Mbowe, Mnyika, Lema na Maganga mmenichekeza sana, kweli wanasiasa akili zenu mnazijua wenyewe

Ekethocho

Member
Jul 19, 2018
99
189
Nimewasikiliza baadhi ya viongozi wa Upinzani wakizungumzia masuala mbalimbali kwa nyakati tofauti nimecheka sana. kweli Wanasiasa akili zao wanazijua wenyewe.

1. Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani ananyimwa dhamana? Ni hatari sana kwa Demokrasia nchini-Freeman Mbowe.
Tafakuri: Hivi yawezekana kabisa Mbowe alikuwa anafanya makusudi kutokwenda kwenye kesi kwa kujidanganya kwamba yeye ni Mwenyekiti na Kiongozi wa Upinzani na hivyo hawezi kuchukuliwa hatua na Mahakama! So Sad!.

2. ACT-Wazalendo sisi ni Wacha Mungu, hatuwezi kumuombea Rais Magufuli kwani kufanya hivyo ni kumkufuru Mungu-Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Yeremia Maganga.
Tafakuri: mcha Mungu halafu hutaki kumuombea Binadamu mwenzako? Mafundisho gani ya Dini na Kitabu gani Kitakatifu kinakuelekeza hivyo?

3, Watumishi wa Mungu mnajua yanayoendelea Nchini, Ukimya wenu ni hatari. Ni Mungu gani mnaye mhubiri ?

Tafakuri: Lema anataka kuwafundisha Watumishi namna ya kufanya huduma zao za Kiroho? Yeye Lema nani anamfundisha kufanya siasa? Kama anaona Watumishi wa Mungu wameshindwa kutoa huduma anayotaka yeye si avae mikoba yao, maana hakuna aliyezaliwa kuwa mtumishi wa Mungu.

4. Kama Magufuli, Waziri wa Katiba na Sheria, Mwanasheria wa Serikali na DPP wanaona Mawakili wa Serikali katika kesi ya Mbowe na Ester Matiko wanatumia vibaya muda na Rasilimali Fedha za Mahakama basi waamuru Mahakama kufuta kesi maana Serikali ina uwezo huo-John Mnyika 05/12/2018 wakati akiongea na wanahabari

Tafakuri: Mnyika anataka Serikali iingilie uhuru wa Mahakama waakti wao ndiyo wa kwanza kusema Mahakama haziko huru?

Hitimisho: Wanasiasa akili zao wanazijua wenyewe. Wanadhani ujumbe wanaoutoa wanaufikisha kwa watu ambao hawajui kuchambua mambo.
 
Ametuchekeza kweli huyu... Kamusi .com ngoja nkaangalie maana yake then ntarud
 
Back
Top Bottom