John Mnyika, kuulalia mkeka uliochanika kunahitaji akili nyingi sana na sio nguvu

Gaidi ni wazazi wako
Wewe ni
images.jpg
 
Comred mnyika mdogo wangu na katibu mkuu wa chama kikuu Cha upinzani chadema.tunataka tuuone utashi ya hekima na busara zako katika kipindi hiki kigumu,chama chako kina Kariba kubwa ya vijana ambao bado wana mihemko.mkeka uliolalia umechanika Sana .usitumie nguvu kubwa utauchana zaidi.maneno yako yawe na busara ya kiuongozi tunachotaka mbowe aachiwe hayo mengine tunayoyasikia kwa vijana wenu mtayafanya akiisha achiwa .isingekuwa maneno yenu ambayo nasema yametokana na mihemko ya vijana wenu huenda krismass hii mbowe tungekuwa nae.ukiwa na njaa usichague mkono utakaokulisha kula ili ushibe mengine yatafuata.kumshambulia zitto na rais kumerudisha nyuma mchakato wa kumtoa mbowe hata mamlaka zinaweza kuhisi mnakiburi, mjumbe hauwawi,,,
Hivi Wasomi Kina Mabere, n.k Wako Wapi.....! Kichwa Kile Cha Mnyika Hikma Hamna Mule.
Mwenye kili Shaka
 
Vijana wanaopiga kelele kuwa Mbowe asisamehewe ni wale wanaoshinda wanachangisha michango kwenye mitandao ya kijamii, kwa Wanachama na Wadau mbali mbali.
Shida Mbowe akitoka watapata wapi tena hela za kupiga? Biashara itakuwa imeisha.
Mbowe anatakiwa atoke hayo mengine wakapambane baadaye, Mnyika ashazidiwa na akina Tundu, Lema ambao nao wananufaika na biashara hii. Huu ni muda muafaka familia ya Mbowe kusimama kidete kuhakikisha mpendwa wao anatoka waache kusikiliza makelele ya wasaka tonge ambao sasa wanaenda kula keki mahakamani eti Mshikamano...NONSENSE...
Sugu aliwahi toka kwa msamaha wa Raisi, baadaye akafuata taratibu mahakama imsafishe..
Familia ya Mbowe hakikisheni mpendwa wenu anatoka kwa njia yeyote, only that ni muhimu kwa sasa hayo mengine baadaye.
Familia kumbukeni akina Lisu wanachokitakaa kesi ifike mwisho mnaweza kuja juta, kama mnajua kuna udhalimu je wakifika mwisho wakamfunga? Mtakuwa mmefaidika nini? Angalieni trend ya kesi inavyoenda, ni muhimu Familia mhakikishe kuwa mnasimama kidete mpendwa wenu anatoka, msimamo wenu kama familia ni muhimu sana kwa sasa, kumbukeni Mbowe ni kiongozi wa Chadema anazungukwa na watu wema, wanafiki, wanaokitaka cheo chake, wanaotaka kunufaika na kesi hii na wengine wengi sio kila ushauri mnaukubali..
 
Sio kila aombae msamaha amekosa...wakati mwingine msamaha uombwa kuepusha dhahma...kinachoendelea mahakamani kimetosha kuthibitisha madai ya Chadema kuwa ni kesi ya mchongo....itoshe sasa mkubali tu mwenyekiti atoke hata kama ni kwa huo msamaha maana imeisha onekana kuwa ni michongo.....Familia ya Mbowe isikubali mzee wao achaguliwe njia ya kupita na waliovaa viatu wakati yeye yuko peku..wenzie hawajui njia yenye miiba!
 
Back
Top Bottom