TANZIA John Mwankenja auawa kwa risasi

Poleni sana Hilda Ngoye na Mwandosya kwa mtihani huu mgumu kwani huyu bwana aliwafaa sana; bwana alitoa na bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.
 
Let's hope kwamba mauajo haya hayahusiani na mambo ya kisiasa. Kama ni hivyo siasa zetu zinaelekea pabaya. Ni muhimu zaidi vyombo husika vipeleleze na hatimae kuwatia nguvuni waliotekeleza mauaji haya na haki itendeke.Mungu awatie nguvu wafiwa katika wakati huu ngumu na ailaze peponi roho ya marehemu. AMIN.
 
May Almighty God Rest his soul in Peace,Amen. Tusubiri uchunguzi tusianze kuweka hisia za kisiasa otherwise tunajipeleka siko
 
Kuna ***** mmoja atatoa tamko kua CHADEMA ndo wana husika,..
ngoja tu akune makalio saivi,akiamka mjue ndo alikua anawaza hivo!
 
Wakati CHADEMA wanabadilisha rangi za bendera yao na kuweka rangi nyekundu ndani ya bendera mpya, watu wengi tulikuwa hatujawaelewa .

Ila hivi sasa kwa yanayo jidhihirisha ni wazi kabisa maana ya rangi hiyo inaonekana wazi. Kwani matukio ya hivi karibuni ya kutaka kumuua Mh. Mbunge wa Tarime kwa kumpiga mawe , na jana kumpiga risasi Mwenyekiti wa halmashauri ya Rungwe, yaonekana kabisa kuna mkono wa CHADEMA na kuna kikosi maalum cha mauaji kimeundwa kwa ajili ya kutekeleza yale yaliyomo kwenye bendera yao ya alama nyekundu ambayo ni mauaji na umwagaji damu

Kama wote tutafikiri kama wewe na bila kuchukua hatua stahiki, tutakwisha. Hufanani na jina lako.
 
poleni sana wafiwa. bottom line tunaishi kwenye nchi hatari sana. kila ukiamka au niseme uingiapo nyumbani kwako salama unamshukuru Mungu. manake jinsi unavyoweza kupigwa risasi na 'watu wasiojulikana' Bongo sasa hivi uhai ni very cheap!
 
Pole sana wafiwa wote na mungu ailaze mahali pema roho ya marehemu. Nafikiri ni mapema sana kuhusisha mauaji hayo na masuala ya kisiasa. Tusubiri uchunguzi wa polisi kwanza.

Mbeya haijafika hapo na Rungwe ni katika wilaya zenye utulivu mkubwa kisiasa hata kama mapambano ya hoja yapo kama kawaida mitaani.

Kiwira ni kwa profesa Mwakyusa ila mwenyekiti alikuwa wa majimbo yote mawili yaani la prof. Mwakyusa pamoja na prof. Mwandosya.

hivi hawa polisi wetu kuna uchunguzi gani wa maana ambao walishawahi kufanya,.chacha wangwe wametupa jibu?kazi zao zote zimeshakuwa za kisiasa,kutumwa na ccm tu ndicho wanachojua,kwa ufupi siwaamini polisi wetu hata kidogo,..wapo kisiasa na uwezo wao huwa naudobt sana...
 
Pole sana wafiwa,Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.Alikuwa mwenyekiti wa halmashauri au wa CCM Rungwe?
 
Wakati CHADEMA wanabadilisha rangi za bendera yao na kuweka rangi nyekundu ndani ya bendera mpya, watu wengi tulikuwa hatujawaelewa .

Ila hivi sasa kwa yanayo jidhihirisha ni wazi kabisa maana ya rangi hiyo inaonekana wazi. Kwani matukio ya hivi karibuni ya kutaka kumuua Mh. Mbunge wa Tarime kwa kumpiga mawe , na jana kumpiga risasi Mwenyekiti wa halmashauri ya Rungwe, yaonekana kabisa kuna mkono wa CHADEMA na kuna kikosi maalum cha mauaji kimeundwa kwa ajili ya kutekeleza yale yaliyomo kwenye bendera yao ya alama nyekundu ambayo ni mauaji na umwagaji damu
Nafikiri hata mauaji ya Kolimba zilikuwa njama za Chadema teh teh teh akili mgando kweli kweli.
 
Nafikiri hata mauaji ya Kolimba zilikuwa njama za Chadema teh teh teh akili mgando kweli kweli.

Ya Kolimba yalikuwa mauaji? Watendeeni haki waliofariki. Vinginevyo hata akina Chacha Wangwe, Mwalimu, yoote tutaita ni mauaji.
 
RIP Mwankenja!
Everybody has his Day!
Hao waliomuua wataishi siku ngapi zaidi yake???
 
Back
Top Bottom