Jackbauer
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 6,038
- 2,199
mkuu hii fani ni kali!specialised contractors for demolition!
Kwi kwi kwi!
mkuu hii fani ni kali!specialised contractors for demolition!
Ama umekwepa kujibu swali langu au ni swali gumu kidogo kwako
Hizi flyover mnazotaka kujenga dar jiulize zitajengwaje makutano ya Morogoro Road na Mandela road kama gorofa hilo halibomolewi. Waziri kaona mbali zaidi kuliko wachangiaji wengi wanavyochangia hapa. Kumbuka flyover zinahitaji eneo kubwa sana ili kupisha ramps za entrance and exit, vinginevyo tutacheza usanii wa kisiasa tu bila kufuata hoja za kiteknologia
Big up Maguvuli, go ahead.
Muuliza hii hoja ungeuliza swali ungejibiwa vizuri sana na kupata elimu ya bure, kwa kifupi
1. Thamani ya barabara itakayopita pale hata iwe ni lane moja thamani yake ni kubwa dynamically mara nyingi sana zaidi ya any standing structures!
2. Ukifocus miaka 50 au 100 ijayo we need six lanes or 8 lanes highways....
Ningekueleza in details whay that building is chaos! siyo Magufuli ni wataalamu, tatizo kubwa ni kuwa masterplan za mji zinachakachuliwa kila siku na siasa inatawala na wanasiasa hao ni kama nyie!
mwanafunzi wa certificate NIT au diploma ya civil engineering DIT, MIST au Arsuha tech wanajua vyema kabisa , achilia mbali watu wa degree ya kwanza mlimani au URP ardhi institut
This is common practise even in developed world especially USA where they have even specialised contractors for demolition!
Try to search in your google you will be amazed
Guys learn to look things in different direction hii ni aibu kubwa !! STOP!
Wanaotakiwa kulaumiwa ni wale walioruhusu ujenzi wa jengo hilo na ni serikali yenyewe bila kufuata taratibu za hifadhi ya barabara. Miundombinu ya sasa tunaona haikidhi je kwa kizazi kijacho tuonekane na sisi tungali wajinga hivyo?
Hapana Mheshimiwa Magufuli go ahead.
Nani alikuambia fly-over zinachukua eneo kubwa?
Acheni huo ushabiki. Wataalamu wana-design kitu kwa kufuata matakwa ya mteja. Msitumie hoja za kitaalamu kutufilisi. Acheni kutumia hela zetu vibaya. Kama mnataka fly-over eneo la sasa la barabara linatosha. Si lazima kituo cha mabasi kiwe ubungo.
Nyie mbona mnadiscuss ujinga? mnalijua lile gorofa la masaki lililobomolewa kwa kuwa kule hakukutakiwa kuwepo jengo lefu kama lile? mnajua gharama za jengo lile? Nyie ni wafuasi wa serikali ambayo inawaonea wananchi na nyie mmekubali. Sheria haijalishi serikali au mtu binafsi. Unaponibomolea kijumba changu kidogo ni sawa na yule unayembomolea gorofa. Mmeshafanya projection in twenty five years mahitaji ya ile bara bara yatakuwaje?
Magufuli yuko sawa myie ndio mmepotoka
na hizi sheria tulizitunga tukijua kuna mazezeta kama tanesko hukwamisha maendeleo.mpaka hapo zitakapobadilishwa,magufuli ana haki ya kutekeleza majukumu yake bila kuangalia nani kavunja sheria.Sheria tunazitunga wenyewe
mzee nakuunga mkono, unajua hii inchi ii iendelee sasa inabidi wapatikane "punguani" wengine kama Magufuli kama watano tu..ni bora tuanze upya kuliko kuendelea na maupumbavu yanayofanyika saiz..kwani wakati hayo majengo yanajengwa walikuwa hawajui kama ni barabara...BOMOA TUUUU...p.%^$**fu!! ndio tutie akili kwamba vitu huwa vinakwenda kwa mipango, na nnahakika wakibomoa leo kesho ndio watakuwa makini zaidi katika haya mambo la sivyo ujinga huu utaendelea kila silku kujifanya wanaweka majengo ya serikali maeneo yasioruhusiwa wakati wakipeana viwanja wenyewe kwenye maeneo yanayoruhusiwa..huu si ujinga...!!?? VUNJAAAA.. kesho ndo watatia akili kwamba mmh tukijenga hapa tena watavunja kama walivyovunja tanesco!! nchi yenyewe ishaoza hii..Strategically, kama majengo hayo yamo ndani ya eneo la barabara ni lazima yabomolewe.
Kabla ya kumwona Magufuli hana akili ni lazima wote mnaopinga uamuzi wa Magufuli kujiuliza maswali.
Hivi ni nani aliyeamuru ujenzi wa majengo haya ya mabilioni bila kukaa chini na kupanga kila kitu kikamilifu??
Master plan ionyeshayo eneo la Barabara ilichorwa mwaka gani?
Kama Master plan ilikuwepo kabla ya ujenzi wa barabara ni kwa nini Tanesco iliendelea na ujenzi katika eneo la barbara? Ni kwa nini serikali haikuizuia Tanesci kujenga akatika eneo la barbara?
Eneo la Ubungo ni Entrence na Exit kuu ya jiji la Dar, kama kwa namna yeyote ile majengo hayo yamo ndani ya eneo la barabara ni lazima yabomolewe kupisha upanuzi wowote wa barabara uiliopangwa hapo awali. Comparatively thamani ya majengo hayo ni ndogo sana ukilinganisha na hasara itakayosababishwa ya kuzuia upanuzi wa barabara.
Kama kwa akili zenu mnamuona Magufuli ni Punguani kwa kushikiria msimamo wake wa kubomoa majengo yote yaliyomo katika eneo la barabara! Mnamuonaje na mtamwita jina gani mtu aliyeng'ang'ania kujenga majengo ya thamani kubwa katika eneo la barabara?
Kulikuwa na Busara gani kujenga majengo hayo ndani yana eneo la barabara??
Ni nani aliyekuwa Waziri wa wizara husika wakati wa ujenzi huo?? Na ninani aliyekuwa Bosi wa Tanesco wakati huo??
Serikali ya CCM ilikuwa wapi na mastar plan yake wakati Tanesco wakijenga katika eneo la barabara??
Kipimo na Ujinga,Upunguani Uhuni na Utovu wa Nidhanmu Tanzania ni nini??
Magufuli ni Punguani, aliyesimama kidete kujenga katika eneo la barabara tutamwitaje??