John Mnyika amepewa nini na CCM?

Fundi Madirisha

Senior Member
Jun 30, 2020
140
1,000
Kwanza niwape pole sana uongozi na wanachama wa CHADEMA kwa madhila anayopitia kiongozi wao mkuu wa chama, hakika ni majaribu makubwa sana kwake yeye Mbowe binafsi, chama, na familia yake kwa ujumla.

MNYIKA AMEPEWA NINI NA CCM?

Hivi kweli CHADEMA leo ni wa kua wapole kiasi hiki kiongozi wao anateseka mahakamani kwa kesi ambayo inaonekana kabisa ni ya kufikirika, hakuna uhalisia wa kesi hapo ni mabishano tu ya kisheria against ukweli wa jambo lenyewe. Wanachama wa CHADEMA wapo kimya hakuna reactions zozote dhidi ya uonevu huu.

CHADEMA tazameni yalikuwa yakiendelea Kenya wakati Raila Odinga anakamatwa na kuwekwa ndani, angalie yaliyokuwa yakiendelea Afrika kusini wakati Jacob Zuma alipohukumiwa? Kesi zenye janja janja ya kisiasa si za kuvumilia wala kuendekeza. John Mnyika Kama katibu mkuu wa chama nilitegemea afanye organization ya wanachama nchi nzima wawe na amsha amsha ya kukataa uonevu. Mmekaliaooh sijui jambo liko mahakamani, jambo lenyewe lina sura gani?

Napata mashaka sana na John Mnyika Kama si Jasusi ndani ya chama.Ameshindwa kabisa ku-organize katiba mpya akidai eti ni swala la kitaifa kila mwananchi achukue hatua, yaani hata wanaccm wachukue hatua kwenye issue ya katiba mpya? Mnyika naanza kutilia shaka kama system haijamdaka na kuanza kumtumia. Wananchi na wanachama wapo tayari kila mkoa yeye anasubiri nini? Kuna Polisi wa kuwakamata wanachama wote nchi hii kwa sababu wanadai tume huru ya uchaguzi na katiba mpya?

Nimemlenga Mnyika kwa sababu ndiye katibu mkuu wa chama upinzani chenye wanachama na wafuasi wengi nchini, mimemtaja Mnyika kwa sababu ndiye mtendaji mkuu wa chama ambacho ndicho kinaweza kua mbadala wa mawazo ya serikali ya CCM. Yaani tangu Mbowe awe ndani chama ni kama hakina mtu.
 

zandrano

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
4,408
2,000
Mbowe ndiye kakifikisha chama hapo kilipo leo hii.
aliambiwa ang'atuke wapi! alilewa uchu wa madaraka, matokeo yake ndio hayo leo hii anadhalilika.
kayataka mwenyewe.
kwa sasa Chama hakina tena viongozi madhubuti.
Mnyika, Benson, hamna kitu hapo.
chama kinahitaji mabadiliko ya viongozi wote wa juu.
 

Baraka21

JF-Expert Member
Mar 15, 2021
1,282
2,000
Acha mambo yaende jinsi yalivyo. Siku zote dhuruma haijawahi kushinda. Hakuna kiongozi katili aliyewahi kutokea Tanzania zaidi ya magufuli ila sasa analiwa kiboga na mapepo wachafu huko kuzimu.
Mfungeni Mbowe mioyo yenu ipate amani.
 

issenye

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
3,541
2,000
Umeandika kinyonge sana hahha Samia amewanyoosha sana anamalizia viporo vya jpm

USSR
katunjoosha kweli kweli maana wanaccm wakienda dukani wananunua bidhaa bei yrahisi tofauti na wapinzani. Tozo za miamala ya simu hazitozwi kwa wanaccm wala makato kwenye manunuzi ya umeme
 

SAGAI GALGANO

JF-Expert Member
Nov 13, 2009
31,826
2,000
Mwaka jana tulipiga dua kuwa aliyeagiza kuvuruga uchaguzi mkuu aadhibiwe na kweli akatoweshwa kwenye uso wa dunia,ni wakati wa kuomba Mungu huyu anayebambikia watu kesi na yamkute hayo hayo,naamini Mungu ataingilia kati tena.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom