CHADEMA wanatengeneza vijana Watukutu na shupavu wenye akili nyingi sana

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,966
Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kwa taifa linahitaji vijana jasiri na watukutu wasiponda kujikomba komba na kujipendekeza, wasikua watu wa "ndio bwanamkubwa. Hili naliona kwa vijana wa CHADEMA, CCM inatengeneza na kulea vijana wengi sana lakini hawajatokea wa kuwafikia hata kijana mmoja wa CHADEMA.

1.TUNDU LISSU
Huyu aliwahi kukamatwa na jeshi la polisi na kuswekwa ndani kwa madai ya makosa ya uchochezi, alipotoka ndani hakuogopa akayarudia tena maneno hayo ya uchochezi akakamatwa tena. Huyu jamaa mpaka anapatwa na madhila ya kushambuliwa na risasi na wasiojulikana hakuwahi kutengua kauli zake na wala hajawahi kujipendekeza kwa mtu.

2.JOHN HECHE
Mmh! Huyu aliwahi kuongea na mmkuu wa nyumba akiwa ameweka mikono mfukoni mpaka akamwomba amheshimu kama mzazi wake.Kwa kijana wa kawaida hawezi kua na ujasiri huo ingawa kimaadili haukua mzuri.
3.HALIMA MDEE
Huyu mwanadada alitoka hadharani na kupingana na nkauli za mkuu na baadae akakazia maneno yake, baada ya hapo akakamatwa na kutiwa ndani, ni mwanamama asiyejipendekeza wala kumuogopa mtu.

5.JOHN MNYIKA
Huyu siku ya jana bila kumung'unya maneno wala kujikomba au kujipendekeza mbele ya mkuu, yeye emesema wazi wazi uso kwa uso na mkuu yaliyo rohoni mwake,chama chake na watanzania wengine wa kawaida ambao hawawezi kusimama na kuyasema mbele ya mkuu.

Ni vijana watutukutu, jasiri,wana akili nyingi, wadadisi wa mambo,watafiti wa mambo, hawapelekeshwi na wala hawajipendekezi kwa mtu.

Pamoja na ugumu wa siasa za upinzani nchini kwa sasa, lakini naona kabisa bado chama chao kina maisha marefu sana na huenda ndio mbadala wa CCM kwa baadae maana hakuna kijana yeyeote kutoka huko akasimama na kuzungumza kama hawa wa upinzani.

Hongera zana Mh Mbowe, unawajengea na kuwanoa vijana volivyo. Wamenoleka wakaiva,chama chako pekee ndio chenye vijana wa aina hii aliowasema mwl Nyerere.
 
Huyo Mwalimu Nyerere alikuwa hapendi kukosolewa Yeye Kila anachofanya anasifiwa tu! Na ndio Msemo wa 'zidumu fikra Za Mwenyekiti' ulizaliwa kuhakikisha Falsafa ya 'yes Sir' inadumishwa!
Usidanganye watu hapa, hayo maneno ya "zidumu fikra za mwenyekiti na ndio bwanamkubwa" aliyaasisi yeye mwenye kwa kuwaasa vijana kuacha uoga na kujipendekeza.
 
Ni vijana watutukutu, jasiri,wana akili nyingi, wadadisi wa mambo,watafiti wa mambo, hawapelekeshwi na wala hawajipendekezi kwa mtu.

Katika sifa zote, hii ndio sifa kuu kwa kiongozi yeyote. Kutopelekeshwa na kujipendekeza.

Chukulia kwa mfano, Mwalimu Nyerere aliyeliamini jambo na kulisemea bila ya kufumbafumba kwa kumwogopa yeyote, hata wale mabeberu.
Sema au simamia unachokiamini, sio kukificha na kulalamikia pembeni
 
Huyo Mwalimu Nyerere alikuwa hapendi kukosolewa Yeye Kila anachofanya anasifiwa tu! Na ndio Msemo wa 'zidumu fikra Za Mwenyekiti' ulizaliwa kuhakikisha Falsafa ya 'yes Sir' inadumishwa!
Si ndio nyinyi mliokuwa mnajikomba kwake ndio mlianzisha msemo huo; kwani aliwalazimisha mseme hivyo? Huoni hata aibu ya kumtwika lawama isiyomhusu?
 
Tuache utani Nyerere alikuwa dikteta na ndiye aliyetengeneza katiba ya kidikteta. Usingeweza kusimama kwenye mkutano wa Nyerere ukapinga sera zake mfu za ujamaa na kujitegemea, ungeweza kufungiwa kijijini hakuna kutoka mpaka kwa ruhusa ya serikali ya kijiji
 
Si ndio nyinyi mliokuwa mnajikomba kwake ndio mlianzisha msemo huo; kwani aliwalazimisha mseme hivyo? Huoni hata aibu ya kumtwika lawama isiyomhusu?

Kwa hiyo Na sisi ndio tulianzisha wazo la kufuta Vyama vingi
Ni sisi ndio tulianzisha Sheria kandamizi ya uhuru wa Habari 1976

Nyerere Ana sifa kadhaa nzuri lakin kumsifia Kwa Demokrasia Na uhuru wa Mawazo Na kukosoa Ni unafiki Kwa Kuwa Nyerere hakuwa anapenda Demokrasia wala kukosolewa

Tulimwita 'Bwana Haambiliki' Kwa tabia yake ya kujiona Yeye ndio Tanzania Na Tanzania ndio Yeye Na Kila anachofanya Ni sahihi
 
Taifa hili lingekuwa na viongozi wa fikra pana hakika vijana wenye sifa hizo wangewatumia kuijenga nchi hii
 
Sasa mnyika ndio.mtetezi wa wanyonge...sio hao watetezi feki wa ccm...ccm.wanamtetea mnyonge against nani?
 
Vijana wa upinzani wengi vichwani wako vizuri sana, shida ya wana Lumumba ni ukiraza, serious yaani unamkuta kijana wa Lumumba anaweza kuwa katibu au mwenyekiti wa ccm wa kata ukimuuliza hivi katibu mkuu wa ccm taifa anaitwa nani? unajibiwa anaitwa nape nauye, sasa haya c n maajabu?
 
Huyo Mwalimu Nyerere alikuwa hapendi kukosolewa Yeye Kila anachofanya anasifiwa tu! Na ndio Msemo wa 'zidumu fikra Za Mwenyekiti' ulizaliwa kuhakikisha Falsafa ya 'yes Sir' inadumishwa!
Uwe unawasikiliza kinawa Warioba waliofanya kazi na mwalimu, wanasema walikuwa wabagomea hadi teuzi zake na anazitengua bila kuwafukuza kazi!
 
Tuache utani Nyerere alikuwa dikteta na ndiye aliyetengeneza katiba ya kidikteta. Usingeweza kusimama kwenye mkutano wa Nyerere ukapinga sera zake mfu za ujamaa na kujitegemea, ungeweza kufungiwa kijijini hakuna kutoka mpaka kwa ruhusa ya serikali ya kijiji
Uongo mwingine wa Ibilisi huu!!

Tupo tuliokwa hai wakati wa utawala wa Nyerere! Acheni kuendekeza stori za kwenye vijiwe vya kahawa!
 
Back
Top Bottom