Uchaguzi 2020 John Mnyika: Kuongea na vyombo vya Habari, saa 8 mchana

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
John Mnyika: Jitihada za mawasiliano na NEC juzi, jana na leo mpaka muda huu kudhibiti hujuma kwenye uapishaji wa mawakala zimekwama maeneo mengi. Nitazungumza vyombo vya habari HQ saa 8 mchana. Kwa sasa , #PeoplesPower itumike maeneo ambayo hujuma zinaendelea. #SasaBasi.

=====

MNYIKA: MAWAKALA WETU HAWAPEWI CHOCHOTE KUTHIBITISHA WAMEAPISHWA

Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika amesema wanaona kitendo cha asilimia kubwa ya Mawakala wao kutopewa uthibitisho kuwa wameapishwa kama tatizo litakaloleta tatizo kubwa zaidi siku ya kupiga kura

Amesema wanaitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuelekeza Wasimamizi wa Uchaguzi kutoa nakala za barua kwa Mawakala, na wao kama Chama wapewe ili Wakala anapoenda Kituoni ajue tayari ameshatambulishwa na ana ushahidi wa hilo

Amesema, "Tume kwa nia njema kabisa isipoyafanya haya ya kurekebisha hili jambo la mawakala, tunawaomba wananchi waendelee kujiandaa kupiga kura tarehe 28 kumchagua Tundu Lissu kwa wingi, kwakuwa tutaungana pamoja kuhakikisha kwa namna yeyote ile Mawakala wetu wanaingia ndani ya Vituo"

Ameongeza, "Ikibidi kutumia falsafa yetu ya People's Power tutatumia, lakini tumeshasema Uchaguzi huu sasa basi. Hujuma tulizofanyiwa huko nyuma imetosha"
 
Hujuma katika sura ya aina yake!
458909807.jpg
 
Sawa. Tunakusubiri. Na usiache kuongelea suala la kuapishwa mawakala wa CHADEMA
 
Mnyika ongea na lissu na mbowe ,hatuwezi kuchanga pesa ili mfike TZ nzima kuwapa watu elimu ya uraia ili wawakatae sisiemu na vibaraka wake halafu NEC wakatae hivi hivi kuwaapisha wamakala wa upinzani ,tunataka jibu moja kwamba kama hakuna mawakala hakuna uchaguzi ,na sio kwamba hakuna uchaguzi kwamba chadema wanasusa hapana ,yaani tunagawa mabox ya kura ,tunagawana na vituo vya kupigia kura, kwa kifupi hakuna mtu kupiga kura mpaka mawakala wa upinzani waapishwe wote kwenye vituo vyote 80k+
 
Back
Top Bottom