John Magufuli: Ninautamani urais!

John Magufuli: Ninautamani urais!

Magufuli ni jembe,CCM wakimteua huyu watapata kazi rahisi sana kwenye uchaguzi wa 2015..

Kwa uwezo wa utendaji kazi,hakuna mwanasiasa yeyote hapa nchini anayemzidi Magufuli kwenye hilo, akiteuliwa huyu kura yangu anayo...
Na hatimae yakatimia. JF ni kiboko
 
m
Magufuli (na wengine wachache CCM) anaweza kua Rais mzuri pale tu atakapopitishwa kwa kura za wanaCCM wengi bila ya kushikwa mkono na kakikundi cha watu fulani fulani au kupata huruma ya M/kiti...hapo atakua na "wide mandate" ya "kufanya" yale ambayo Magufuli tumezoea anafanya...otherwise Marais wote wa CCM watategemea a combination ya Dhaifu pamoja na kikundi fulani kitakachomfanya Rais ajaye wa CCM awe dhaifu mwingine (labda atokee kichaa atakayepiga sarakasi na kuwageuka wote waliomuweka kwenye kiti)....


mnammiss dhaifu
 
Aisee duh! Lakini bado mafisadi Mkapa na Kikwete wakamsukumizia Ikulu!!!

Huyo jamaa hafahi kuwa rais hana hekima wala busara maamuzi yake huwa ni ya kukurupuka sana ameitia sana hasara serikali imekuwa ikilipa fidia mara kwa mara kutokana na maamuzi yake ya hovyo tumeona kwenye ile meli ya samaki tumetakiwa kulipa fidia shilingi bilioni 2 baada ya kushindwa kesi pia huyu jamaa ndiye aliyepeleka pendekezo na kushupalia kuuza nyumba mbali mbali zilizokuwa zinamilikiwa na serikali na yeye mwenyewe akiwa mnufaikaji wakati wa utawala wa serikali ya Mkapa wakati huo Magufuli alikuwa waziri wa nyumba na makazi wamejiuzia na kujichukulia majumba mengi ya serikali kwa bei chee mpaka aibu maeneo mbali mbali nchini mfano Nyumba za Oysterbay,Masaki,Msasani,Chang'ombe,Kurasini,Mikocheni yani wamejiuzia yale amjumba yaliyokuwa kwenye maeneo mazuri yote nchini katika mikoa yote .Hayo tu machache leo mnasema huyu jamaa anafaa kuwa rais hfahi hata kidogo na ikitokea tu CCM wamempitisha huyu jamaa wapinzani wana mengi ya kuzungumza kuhusu huyu jamaa hafahi hata kidogo ni Fisadi sana kwa watu wanaomjua vizuri
 
CCM hawawezi kumteua huyu apeperushe bendera ya urais maana atawafunga wote waliofanya ubadhilifu. Wanachofanya ni kumwekam2 atakayelinda mfumo wa kifisadi, wanataka m2 subjective sio objective kama Magufuli.
Malolella upo Mkuu!, hakika ulimfahamu barabara Magufuli [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Huyu atakuwa dhaifu kuliko JK! Mambo mengi ya kitaifa ananyamazia hatujui msimamo wake...kwanza toka lini injinia akawa raisi! Akajenge madaraja huko!
Mkuu uliona Mbali sana, comment yako hii ilikuwa utabiri tosha 2O13/....
 
Hana Nguvu za kisiasa ndani ya CCM na wala hana sifa zozote kuwapita wenzake ndani ya CCM kama Lowassa, Membe, Sitta, Mwakyembe, Mwandosya, Wassira, Mwigulu, Nchimbi.
Ila sifa moja ya kiCCM ya msingi anayo, ambayo ni Ufisadi. Magufuli ni Fisadi mzuri sana.
Lakini pia ni mnafiki mkubwa, kwani ni juzi tu alimkana Sitta na kudai hana mpango wa Urais kabisa!!
Ukweli ukweli...
 
Magufuli ni jembe,CCM wakimteua huyu watapata kazi rahisi sana kwenye uchaguzi wa 2015..

Kwa uwezo wa utendaji kazi,hakuna mwanasiasa yeyote hapa nchini anayemzidi Magufuli kwenye hilo, akiteuliwa huyu kura yangu anayo...
Ulijuaje??
 
Back
Top Bottom