Joseph Yona: 06/01/2014 nilitekwa na CHADEMA kwa maagizo ya Mbowe na Mnyika

Trump2

JF-Expert Member
May 28, 2017
1,553
2,608
Hakika siku ya leo tarehe 29/03/2018,Mimi Joseph Yona mtanzania maskini na familia yangu ya PAVEA niliyetekwa na chadema tarehe 06/01/2014 katika ardhi yangu ya Tanzania na kuharibiwa direction ya maisha nina furaha furaha sana.

Furaha yangu inatokana na watu waliotoa maagizo ya kutekwa kwangu Mbowe na Mnyika(huyu kila mtu ajue alikuwa jirani yangu kwa maana ya kwangu na kwake/kwao temeke ilikuwa ni umbali wa mita 600 tu).

Pia watanzania mjue Mnyika Kwake/kwao na nilipokuwa naishi ni kata mbili jirani azimio na Mtoni.

Watanzania wenzangu najua mtaniuliza kwanini furaha yangu iko kwa Mbowe na Mnyika na si Peter Msigwa,Vicent Mashinji na Mwalimu wangu Mpendwa Ester Matiko.

Mbowe na Mnyika walikuwa wanajidai wanajua kila kitu na ndo chanzo cha kuvuruga chadema, Nitaeleza.

Mbowe na Mnyika waliwatuma Medi, Sabula kutoka kurugenzi ya ulinzi na usalama makao makuu chadema kufunga ofisi yangu ya wilaya wakiwa na gari ya Halima Mdee(Toyota Hillux) Nyeusi na kuagizwa nitekwe nipigwe niuawe kwa kukisaliti chama,eti nimemuunga mkono Zitto Zuberi Kabwe Chaaa!!.

Mbowe na Mnyika walifanikiwa kuniteka na kunipiga na kumuagiza mwanasheria wao ahakikishe nafukuzwa kazi Chuo cha DUCE na kweli nikiwa naumwa nilipata barua ya kufukuzwa bila kusikilizwa.

Mkuu wangu wa chuo kwa sasa ni Mkurugenzi wa PUMA alinifukuza kama Kuku bila kunisikiliza lakini Mungu yu mwema Mbowe,Mnyika wako ndani na Halima Mdee atatiwa ndani good.

KWA NINI NINA FURAHA NYINGINE?

Mwezi mmoja kabla ya kutekwa kwangu, niliandikwa kwenye kumbukumbu Mbinguni kuwa Mtanzania wa kwanza kumkoromea Mbowe kwenye kikao cha chama uani makao makuu wakiwepo Meya wa jiji leo Isaya Mwita, Boniphace Jacob, Mnyika, Halima Mdee, Dr Slaa nk.

Baada ya kumwambia Mbowe Ukweli kuwa asijidanganye kuwa Chadema ina wafuasi walioiva kiitikadi no no!,Chadema ina washabiki tu. Na nikamwambia wenye shida ni viongozi wa chini na si yeye anayekuja na V8 anakuta umati anahutubia anaondoka.

Nikamalizia nikamwambia ili aelewe kuwa wanachadema wengi hawajajengwa kiitikadi bali ni washabiki tu,Mbowe alikasirika na kuagiza Mabaunsa waniondoe,busara ya Dr Slaa,maneno yangu yalimuingia akaomba nisitolewe niachewe.

Kwa hiyo baada ya Kauli hiyo leo ninapoona mdogo wake Mbowe wa Machame shemeji yangu Godbless Lema akishuhudia Mbowe anabaki peke yake gerezani hamna hata Sisimizi akiandamana au wa kumtetea wajue wako bungeni bara na Visiwani kwa hisani ya CCM basi.

KWA NINI MNYIKA NA MBOWE WALIHARIBU CHADEMA?

Miaka ya nyuma kabla Chadema haijavamiwa na Combination ifuatayo ilikuwa poa sana,ilijengwa kuchukua Dola mwaka 2025.

COMBINATION MBAYA

NCCR MAGEUZI TO TLP (WASOMI) WAPAMBE WA MREMA WAWILI UKAJUMLISHA NA CUF WAPAMBE WAWILI WA PROFESA LIPUMBA (MAPANGA SHAA,SAIGON) WAKAAMIA CHAMA KINACHOJIJENGA.

KWANZA WOOTE WANNE WALITAFUTA UPAMBE KWA MBOWE NA MNYIKA NA KUJA NA MIKAKATI PUMBAVU ILIYOKIUA CHADEMA.

NI KINA NANI HAO.

Nccr/Tlp wapambe wa Mrema waliokuwa wabeba mabegi,ni GODBLES LEMA NA TUNDU LISSU, Vijana wa #ChademaMangeKimambe hawajui kuwa hao jamaa ndo walikuwa wabeba mabegi ya Mrema mnayemdharau leo, walikula, wakaiba kwa hisani ya Mrema.

Hawa walikuja na Dharau na mikakati ya kihovyo na mikelele kwenye chadema kwa hiyo utoto wao ukasikilizwa hatimaye chadema ni Mahututi.

CUF wapambe wa Profesa Lipumba,hao ni Mbunge wa Bukoba mjini Wilfred Lwakatare na Mbunge wa Ubungo SAYED KUBENEA.
Vijana wa #ChademaMangeKimambeMitandaoni hawajui kuwa huyu Kubenea alianza kuandika gazeti la Prof Lipumba na kubeba mabegi yake.
Kwa hiyo Baada ya Lwakatare naye kuhamia chadema na kupewa ukurugenzi wa Ulinzi na usalama wa mali za Chadema na viongozi akaleta mfumo wa kuteka,Kuua na kutindikali watu.

Hii mikakati nayo imechangia chadema kufa kifo kitakatifu,walijua wanajenga kumbe wanabomoa.

Mwisho wakuu wakuu leo nina furaha,Mbowe asitegemee Sisimizi ataandamana na dada yake Mange Kinambi ajitafakari sana.

Nchi hii watu wanataka Viwanda wakuu, Mtoto wa Mbowe, DUDLEY alimaliza SUNSEX UNIVERSITY UK akafanyiwa sherehe SERENA HOTEL leo ameajiliwa STANBIC BANK MAKAO MAKUU HAJUI HATA KISWAHILI,LEO MBOWE ANATAKA TUFE WATU 100 NO NO NO NO NO.

UJUMBE KWA RAIS,AMIRI JESHI MKUU NA MKUU WA NCHI WETU MPENDWA JIWE DR JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI,
tuko nawe tulinde na tulindie familia zetu,sina hata PASSPORT HALAFU MBOWE ANATAKA TUFE CHAA!.

NI WENU MTANZANIA MNYONGE JOSEPH YONA.

Mwenyekiti wa CHADEMA Temeke Joseph Yona, apigwa na kuumizwa vibaya!
 
"UJUMBE KWA RAIS,AMIRI JESHI MKUU NA MKUU WA NCHI WETU MPENDWA JIWE DR JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI"

Jiwe halina hisia , haliwezi kupokea ujumbe wowote na kuufanyia kazi.
Jiwe lipo lipo tu halihisi maumivu ya watu wengine wanaokanyaga jiwe hilo
Jiwe lipo lipo tu mpaka lisukumwe na wasamalia wema ndio liweze kujongea ipo siku jiwe litasombwa na mafuriko.
 
Uhuru wa kuongea na kutoa maoni, bunge live, mauaji yanayofanywa na polisi na watu wasiojulikana, kutekwa na kupotezwa, ukosefu wa ajira, ukandamizaji wa vyama vya upinzani, tume huru ya uchaguzi, matumizi yasiyoidhinishwa na bunge, unyanyasaji wa watumishi wa umma, upendeleo wa maendeleo kwa itikadi ya vyama na ukanda
Haya ni baadhi tu ya yale yanayotujaza hasira. Hapo hakuna Mbowe wala Chadema. Namba ya maajabu 2604
 
"UJUMBE KWA RAIS,AMIRI JESHI MKUU NA MKUU WA NCHI WETU MPENDWA JIWE DR JOHN JOSEPH POMBE MAGUFULI"

Jiwe halina hisia , haliwezi kupokea ujumbe wowote na kuufanyia kazi.
Jiwe lipo lipo tu halihisi maumivu ya watu wengine wanaokanyaga jiwe hilo
Jiwe lipo lipo tu mpaka lisukumwe na wasamalia wema ndio liweze kujongea ipo siku jiwe litasombwa na mafuriko.
Nimetoka kuota...umejiunga Ccm
 
Back
Top Bottom