Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, Mbeya Ndugu John Mwankenja ameuwawa kikatili na watu wasiojulikana jana usiku.
Ndg John Mwankenja aliuwawa nyumbani kwake kwa kupigwa risasi wakati anaegesha gari lake, alikuwa amerejea tu kutoka Mbeya Mjini alikokuwa ameenda kumwona mke wake aliyelazwa hospitali ya Rufaa Mbeya.
Wauwaji hawajachukua kitu.
Ndugu J Mwankenja alikuwa vile vile Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya.
Mungu amuweke pema roho ya marehemu . AMEN