.Kama kawaida ya binadamu,wapo waliomuunga mkono na wapo waliompinga kwa nguvu huku wakidai kwamba huenda anajitafutia tu "umaarufu" au kujifagilia njia ya kisiasa.Wengi wakawa wamemhukumu bila kumpa nafasi ya kumsikiliza.


Baada ya kusoma ule mjadala na kutafakari mambo kadhaa,BC tuliamua kumtafuta bwana Mashaka ili kufanya naye mahojiano utakayoyasoma hivi punde.John Mashaka ni nani?Je,Mashaka anajiandalia tu njia ya kuukwaa "ubunge" siku za mbeleni?Je ni kweli anakerwa kwa dhati na matatizo yanayomkabili mtanzania wa kawaida hivi leo?Vipi,inawezekana na wewe ukamuunga mkono katika anachojaribu kukifanya?You will be the Judge!Fuatana nasi katika mahojiano yafuatayo;



BC: Mashaka,Shukrani sana kwa kukubali kufanya nasi mahojiano haya.Kwanza kabisa watu wengi wangependa kufahamu kidogo kuhusu historia ya maisha yako.Unaweza kutuambia ulizaliwa lini,wapi na kisha ukasomea wapi mpaka kufikia hapo ulipo hivi sasa?


JM: Nimezaliwa na kukulia huko Tanzania miaka 30 iliyopita, na hatimaye kusoma shule ya msingi na sekondari nchini Kenya kabla ya kujiunga na elimu ya juu nchini Marekani kwa shahada za kwanza na zingine za juu.


BC: Hivi sasa hapo nchini Marekani unajishughulisha na nini haswa? Unafanya kazi gani?


JM: Nafanya kazi kama Investment Banker. Ila, sitapendelea elimu yangu, au nafasi yangu katika jamii, ihusishwe na kazi zangu au wito kwa binadamu wenzangu. Sipendelei kuyazungumzia kwa sababu haya yote ni batili tunapolizungumzia suala la ubinadamu.
Let my character and deeds decide on who I am. Elimu isiyotumika katika njia sahihi ya kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya kijamii inakuwa ni mzigo mkubwa, nafasi au cheo isiyo na manufaa kwa binadamu wenzetu inakuwa kero.
Wapo vijana wengi wenye elimu, na kazi nzuri kuliko mimi ambao wanahitaji msukumo au changamoto ili nao pia wasaidie nyumbani. Ila nikiingia ndani sana kuhusu kazi ninazozifanya nahisi kwamba nitakuwa nakiuka imani zangu na baraka za Mwenyezi Mungu, na kuikaribisha jeuri.


BC: Mara nyingi waafrika tumekuwa tukitupiwa lawama kwamba hatuna moyo wa kujitolea(volunteerism) ikilinganishwa na wenzetu wa nchi za magharibi. Je unakubaliana na lawama hizi na kama ndio unadhani ni kwanini waafrika hatupendi au hatuko mstari wa mbele katika kujitolea? Nini kinaweza kufanyika ili kubadili hali hiyo?


JM: Waafrika tumsilaumu shetani.Shetani ni sisi wenyewe. Kumsaidia mwenzio inakuwa shida kwa kuhofia atakushinda bila kufahamu ya kwamba shida inayomkabili mwenzio hivi leo usiposaidia kuitatua itakuja kukuathiri hata wewe mwenyewe kesho.Siyo lazima uwe na hela au tajiri ndio uweze kusaidia.Yeyote anaweza kusaidia. Kuna watoto wengi wanaoharibikiwa maishani kwa kukosa muongozo mzuri ili wawe raia wema, na hii inaweza kutekelezwa na mtu yeyote mwenye moyo wa kujitolea siyo lazima uwe na hela nyingi kama ambavyo wengi tunadhania.
Sioni kitu cha ajabu kwa mtu kujitolea kwani ni jambo la kawaida huku katika nchi za magharibi au Ulaya kama ilivyozoelekwa miongoni mwa wengi.Ajabu ni kwamba tunaporudi kusaidia nyumbani kila mtu wazo lake ni ubunge au siasa. Nadhani hii kasumba inatokana na mazingira mtu anayoishi ambayo yanatawaliwa na wanasiasa.
Maendeleo katika jamii hayaletwi na mwanasiasa, yanaletwa na watu kama mimi na wewe.Kujitolea hali na mali ndio dawa pekee ya kukomesha ujambazi, uzururaji na pia wimbi la watoto yatima wanaojitokeza kila kona,kila kukicha.
Hii ndio dawa pekee dhidi ya umasikini siyo kuwatazama macho viongozi tukidhania kwamba watatuletea miujiza. Uongozi lazima uanzie kwenye nafsi zetu. Sikuzaliwa na chochote, maishani nimesaidiwa, sikusaidiwa na mwanasiasa hata mmoja nilisaidiwa na raia wa kawaida.


BC: Tangu habari zako zianze kusambaa kupitia vyombo vya habari na blogs mbalimbali za watanzania, kumekuwepo baadhi ya watu ambao wamekuwa wakidai kwamba wewe unasaidia yatima ili kujiwekea mazingira ya kugombea nafasi za kisiasa baadaye(kama ubunge) au kujipatia tu umaarufu na mambo kama hayo.Unasemaje kuhusu shutuma au habari kama hizo?


JM: Kuna umaarufu wa aina mbili.Umaarufu unaotokana na wema (vipaji maalum) na ule unaotokana na uovu. Sitapenda umaarufu wa aina yoyote, kwa maana nikiwa maarufu kutokana na wema, nitakuwa natekeleza jukumu langu kama binadamu.Wote tumeumbwa ili tupendane na kutenda wema. Namuomba Mungu anipe moyo wa unyenyekevu ili niepukane na tabia mbovu kama kiburi ambayo ni matunda ya umaarufu.
Nakumbuka mwandishi wa habari Tanzania aliniuliza swali kama hilo, lakini kwa kifupi ni kwamba mabadiliko katika jamii siyo lazima yaletwe na mbunge au mwanasiasa.
Wote tuna majukumu ya kuibadilisha sura za jamii zetu, nchi yetu, bara letu na pia dunia kwa ujumla. Raia wa kawaida anayeguswa na matatizo yanayoikabili nchi lazima atatafuta namna ya kusaidia.
Hebu niambie, utafurahi kumuona mtoto anakufa kwa kukosa matibabu ilhali hela unayo mfukoni? Ni lazime uwe mwanasiasa ndo uchungu ukuingie?
Haja ilipokuwepo Afrika Kusini, Nelson Mandela alijitolea na kupata mateso ili nchi yake iondokane na ubeberu. Haja ilipokuwepo nchini India, Mahatma Ghandhi alijitolea nafsi yake ili nchi yake iondokane na ukandamizaji toka kwa mwingereza. Kadhalika Marekani walibarikiwa kumpata Martin Luther King ambaye aliyatoa maisha yake kwa ajili ya watu weusi.
Unapoishi katika mataifa kama haya kwa kipindi kirefu na kurudi nyumbani kuiona hali ya kawaida, utajiona kama msaliti usiposaidia.
Nadhani hata Yesu alipokuwa duniani alitupiwa shutuma za kila rangi akafika hata kusulubiwa. Sitashangaa nikikimbiwa na ndugu hata marafiki kutokana na imani yangu. Hakika sitaweza kuikana ukweli kwa ajili ya urafiki wa kibinadamu.

mashaka2bc.jpg


BC: Je shutuma kama hizo huwa zinakufanya wakati mwingine utake kukata tamaa kuhusu misheni yako ya kusaidia ma-yatima na wengine wasiojiweza?


JM: Siwezi kukata tamaa kutokana na shutuma kutoka kwa watu wachache kwani mambo kama haya ni ya kawaida maishani. Wapo wanaokutakia mema, na wengine wanaoomba usiamke usingizini, lakini yote ni ya Mungu. Watu kama hao wapo, nawaombea Mungu awaguse nao wauone mwanga na kuweza kujitolea kuliokoa taifa lao na binadamu kwa ujumla.
Sidhani kama kuna shutuma, kwa maana sijaenda kwa mtu kuomba anisaidie chochote, yote nafanya mwenyewe kutokana na kipato changu kidogo. Na iwapo wapo watu wa aina hiyo, basi shutuma zao nitazichukulia kama msukumo wa kutafuta ufumbuzi zaidi ili nao pia waguswe ili badala ya kushutumu washirikiane na mimi katika hizi shuguli za kutafuta amani.
Nitafurahi sana kukutana na mtu hata mmoja mwenye rekodi ya ubinadamu ambaye anaweza kujadili maswala kwa ufasaha ili tutafute ufumbuzi zaidi wa matatizo yetu ya kijamii.


BC: Kwa mtazamo wako,kibinadamu na kisha kitaaluma kama mchumi, unadhani umasikini uliotapakaa hivi leo barani Afrika na sehemu zinginezo nyingi duniani, unatokana na nini? Nini kiini cha tatizo la umasikini?


JM: Sitaki niingie katika kundi la watu wanaobeza au kulaumu kila kitu, umasikini na vita barani Afrika kwa ukoloni au nchi za magharibi. Uhuru tumeupata miaka zaidi ya arubaini iliyopita. Mpaka leo hatujatambua kwamba nchi yetu ndio moja ya nchi matajiri katika bara la Afrika.Bahari ya India inatosha kuifanya Tanzania nchi tajiri kuliko nchi zote Afrika ikiwa tutaweka mikakati mizuri na uongozi mzuri wa kuitumia. Tazama Dubai, ina nini zaidi ya Tanzania? Kitega uchumi chake kikubwa ni bandari zake.
Vivutio vyetu vya kitalii na kihistoria vinatosha kuiweka Tanzania katika kundi la nchi zenye nguvu zaidi kiuchumi. Amani na utulivu tulionao nchini vinatosha kuwakaribisha wawekezaji toka pande zote za dunia.
Ukoloni isiwe kigezo. Kwani nchi kusini mwa Afrika kama Zimbabwe ilipata maendeleo makubwa chini ya utawala wa kigeni, hadi pale Mugabe alipoibuka upya na sera zake za karne ya kumi na saba na kusambaratisha uchumi na kuifanya Zimbabwe kuwa kicheko cha uongozi bora Afrika.
Vitu ambavyo ningependa kuvizungumzia ni , bidii ya kazi, uadilifu, uzalendo na upendo kwa binadamu wenzetu. Mzalendo hawezi kuiba mabillioni ya fedha toka nchi masikini kama Tanzania na kuzirudisha Uingereza, Uswisi na kwingineko zilikotoka ilhali watu wake wanakufa na njaa.
Mtu mwenye upendo katika nafsi yake, kamwe hawezi kuishi kama mfalme na kuzidi kuiuza nchi yake ilhali amezungukwa na ma millioni ya watu wasio na matumaini maishani, wanaoishi kwa miujiza siku hadi siku
Israel ni nchi ndogo sana, haina chochote (utajiri)kulinganisha na Tanzania. Hii nchi imezungukwa na "lethal and vicious enemies", lakini licha ya haya yote , ndio moja ya nchi zilizoendelea sana duniani. This clearly tells us that, where there is need there is a way. If our leaders had the passion and love for their country, then we would have been far by now.
Rather than being pessimistic, I am optimistic, and very confident, that our current president will soon tap the talents he has at his disposal to implement his economic policies stagnated by the corrupt individuals who are giving him headache day and night.


BC: Sina uhakika kama unafuatilia kwa karibu siasa za Tanzania. Pamoja na hayo ningependa kukuuliza; unadhani Tanzania hivi leo inapiga hatua kwenda mbele au nyuma kunako suala zima la kuleta maendeleo kwa mwananchi wa kawaida?


JM: Kashfa ya Richmond imeleta matumaini makubwa kuona Bunge likijadili kwa uzalendo wa hali ya juu hili suala la aibu, ambapo chama tawala na upinzani vilishirikiana kwa maslahi ya nchi. Huu ni ukomavu mkubwa hasa kwa nchi inayoendelea kama Tanzania.
Kinachoididimiza Tanzania kwa upande mwingine ni mwananchi mwenyewe.Unapouza kura yako kwa chai kikombe kimoja, unauza haki za watoto wako kupata elimu bora, huduma nzuri za kiafya na mengineyo. Unapompigia kura kiongozi fisadi ambaye miaka nenda rudi anajilimbikiza utajiri unategemea nini?
Rais siyo mungu, ni binadamu.Lazima wananchi wampe viongozi wema wenye uzalendo na kujituma. Hawezi kufanya kila kitu mwenyewe, anahitaji usaidizi. Wananchi inabidi wamchague kiongozi kutokana na utendaji wake, siyo kutokana na chama chake cha kisiasa.
Tanzania ina mwelekeo mzuri chini ya uongozi wa rais Kikwete , ukizingatia, kwa mara ya kwanza, tunaona matangazo ya mali asili za Tanzania katika televisheni kama CNN , FOX, CBS etc. Kilichobaki ni kwamba sheria za Tanzania itabidi zibadilishwe ili Rais awe na uwezo wa kuteua mawaziri au viongozi ambao siyo wabunge kwa maana Tanzania ina watu wenye vipaji vya hali ya juu ambao siyo wabunge
Kadhalika, ingekuwa vyema ikiwa viongozi wote watalazimishwa kusaini mikataba ya utekelezaji kila baada ya mwaka mmoja.Yule atakayeshindwa itabidi aachie ngazi. Bila shaka kutakuwepo utekelezaji wa hali ya juu katika wizara na mashirika yote ya umma.


BC: Katika mahojiano yako uliyofanya na gazeti la Charlotte Observer ulionyesha kukerwa sana na chuki miongoni mwetu binadamu,vita na mateso mbalimbali yanayowakumba binadamu duniani kote. Ungeshauri nini kifanyike?


JM: Binadamu wa karne ya ishirini na moja amepiga hatua kubwa sana katika fani zote; Amefika mwezini, amegundua tiba dhidi ya maradhi mengi. Binadamu amerahishisha mawasiliano kwa kuifanya dunia ionekane kama kidude kidogo, lakini cha kusikitisha licha ya maendeleo makubwa tuliyoyapata,tumeshindwa kupendana.
Tunauana, tunachukiana kupita kiasi, wengine wanakufa kwa njaa ilhali wachache wamebeba utajiri wa dunia mikononi mwao, na hii ndo sababu kubwa hatuna amani.
Lengo langu kubwa au nia yangu kubwa ni Amani na upendo baina ya binadamu. Lengo langu kubwa ni kuleta matumaini kwa binadamu wenzangu bila ya kujali rangi wala mpaka. Sitapendelea kumtazama binadamu kutokana na kabila au tabaka lake. Rwanda, Sierra Leone, Sudan, Kenya etc. Ni mifano ambayo inaonyesha binadamu asivyo na hutu. Ni kwa nini tuuane, kwa nini watoto na wanawake wasiokuwa na hatia wachomwe moto wakiwa hai?
Huzuni, lakini kweli, ni kwamba amani ya aina hii haiwezi kudumu kwani anayeshindwa daima anakuwa na kinyongo cha kulipiza kisasi rohoni. Ila mbegu za upendo daima zitazaa amani. Kama binadamu mwingine, namuomba Mungu anipe nguvu na muda kidogo kuishi ili angalau niguse mioyo michache ambayo pia inaweza kuyasambaza hizi mbegu za upendo ili amani iwepo duniani.
Amani haiji kwa mtutu wa Bunduki au mapanga, amani haiji kwa mabomu. Amani inapatikana pale watu wanapokaa na kujadili namna ya kusuluhisha matatizo. Amani haipo binadamu anapokosa chakula, amani haipo pasipo tumaini, amani haipo pasipo haki. Ni lazima tuungane kwa pamoja ili tutafute ufumbuzi wa haya maswala.
Binadamu ndiye kiumbe pekee Mungu alimuumba kwa mkono wake akampa akili za kufanya maajabu, na kwa bahati mbaya ndiye kiumbe hatari kuliko wote. Suluhisho ni kuibadilisha mioyo sugu kwa kuitendea mema.


BC: Kila mwaka wewe hupenda kutembelea Tanzania na kutoa misaada mbalimbali kwenye vituo vya watoto yatima na pia kusaidia watu wengine wenye shida.Ni vituo gani mpaka hivi sasa ambavyo huwa unavipelekea msaada kule nyumbani?Je ungependa kutoa ujumbe gani kwa watanzania.


JM: Ni bahati mbaya kwamba kila ulifanyalo katika hii karne ni lazima itapatikana katika vyombo vya habari. Ningekuwa na uwezo ningejaribu namna ya kufanya haya mambo kimya kimya. Kwani nimeanza hizi shughuli mwaka 2000 nikiwa chuo kikuu.Lakini pale nilipoanza kushirikiana na watu, basi habari nyingi zikawa zinaenea kila kona.
Nakumbuka msaada wangu wa kwanza ilikuwa ni kwa watoto waathirika wa ukimwi mwaka 2000 huko Bukoba.Na huo msaada niliutoa kupitia kwa masista wa kikatoliki.
Nisingependa kutaja ni vitu gani au hela ngapi nimetoa, nimetembelea vituo vingi Dar es salaam. Kijijini, huko Musoma, mara nyingi nimewapelekea chakula na kusaidia katika matatizo mbalimbali, nimesaidia wajane, wazee na watu wasiojiweza lakini nisingependa kutaja vitu nilivyofanya.Nadhani jamii itanihukumu kwa kusaidia kwa malengo tofauti. Mimi ni mtumishi wao, chochote ninachokifanya, nakifanya kutokana na ukweli kwamba walijinyima na kunituma kutalii na kujifunza namna ya kuwakomboa. Kwa hiyo sioni sababu ya kuyazungumzia niliyoyafanya.


BC: Utawashauri vipi wengine wenye uwezo wa kufanya hivyo, kuhusu umuhimu wa kusaidia watoto yatima na masikini wengine nyumbani Tanzania?


JM: Kusaidia katika jamii siyo swala la utajiri. Mimi siyo tajiri na siwezi kuwa tajiri kutokana na majukumu niliyonayo.Sina lolote, nafanya kazi kama vijana wengine wa kitanzania wanaohangaika pale Kariakoo. Sina tofauti na vijana wengine wanaoishi kwa kubahatisha huko vijijini, ila najiona kama mwakilishi au mtumishi wao waliyemtuma kutafuta ufumbuzi wa matatizo yanayowakabili.Kinachohitajika ni kuwa na moyo wa kujituma bila kutegemea chochote kwa kutenda wema.


BC: Kuna msemo usemao kwamba "Nipe samaki na utakuwa umenilisha kwa leo.Nifundishe jinsi ya kuvua samaki na utakuwa umenilisha milele'. Sasa unapoangalia suala zima la kusaidiana na kutoa misaada hivi leo, unadhani ni juhudi gani zinaweza kufanyika,kwa upande wa serikali na watu binafsi na taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali katika kuhakikisha kwamba misaada inayotolewa inalenga zaidi katika kuwafundisha watu "kuvua samaki" na sio kuwalisha kwa siku moja tu?


JM: Ili binadamu azidi kuwa hai na mwenye afya bora na akili timamu ni lazima apate chakula, mavazi na sehemu ya kujisitiri. Lengo langu siyo kuja kila mara na kugawa chakula, nitakuwa sisaidii ila nawadanganya wana jamii. Ila, kila kitu kina mwanzo wake, na huu ndo mwanzo na haya mahitaji ni muhimu
Natafuta mbinu au suluhisho za kudumu. Panapo majaaliwa, nitatumia baraka alizonipa Mungu, angalau niweze kutafuta usaidizi wa kudumu kama vile kujenga zahanati, shule na pia kuanzisha mfuko maalum wa kuwawezesha vijana wachache wenye vipaji wasio na uwezo waweze kupata elimu.
Mungu anatupa nafasi kama hizi pamoja na uhai kwa sababu zake; nina imani kwamba mipango yake itakuwa dhahiri pale tutakapoleta mabadiliko katika maisha ya wengine. Na ikiwa vijana waliobahatika watajitolea kusaidia mmoja mmoja, nadhani dunia itakuwa tofauti.
Suala la watoto yatima nafikiri serikali ingelitafutia suluhisho la kudumu, kwani kuwaona wanaandamana kama ilivyotokea huko Temeke, mwanzoni mwa mwaka huu wakidai haki yao, ni swala la kuhuzunisha, hasa ukizingatia kwamba misaada wanayopewa inaishia katika mifuko ya watu wengine.
Ni laana kwa mtu wa kawaida kuwachukulia watoto wasiokuwa na namna kama kitega uchumi. Licha ya hayo, taifa kama Tanzania ambalo limejengwa katika misingi ya undugu isingekuwa na vituo vya watoto mayatima, kwani ndugu na marafiki wange wafungulia hawa watoto milango yao.


BC: Kuna hii habari kwamba kuna wakati uliwahi kuuza gari lako binafsi ili ukawasaidie watu waliokuwa wamekumbwa na njaa kutokana na ukame huko kijijini kwenu Tanzania. Unaweza kutuambia kidogo hii ilikuwaje? Nini kilitokea mpaka ukachukua uamuzi wa kishujaa namna hiyo?


JM: Sioni ushujaa au kitu cha ajabu kwa mtu kuuza gari yake, kwani hivi ni vitu vya kidunia ambavyo tunakufa na kuviacha. Sipendi kuzungumzia hili swala kwa sababu ni jukumu langu kusaidia. Gari halina manufaa yoyote kwangu ikiwa watu wangu wanakufa kwa njaa.
Kumbuka kwamba, chochote chaweza kutokea na hiyo gari kuniua, au kunifanya kilema nisiweze kuitumia tena. Lakini binadamu mwenzangu anaweza kutoka katika baa la njaa na kunisaidia au kuninunulia magari mengine kumi. Au weka picha ambapo umezungukwa na na masikini kila kona, kila unapotembea na hiyo gari yako unaowaona ni watu wenye njaa, je amani ipo kweli hapo?
Nitakuwa mtumwa wa kiitikadi na wa kifikra nikikumbuka kwamba nilimuacha mtoto akafa kwa njaa ilhali nilikuwa na uwezo wa kuokoa maisha yake. Mungu amenibariki na akili timamu ya na bidii ya kazi, kwa hiyo thamani ya gari nisingeweza kuilinganisha na uhai wa binadamu.

mashaka3bc.jpg


BC: Tumesikia kwamba hivi sasa uko mbioni kuanzisha taasisi yako binafsi ambayo itashughulikia masuala mbalimbali ya maendeleo nchini Tanzania katika mambo kama vile elimu, afya nk. Unaweza kutuambia kidogo mipango inakwendaje mpaka hivi sasa?


JM: Maswala kama haya yanachukua muda, na pia yanafanywa kwa uangalifu kutokana na sheria za nchi. Suala hilo lipo mikononi mwa wanasheria wanaonisaidia, ila kila kitu kikiwa tayari nadhani mtafahamu kwa maana nitaisajili Tanzania pia, ila isije kutokea uzushi kwamba napata misaada toka kwa watu, hapana kila kitu ninachotoa ni kujinyima kwangu mwenyewe.


BC: Je umeshaoa bwana Mashaka?


JM: Bado!


BC: Mwisho una ujumbe gani kwa watanzania? Na kwa wale ambao wangependa kuungana nawe au kushirikiana nawe katika jitihada hizi wanawezaje kufanya hivyo?


JM: Development in a country is not a political leader's responsibility; it is a common man's work. Greatest achievements in the history of the universe, have been made by common men. Farmers, carpenters, teachers, businessmen and many others, cornered without a way out of their problems, are the ones finding ways, which in turn makes life easier for all of us. Therefore, our poverty should not discourage us, but propel us to strive higher.

I am sure, our society has people, who can leave memorable deeds, if only we could utilize our skills, talents and social potitions positively . Politicians, controlling their lust, civil servants being honest in their dealings, and those in the private sector working diligently, our country can re-write another chapter in the world history.
Those that we envy especially the western world, prospered through passion, discipline and hard work

To my fellow young people, we are the future of Tanzania. We must not disappoint those who look up to us, by returning back to them with rotten cultures and behaviours. We have our own culture, which we should be proud of. We must sacrifice, and give our lives should the need be, in order to make the needed change.
Those privileged to have education, should share their knowledge with a broader society and not center their talents on themselves. The future of Tanzania, and peace for humanity lies in our hands, and this can be possible if only we could embrace each other not hate one another.

My harms and heart are open to anyone willing to join me in the effort to reduce suffering amongst our people, and I do believe, even though we can't change the world, we make a difference by making the world more liveable and a peaceful place.



 
kama kweli nilijua huyu panya atakuja na story kama hizi mwishoni,jamani naomba niulize hivi nyinyi wabongo hasa mliosoma nje hamuwezi kufanya kitu ingine zaidi ya kuwadanganya watu na hivyo visenti vyenu vya pipi kuwaibia?we john mashaka huna biashara nyingine ya kufanya na hizo vx zako 4 na dola 350,000 zaidi ya kununua ubunge?si lazima wote muwe wanasiasa,halafu chama chenyewe ccm unahitaji nini cha zaidi humo?si ufungue hata travel agency au jenga hotel basi kama hela zinakuwasha,e bwana mi sina mjadala mrefu watu washamba kama hawa anaona kukaa marekani basi we ndio mungu utafanya lolote unalotaka,kama muda wa kupiga box umeisha rudi home tu anzisha biashara ya matikiti maji na matango basi kama obama wa urusi.
Hiyo ndiyo Typical Bongo Style! Hizi ni tetesi tu, huyu jamaa anataka kufanya anayoyaona yeye, na mie naweza kusema kuwa, wasomi vijana, pamoja na wasomi wengine popote pale walipo wawe na changamoto ya kufanya mambo makubwa. Wawe msitali wa mbele vilevile, siyo kulaumu tu wazee au wale ambao hawajasoma ndiyo wanachukua madaraka. Let the boys and gals work their way up. The good thing is is not so easy to convince Tanzanians by your only money or VXs; will much depend on what your lips will evict. Note that Tanzania of today is not that of 1947.

Let everybody try their best then from these we can get the best to serve our nation!
 
[FONT=Tahoma, Verdana, sans-serif]Events Calendar[/FONT]
The John Mashaka Foundation is planning to help orphaned children in various hospitals in Tanzania who would not otherwise afford to pay for their treatment. It is also planning to sponsor special summer programs in 2009 which will enable poor (at risk) children in the United States (State of North Carolina) get a chance to earn various vacations.
The foundation will also be working in very remote regions of Tanzania on water projects.
As we count towards 2009, we count on your moral support to make these noble causes happen. Any donation is welcomed.
Checks / Money Order Donations can be mailed to
The John Mashaka Foundation Inc.
9506 Grove Crest Ln #623
Charlotte, NC 28262
All donations are Tax Deductible

Nimeikuta kwenye foundation yake hiyo, kwa kweli huyu kijana anajitahidi. Ila mie namshauri asijiingize kwenye siasa, yeye aendelee kusaidia jamii kama anavyofanya sasa.
 
[FONT=Tahoma, Verdana, sans-serif]Events Calendar[/FONT]
The John Mashaka Foundation is planning to help orphaned children in various hospitals in Tanzania who would not otherwise afford to pay for their treatment. It is also planning to sponsor special summer programs in 2009 which will enable poor (at risk) children in the United States (State of North Carolina) get a chance to earn various vacations.
The foundation will also be working in very remote regions of Tanzania on water projects.
As we count towards 2009, we count on your moral support to make these noble causes happen. Any donation is welcomed.
Checks / Money Order Donations can be mailed to
The John Mashaka Foundation Inc.
9506 Grove Crest Ln #623
Charlotte, NC 28262
All donations are Tax Deductible

Nimeikuta kwenye foundation yake hiyo, kwa kweli huyu kijana anajitahidi. Ila mie namshauri asijiingize kwenye siasa, yeye aendelee kusaidia jamii kama anavyofanya sasa.


Huyu kijana kusema kweli, amekuwa Cheche nchini Tanzania, anawafanya mafisadi wasiwe na amani kabisa. Speeches Zake ni kali mno
 
- Mkuu kila unapofungua kinywa unazidi kuonyesha uwezo wako wa kufikiri ulipoanzia na kuishia, kila siku unalia lia hapa kwamba Kyela unaibiwa na kuongozwa na mafisadi, hivi kweli unaweza kulinganisha maendeleo ya jimbo la Ukonga na Kyela?

- Mkuu jimbo la Ukonga lina kata nyingi zikiwemo za Kinyerezi, Kipunguni, Kitunda, Ukonga Magereza, Majumba Sita, Sitaki Shari, Segerea, Airwing na zinginezo, sasa hebu nitajie kata moja tu kati ya hizi unayoweza kulinganisha na hata jimbo zima la Kyela kimaendeleo?

- Ndio kwanza tumefungua bara bara mpya ya lami, kutoka getini Airwing yaani njia panda ya Airport mpaka gerezani Segerea kufikia Tabata unaunganisha mpaka Kimara. Mahanga sio siri ni kiongozi mchovu, lakini Ukonga sio Mahanga ambaye amekaa bungeni kwa miaka minne tu so far, hili jimbo ni bomba kabla hata yeye kuhamia Ukonga.

- Eti mkuu jimbo lenye vitega uchumi na kutoa ajira kwa wananchi jimboni kama Julius Nyerere International Airport, FFU HQ, JWTZ-Airwing HQ, JWTZ-Mizinga Squad, Gereza Kuu la Ukonga, Gereza Kuu la Segerea, Viwanda vya nguo Kiltex na Sungura tex, Kiwanda maalum cha kutotota vifaranga vya kuku, Segerea Catholic Seminary, unasema unaweza kulinganisha hili jimbo na Kyela? Hivi unajua hili jimbo lina secondary ngapi mkuu? Hebu nitajie jimbo moja tu Tanzania nzima linaloweza kulifikia jimbo hili la Ukonga kwa maendeleo?

- Na pia jimbo hili tunajivunia sana kwa kuwa na kata ninayotoka ya Kinyerezi/Sitakishari ambayo ni a home for national celebrities kama the sitting national leaders Waziri Wasirra, Mkuu wa Itifaki Balozi Itatiro, RC wa sasa Mbeya Mwakipesile, Mbunge wa Kawe Rita Mlaki, Managing Director Azania Bank Charles, Managing Director Wananchi Bank Mzee Mkwawa, pia tuna wastaafu wa taifa kama familia ya waziri wa zamani wa afya Mzee Sterling, Mzee Apiyo, familia ya marehemu Waziri Itatiro, familia ya marehemu makamu wa mwenyekiti wa kwanza wa Chadema Mzee Ngwilulupi, familia ya Balozi wetu wa zamani Nigeria Marehemu Mwasakafyuka, Wakuu watatu wa zamani wa Magereza Mzee Mwanguku, Mzee Mwaijande na Mzee Mwaipopo, familia ya mkuu wa polisi zamani marehemu Mzee Liani, Pia tuna wafanya biashara maarufu kama kina Mujuluzi, majority owner wa Imma, Dr. Mwaijande owner wa pharmacy maarufu pale Muhimbili hospital, kampuni kubwa ya mabasi na malori ya Mahende, Club maarufu sana Dar ya Hill-teck, pia ni a home for a former Simba player/national team Idd Pazi "Father" na pia ni a home for mimi mwenyewe Mukulu Field Marshall Es, yaani wazee wa sauti ya umeme! na Mkulu Mashaka John.


Respect.

Field Marshall Es!

Na wenu mtiifu....
 
[FONT=Tahoma, Verdana, sans-serif]Events Calendar[/FONT]


Nimeikuta kwenye foundation yake hiyo, kwa kweli huyu kijana anajitahidi. Ila mie namshauri asijiingize kwenye siasa, yeye aendelee kusaidia jamii kama anavyofanya sasa.

Wakuu mimi kila ninaposoma maandiko au mahojiano ya huyu mtu jinsi yanavyosisimua sitaki kuamini mapema kuwa anataka kujiingiza kwenye siasa. Tungoje tuone, 2010 sio mbali imebaki miezi michache sana. Kuna mahali humu ndani JF tumeanza kujilaumu kwamba tulimhukumu Mrema mapema mno. Tutajuaje kama haya anayoyafanya yana au hayana mlengo wa kisiasa?
Soon Time will tell.
 
I would like to see some new blood in the parliament.Of course watu wanaweza kusema jamaa anakuja na gia opportunistic and all which is true and I would rather see straight talk, lakini at least tunaweza kuona siasa zetu zinakuwa elevated to another level.

I know John Mashaka is corny as hell in many ways, but what is the alternative? I will take a John Mashaka from "Wall St. South" any day rather than a John Komba or Makongoro Mahanga.

It's time to elevate the game, and unless we have a change of regime/ leadership we are guaranteed to revolve in a vicious cycle of mediocrity.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom