Waungwana naomba mulonge si kwa ushabiki wala unafiki, ila kwa hoja zilizoshiba na zenye mashiko. Kama uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ungefanyika leo, ni nani ungempa kura yako aiongoze Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kati ya Dr. MAGUFULI na EDWARD LOWASA?
Kiongozi ambae ataweza kututoa kwenye hii bahari ya Ufukara, asimamie haki na kutetea maslahi ya wanyonge wa Tanzania na raslimali zao ambazo kwa mda mrefu sasa zinawanufaisha wachache hasa wa tabaka tawala?
Najua wengi ni wakereketwa wa vyama fulani fulani vya siasa hapa nchini, naomba tutoke huko kwa mda mfupi, tujengane kwa hoja zenye mashiko bila kujali chama cha siasa wanachotoka niliowataja. Mikataba isiyo na tija kwa Taifa, hofu ya kuwawajibisha mafisadi, wala rushwa na wimbi la uanzishaji wa mifumo ya utendaji kazi isio na tija kwa Taifa iwe dira yetu katika kuchambua uwezo wa wawahusika niliowataja hapo juu kwenye nafasi ya Uraisi wa nchi hii.
Mashiko ya hoja zenu, yatatujenga wengi na kutoa mwelekeo mpya wa harakati zinazoendelea hapa nchini na baadhi ya vigogo wenye nia ya kuwania nafasi 2015.
By LULAMSO