Johnson Mashaka na mbio za Ubunge Ukonga

Hizi zote ni dirty politica maana huyu jamaa anaweza kuja na kuharibu kabisa haiba yake ya jamii maana huwezi kufanya mambo kama haya ndani ya CCM
 
Na msinisahau Mkandara nipo Matembele, Ukonga..

Mkandara,

Usijiangushe kaka yangu, na wewe unakaa huko kwa wachovu Ukonga?

Mizee yote hoi hoi ile ya huku kwetu Kyela inakaa hayo maeneo ukianzia akina Mwakipesile, Mwakalukwa mpaka yule aliyekuwa mkuu wa magerza.

Sikushangaa nilipoona Malafyale na ES nao ni mwendelezo huo huo wa hoi hoi wa Ukonga wakiongozwa na mbunge wao hoi Mahanga.

Nakushauri hama huko, usije ukaishia kama yule katibu mkuu wa rais hata jina nimesahau.

Watu wa UKONGA mko hoi sana, afadhali hata sisi wa huku Kyela.

Labda Mashaka awachangamshe kidogo.
 
- Mkuu Malafyale heshima mbele sana mkuu, kumbe mkuu na wewe ni jirani unajua mimi mkuu nipo chini yako hapo Kinyerezi mkuu ukivuka reli tu njia ya kwenda Segerea, saafi sana sasa lazima tuhamishie hii elimu tunayoipata hapa JF mpaka huku jimboni kwetu saafi sana na tupo pamoja.
- Kwa leo sina comments na hizi habari za Mashaka, lakini in due time nitasema, kwanza ni jimbo langu anyways, ngoja niwasiliane na wazee wa jimbo kwanza and then nitasema tena loud and very clear, when the time is right.

Respect.

FMEs!

Bahati nzuri kwa Dar yalipo makazi yangu ni Kipunguni-kitunda,na sijaona hata siku moja John Mashaka akishirikiana na sisi kweye suala la maendeleo;kwa ufupi kama kweli anakuja kugombea Ukonga na aje na "tutamnyoa" na hizo" hela zake!Kama suala ni mgombea kiana wapo wengi tu Ukonga na sio lzm awe John Mashaka ambaye umaarufu wake kwa wana Ukonga tunausikia tu kupitia blog ya Michuzi inayomtangaza kweli kweli!
Pia kama kweli ataleta Wamarekani kuja kumfanyia kampeni hapo atakuwa anavunja katiba,sheria mama za uchaguzi wa TZ zinakataza kabisa kwa mtu asiye raia wa tz kuhusika kwa lolote lile ktk uchaguzi wetu kama sisi ambavyo hatuingilii chaguzi za nchi zingine!

"Mwisho ni hii habari ya dola 350,000 na gari hizi zake za kifahari",Kwa maisha ya USA kujikusanya hadi kufikisha hela hizo na kununua magari hayo ni ngumu;anyway acha niamini kama anavyo vitu hivyo,lkn je vitamsadia kupata Ubunge wa Ukonga bila mtaji wa watu?

Kwa jinsi Mashaka anavyopenda kujitafutia umaarufu, nashangaa kwa nini hayo anayosemekana ameyafanya Ukonga hayajawekwa kule kwa Michuzi.

Akitumia hela za michango anayopewa huko USA kuja kufanyia kampeni za kisiasa atakuwa amekosea heshima hao walimchangia kwa kigezo cha kuja kuendeleza huduma za kijamii.

Mbunge wa sasa Dr Makongoro ni mkazi wa Ukonga, na zaidi ya hapo iwe ni kwa juhudi zake au "bahati" yake. Katika kipindi chake cha Ubunge Ukonga imebadilika sana. FMES na Malafyale mtakubaliana na mimi kuwa mwaka 2000 kulikuwa hakuna barabara ya lami Kinyerezi, Kipunguni, Vingunguti na pengine hata Tabata. Na nimesikia kuwa kuna mchakato wa kupanua barabara ya Ukonga ziwe barabara mbili. Kwa hakika mabadiliko haya yatampa kifua sana Dr Makongoro ikifika 2010. Hayo ndiyo niliyoyaona mimi, na kwa upeo wangu wa kuwafahamu wapiga kura Ukonga, itakuwa kazi kwa outsider kuja kumtoa Dr Makongoro iwapo ataamua kugombea.

Mkuu Malafyale,

Kijana Jerry Slaa "kwa maoni yangu" anahitaji muda zaidi wa kujifunza mamba, unajua ni kama alitoka Mlimani na kuingia kwenye siasa moja kwa moja. Bado sijaona juhudi na kazi yake zaidi ya vigogo kumkingia kifua kwenye kila kila chaguzi ndani ya CCM. I could be wrong but as always….

Time will tell.
 
Kama kweli anataka ku-invest hizo dola laki 3.5 lazima aseme kwanza atazirudisha vipi. Hatuwezi tukawa tunafanya kazi ya kuwapigia kelele wezi na kuwakaribisha majambazi, au tukubali kununuliwa na majambazi.
Katika hali ya kawaida mtu mwenye dola laki 3 na 4x4 nne hata jiingiza kwenye "mchezo mchafu", aanze kwanza kwa ku-invest hizo dola kwenye jimbo hilo then tuone kama anawasaidia wananchi, otherwise ni kwamba anataka kuwanunua wananchi ili ajichotee
Tawile!Nadhani sasa JF imeingiliwa na virusi,yaani tunapiga vita matumizi mabaya ya pesa huyu jamaa anakuja kusifia eti John Mashaka anamwaga mafedha jimboni akishirikiana na akina BUSH kuja kutawala ukonga,aibu!Huyo Wasiwasi(Mashaka)hana tofauti na RA na mkimfagilia mtaona mashaka yake.
Kila siku nasisitiza wengi wamesoma lakini hawakuelimika je mmewaona hao?
 
Hizi habari jinsi zilivyoletwa zimekaa kifitna fitna tu! hata kama zina ukweli ndani yake ila namna zilivyowasilishwa zinatia shaka
 
Ingawa sina uhakika na hicho chanzo: Kuna usemi mmoja wa Chadema unasema kuwa:

MABADILIKO YA KWELI HAYAWEZI KULETWA NA WATU WALE WALE WA CHAMA KILE KILE WAKIENDELEZA YALE YALE ETI KWA ARI, NGUVU NA KASI MPYA.

Nasikia mojawapo ya majimbo ambayo Chadema itayachukua 2010 hapa Dar es Salaam ni jimbo la Ukonga.

Waacheni wapunguze umasikini kwa wananchi wa Ukonga!!
 
Bahati nzuri kwa Dar yalipo makazi yangu ni Kipunguni-kitunda,na sijaona hata siku moja John Mashaka akishirikiana na sisi kweye suala la maendeleo;kwa ufupi kama kweli anakuja kugombea Ukonga na aje na "tutamnyoa" na hizo" hela zake!Kama suala ni mgombea kiana wapo wengi tu Ukonga na sio lzm awe John Mashaka ambaye umaarufu wake kwa wana Ukonga tunausikia tu kupitia blog ya Michuzi inayomtangaza kweli kweli!

Pia kama kweli ataleta Wamarekani kuja kumfanyia kampeni hapo atakuwa anavunja katiba,sheria mama za uchaguzi wa TZ zinakataza kabisa kwa mtu asiye raia wa tz kuhusika kwa lolote lile ktk uchaguzi wetu kama sisi ambavyo hatuingilii chaguzi za nchi zingine!

"Mwisho ni hii habari ya dola 350,000 na gari hizi zake za kifahari",Kwa maisha ya USA kujikusanya hadi kufikisha hela hizo na kununua magari hayo ni ngumu;anyway acha niamini kama anavyo vitu hivyo,lkn je vitamsadia kupata Ubunge wa Ukonga bila mtaji wa watu?
hivi ukonga mahanga ameleta maendeleoo ganii??

huyu mahanga ana skendooo kibaoo mpaka kesi ya utapeli ila gafla akazawadiwa uwaziri kisa mtandaoo..jamani ukonga hebu chambueni pumba na mchele kwa sasa hamna haja ya kuendeleaa kuwa na kiongozii kama huyuu..

john mashaka simjui zaidi ya kumsoma kwa blogu ila natumai ukonga mna watu makini zaidi ya hawa wa kwenye bloguuu..
 
ndani ya ccm hawezi kitu, wazee wameshika nchi, pole zake!!!
spika mwenyewe ameshindwa. Ubunge anaweza kupewa kwa njaa za watanzania, na tamaa ya vipesa na lifti za gari, ila atafanya kazi within limits ambazo atawekewa na wazee wenye nchi (CCM wenye nchi yao)
inasikitisha kuwa kama akipata kweli, baada ya miaka kadhaa, utamkuta akiwa na sera kama zilizopo sasa tu!
why kill himself?
ina maana ni mjinga hivyo?
au ametonywa na wazee ndani ya chama?
sasa kama kweli ni mpiganaji, wazee watakula wapi?
vitega uchumi vyote Dar vimekaa kiajabu ajabu, Dar haitawaliki kwa ajili yao.
 
Kwani kupata Ubunge huko Tz siku hizi ni lazima uhonge pesa nyingi kiasi hicho? Je atazirudishaje baada ya kupata? au ndo wale wakichaguliwa wanakua mafisadi? maana yake ubunge wake aliununua kwa fedha zake.
 
Wrong and very bad start:

i) Anatumia hela katika kujaribu kupata huo ubunge. Huo nao ni ufisadi na hadaa, maana anatumia umaskini na shida za wana Ukonga kujipatia ubunge. Mara baada ya uchaguzi atafanya kazi ya kutafuta namna ya kurudisha hizo sh 350,000m. Ameingia kwa gia ileile aliyoingia nayo Masha huko Nyamagana na tukamshangilia sana, tena hapahapa JF, lakini leo sote tunajua anachofanya Masha!

ii) Kupitia CCM. Sign of cowardness. Mapinduzi na mabadiliko ya kweli hayawezi kuletwa kupitia CCM. Atakachofanikiwa sana sana ni kujifunza kutetea ufisadi.

Anyway kama anataka uwaziri huko CCM ndiko kunakomfaa. Lakini kama kweli ana nia ya kushiriki kuleta mabadiliko aende upinzani, aache longolongo na woga.
 
Wengi watakuja na kujisafanya wanatetea wanyonge, wanapigana na mafisadi wanauchungu na nchi. Hizi nazo zitakuwa ni ishara za mafisadi watatumia shida na umasikini wa wananchi kujinufaisha na kuwaibia. Yeyote anayetaka uongozi kwa kutumia fedha tena nyingi huyo ni mwizi na ni fisadi. Yeyote anayetaka kuuwa watu kwa ajili ya uongozi huyo ni wa kuogopa kama ukoma.

Mtanzania wa kweli na mzalendo wa kweli atatumia rasilimali zake nyingi kuelimisha wapiga kura wake nini maana ya kura yao, na kwa nini achaguliwe kiongozi mwadilifu. na atakuwa wazi kuwaeleza wananchi wake sifa za kiongozi mwadilifu. Wakati ule wa wizi Daniel Yona alikuwa anatumia vifurushi vya fedha kushinda kule same, waulizeni watu wa same baada ya kupewa hizo fedha kutoka kwa yona walipata nini??? kwa muda wa ubunge wa mheshimiwa-0.

Kununua uongozi ni ufisadi, dhuluma, uhujumu, usaliti, uzandiki, wizi na kuwakosea wananchi kwa hali ya juu. Kiongozi wa namna hii hutafuta manufaa yake mwenyewe na mwishowe huuza nchi kama Masha, Ngeleja, Chenge, Kikwete, Mkapa, Nk.
 
Wrong and very bad start:

i) Anatumia hela katika kujaribu kupata huo ubunge. Huo nao ni ufisadi na hadaa, maana anatumia umaskini na shida za wana Ukonga kujipatia ubunge. Mara baada ya uchaguzi atafanya kazi ya kutafuta namna ya kurudisha hizo sh 350,000m. Ameingia kwa gia ileile aliyoingia nayo Masha huko Nyamagana na tukamshangilia sana, tena hapahapa JF, lakini leo sote tunajua anachofanya Masha!

ii) Kupitia CCM. Sign of cowardness. Mapinduzi na mabadiliko ya kweli hayawezi kuletwa kupitia CCM. Atakachofanikiwa sana sana ni kujifunza kutetea ufisadi.

Anyway kama anataka uwaziri huko CCM ndiko kunakomfaa. Lakini kama kweli ana nia ya kushiriki kuleta mabadiliko aende upinzani, aache longolongo na woga.

Wrong and bad assumption:

1. Ku conclude kuwa madai udaku kuwa ni kweli na kutolea uamuzi

2. Kwamba kugombea kupitia CCM ni sign of cowardness, upinzani gani unao uongelea hapa? wale walio mzuia Zitto kugombea?
 
FISADI-ORIGINAL

Unamchezea "rafu" John Mashaka!

Ukisoma vizuri Hii habari ulivyoilete na wachangiaji inaonyesha dhairi kuwa wewe na Makongoro Mahanga ni kitu kimoja na inaonekana mme-"smell rat" na hivyo mnaaza kumchafua John Mashaka kabla hata hajaonyesha nia ya kugombania ubunge "jimbo lenu la ukonga"

John Mashaka simfahamu na indeed I would not care kumfahamu ila suala la msingi ni kwamba hizi siasa za kuchafuana will lead us to nowhere!

Gossip,
Gossip,
Gossip,
Gossip,
Gossip,
Gossip,
 
Ni ukweli usiopingika kijana mwenye ari na moyo wa kweli wa kumsadia mtanzania hawezi kugombea kwa tiketi ya CCM kwa sasa. Huu ni woga, na kutojiamini, ila wengi wanasukumwa na njaa na kutumia siasa kama chanzo cha ajira pamoja na sababu nyingi zenye mbwembwe wanazotumia, sio wabunifu na hawana uwezo zaidi wa kujisaidia wenyewe wala watu wao. Wachovu.
 
Wrong and very bad start:

i) Anatumia hela katika kujaribu kupata huo ubunge. Huo nao ni ufisadi na hadaa, maana anatumia umaskini na shida za wana Ukonga kujipatia ubunge. Mara baada ya uchaguzi atafanya kazi ya kutafuta namna ya kurudisha hizo sh 350,000m. Ameingia kwa gia ileile aliyoingia nayo Masha huko Nyamagana na tukamshangilia sana, tena hapahapa JF, lakini leo sote tunajua anachofanya Masha!

ii) Kupitia CCM. Sign of cowardness. Mapinduzi na mabadiliko ya kweli hayawezi kuletwa kupitia CCM. Atakachofanikiwa sana sana ni kujifunza kutetea ufisadi.

Anyway kama anataka uwaziri huko CCM ndiko kunakomfaa. Lakini kama kweli ana nia ya kushiriki kuleta mabadiliko aende upinzani, aache longolongo na woga.

Yaani Kitila na wewe umechotwa mzobemzobe na hii story.. Milioni 350 kwa ajili ya magari tu Mashaka anatoa wapi ? mwenyewe anajikongoja na kuomba huko na huko ili aweze toa misaada anayotoa.Mimi nasema hata kama kuna ukweli juu ya hii habari lakini imeletwa kinamna ya kumtengenezea Mashaka mazingira ya Kifisadi
 
well, kama hilo ulilolisema ni la kweli nadhani ni jambo la kheri, huyo mbunge "the said mahanga" amefanya nini ukonga? ama ni barabara anayopalaza mwezi huu hiyo? we need changes jamani
 
Back
Top Bottom