John Pombe Magufuli unatuchefua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

John Pombe Magufuli unatuchefua

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Raia Fulani, Dec 18, 2011.

 1. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #1
  Dec 18, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Mwanzoni tulijua kuwa wewe ni mtu makini kume tumekosea. Nadhani hata wanaokutumikisha wanajua kuwa wewe si makini na ndio maana wanakuwekea spidi gavana na kukuambia uache ubabe. Mwanzoni nilidhani wamekuonea kumbe walikuwa sahihi. Upo kama roboti. Nimegundua hili kutokana na matamshi na kauli zako. Barabara zote nchini unazijua wewe. Vifungu vyote vya sheria umevikariri wewe. Hizo sheria ni kwa ajili ya binadamu lakini wao/sisi sio programmed kama wewe.

  Juzi hapa mkizindua barabara pale Dodoma, Pinda alikupiga dongo kuwa Rais alikupeleka uvuvi, na kule unajua idadi ya samaki nchini. Rais akaona bora akurudishe ujenzi. Tatizo lako mkuu unamtumikia kafiri kupitiliza, hadi unampa kero.

  Wewe ni mchapakazi sawa, lakini yawezekana huna maadili ya kazi. Hakuna mtanzania anayekuwazia urais. Wanakuwazia uwaziri tu kwa kuwa watanzania wanajua unajua kutumika.

  Achana kabisa na siasa zako za maji taka. Sio kila unapotoa neno hadharani usifie chama chako na kuponda upinzani. Kwa taarifa yako, unaowahutubia ni wapinzani. Sasa unapoponda viongozi wao na harakati za upinzani, wanakuchukia kweli. Wanakuoanisha na majina yako.

  Tatizo lako mkuu unatupa mawe hovyo kiasi cha kuwatwanga na wazazi wako pia. Nakufananisha na Abunuwasi kukata tawi ulilokalia. Hilo tawi ni wananchi. Mpita njia akikuambia kuwa unafanya kosa kwani utaanguka, unamkejeli. Utakapoanguka utamkimbilia aliyekuambia ukweli kumwomba utabiri zaidi, angalia asijekwambia utakufa lini.

  Achana na upinzani kwani ni jeshi kubwa kwa sasa. Una kashfa nyingi tu tunazozifahamu na nyingine zitafahamika. Una kashfa ya kuuza nyumba za serikali. Una kashfa za kumpa kimada wako nyumba ya serikali. Una kashfa ya kunyanyasa staff wako kwa kuletewa majungu na wapambe wako. Una kashfa ya ubabe, n.k, n.k. Fanya kazi, kiongozi kwani huijui kesho. Kazi ya kubwabwaja mwachue nape. Kaajiriwa kwa kazi hiyo. We kazi yako miundombinu. Usiwe kama mzazi anayewapa wanae mahitaji kwa masimango. Wenzako umeshwasikia wanabwabwaja hovyo? Time will tell
   
 2. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #2
  Dec 18, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Very interesting coment,
   
 3. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #3
  Dec 18, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Word...!
   
 4. j

  johnmashilatu JF-Expert Member

  #4
  Dec 18, 2011
  Joined: Sep 16, 2010
  Messages: 538
  Likes Received: 265
  Trophy Points: 80
  kuna hilo pia limejitokeza Alhamisi wiki hii katka mji wa Chato kwenye jimbo la Dr Magufuli ambapo wananchi waligoma kuhudhuria mkutano wake wa hadhara na mbunge huyo aliondokakwa ghadhabu licha ya mkuu wa wilaya hiyo Bi Hadija Nyembo kumowmba avute subira. Je ni Nabii kwmaba huw ahatambuliki kwao?
   
 5. I

  Imurumunyungu Senior Member

  #5
  Dec 18, 2011
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 108
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu jamaa watu wameshamchoka hata yeye analijua hilo ndo maana analopoka ovyo.Kwanza alishawahi kumuuzia nyumba ya serikali mdogo wake aliyekuwa mwanafunzi wa chuo kikuu kwa wakati huo.Huyo ni fisadi wa first class mwacheni alopoke maana hasomi alama za nyakati.Mawazo yake bado yako kwenye miaka ya 1990.
   
 6. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #6
  Dec 18, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Labda alikua na b0o0m
   
 7. Ng`wanakidiku

  Ng`wanakidiku JF-Expert Member

  #7
  Dec 18, 2011
  Joined: Apr 18, 2009
  Messages: 1,196
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nina uhakika na uthibitisho kwenye kura za maoni alishindwa ila kilichofanyika
  1. Alihonga kila mpiga kura 1500 au zaidi
  2. Akaiba kura kwa nguvu
  Kwa hiyo magufuli chato hakubaliki kama unavyodhania.
  Aliyeshinda kura za maoni 2010 na anayekubalika ni bwana mmoja anaitwa Dr Benedicto Lukanima!
   
 8. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #8
  Dec 18, 2011
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,148
  Likes Received: 10,500
  Trophy Points: 280
  poor magufuli. hujui ulitendalo masikini weee.
   
 9. M

  Mafie PM JF-Expert Member

  #9
  Dec 18, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 1,318
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Huyu jamaa nilikuwa nampenda sana na kumuamini lakini nimekuja kugundua sii lolote tena, pale tu aliposema ccm ni chama cha Mungu kila mwenye hekima alitakiwa aachane naye kabisa. Simpendi tena
   
 10. Mbugi

  Mbugi JF-Expert Member

  #10
  Dec 18, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,488
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 160
  "Kama ni Wakusikia kasikia" Kwani kwa sasa unawakera waajiri wako, kwa kauli zako tata, kama kuwavunjia nyumba wananchi kwa madai ya kusimamia sheria pasipo fidia kwa madai watu walizikuta barabara na ungali ukijua siku zote kwa nchi kama zetu Unplanned barabara ndizo hufuata watu walipo.

  Chukua mfano mdogo tu wa viwanja vyetu hivi vinavyopimwa kwa sasa halmashauri zetu hugawa viwanja kwanza na baadaye kujenga barabara.

  pili sheria unayoendelea mara kadhaa ni ile kwa mfano ya upana wa barabara yaani kabla ya mwaka 2008 inatamka juu ya 22.5 meters na baada ya hapo 30 meter leo unachora nyumba za watu hovyo hovyo, bila kujali economically unawapalalaizi. huu si uungwana, kwani sheria kwa upande wako uniona inafanya kazi wananchi wanapolalamika.
   
 11. kawakama

  kawakama JF-Expert Member

  #11
  Dec 18, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,303
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Acheni ushabiki wa kijinga huo,mtu akiponda chadema tu mnamchukia na kumuundia zengwe....mbona ninyi huwa mnaponda magamba lakini hakuna mtu anayewaona kama ni hopeless
   
 12. m

  mpigilie JF-Expert Member

  #12
  Dec 18, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 306
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kabla ya 2015 tutayasikia mengi...  Sichangii mada.
   
 13. jamii01

  jamii01 JF-Expert Member

  #13
  Dec 18, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,836
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Hakuna mtu asiyekuwa na mapungu kama mwanadamu..huyu jamaa katika mawaziri wanaofanya kazi zinaonekana huyu ni number one..tuache habari za CCM na CDM,Tanzania bila nguvu ile nchi aiendi hata kidogo..

  hasa upande wa miundombinu sababu kila kona kumeoza hakufai. Natamani kuona barabara za bongo ziko kama za Tokyo
  Mpeni Hongera zake pale anapostaili na ushauri pale anapokosea.
   
 14. A

  ACHEBE JF-Expert Member

  #14
  Dec 18, 2011
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 348
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Magufuli the Great songa mbele usivisikilize hivi visisimizi! Vimekereka kwa sababu umeviponda endelea kuvipa live, vinataka kusifiwa tu bila kukosolewa. Usirudi nyuma tupo wengi sana tunaokuunga mkono. Vibaraka wa chache tena with no adress ndo vinaleta maneno ya maliwatoni. Wachambishe hao wataisoma namba.
   
 15. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #15
  Dec 18, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Ni kweli anachapa kazi lakini naye amezidi kuropoka na kupenda misifa.
   
 16. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #16
  Dec 18, 2011
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  hatukatai kuwa magufuli hafanyi kazi. Tatizo lake ni kuingiza ushabiki wa kisiasa kila linapokuja suala la maendeleo. Aache kauli za hovyo hovyo la sivyo tutaendelea kumuona hovyo
   
 17. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #17
  Dec 18, 2011
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,167
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  huyu mzee wa data anataka kujichafua mwenyewe atanuka shombo sasa hivi la magamba
   
 18. Mtu Mzima

  Mtu Mzima JF-Expert Member

  #18
  Dec 18, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 381
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Umeshachangia...
   
 19. Timtim

  Timtim JF-Expert Member

  #19
  Dec 18, 2011
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 603
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Misifa tu hana busara kabisa.
   
 20. LE GAGNANT

  LE GAGNANT JF-Expert Member

  #20
  Dec 18, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 1,247
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Ukishakuwa ndani ya magamba tu busara yote inayeyuka.

  Yuko wapi sitta?
   
Loading...