John Magufuli: Ninautamani urais!

John Magufuli: Ninautamani urais!

Hii ni habari moja njema sana huyu mtu atatufaa watanganyika wote kama atachaguliwa kuwa kiongozi wetu baada ya Jakaya,urais ni halali yake ,wenyewe kazi yake mmeiona na mnaijua,mimi ndio chaguo langu kubwa na ninaamini atakuja fanya makubwa sana nchini.M/Mpamba.
 
Hii nchi kila mtu anaweza kuwa Rais mbona Zitto ni Rais wa Gombe advisors bana ?
 
Ingekuwepo award ya politician performer ktk maisha yao ya siasa za Tanzania huyu angepata na tena ile ya heshima kabisa ni waziri pekee watanzania wametokea kumpenda!

Huwa japo napata kumfananisha na marehemu Sokoine!
 
Makufuri anafaa kuwa president, bt mahali pa kupitia cpaoni, maana jamaa wanaogopa wakimruhusu tu kunawatu wataihama nchi,

C unakumbuka ile inshu ya kutaka kujihudhur kwa kuingiliwa ki utendaji? Ukiconect utajua kuwa pamoja na utendaji bado kunawatu katika siasa(ccm) wanamuona hafai kuwa rais maana hana Subira, japo kwa watz wengi anafaa kuwa presidor!
 
Magufuli anafaa kuwa Waziri Mkuu kwa maana ya utendaji kuwafatilia mawaziri hapo nadhani atafit.
 
Tangu Edward Sokoine, hii nchi haijawahi kupata waziri mchapa kazi na anayependwa na wananchi kama Magufuli. Lakini ukisoma kwenye magazeti na mitandao kila siku unasikia watu wanaimba Lowassa, Lowassa, Lowassa!! Ukweli ni kuwa Lowassa hamfikii Magufuli kwa utendaji hata nusu, ila Lowassa ana mtandao wenye mapesa mengi ya kifisidadi ambayo yamenunua media ya Tanzania ku-brain wash watu wadhani eti yeye ni mtendaji bora. Kumbe Lowassa ndiye aliyeleta shule za kata zenye walimu vodafasta zilizoporomosha elimu ya Tanzania, ameleta mzimu wa Richmond unaoendelea kuitafuna nchi na kujilimbikizia mali kibao ndani na nje ya nchi.
 
WAZIRI wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, amesema kuwa hana mpango na urais wala kujitangaza kuwania nafasi hiyo.


Hatua hiyo ilitokana na wananchi wengi kumshangilia na kumwita Rais wakati ziara ya siku tatu ya kukagua miradi ya ujenzi wa barabara, madaraja na vivuko.


Akiwa katika eneo la Tegeta, aliwaeleza wananchi kazi ambazo serikali imekuwa ikizifanya katika kuhakikisha inaondoa adha ya foleni jijini Dar es Salaam ambapo wakimshangilia na kumpatia sifa za kuwa Rais 2015.


Hata hivyo, Dk. Magufuli alikanausha habari hizo na kueleza kuwa ni maono ya wananchi na si yeye.


"Sina mpango huo nipo katika ziara kuangalia utendaji wa watu tuliowapatia kazi, hayo ni maono yao,"alisema.


Magufuli anaonekana kuwa tofauti na baadhi ya vigogo wa CCM ambao kwa nyakati tofauti wamekuwa wakijinadi kuusaka urais.

Source: Tanzania Daima
 
MAGUFULI ni mchapa kazi japo urais hafai, anafaa apewe uwaziri mkuu au uwaziri wa Elimu. Sikujua kwanini Jk alimnyima Magufuli uwaziri mkuu akampa Pinda pinda! Sijui alishauriwa na nani na kwa maslahi ya nani!
 
Apewe uwaziri wa elimu aisee.atasaidia kuokoa elimu ya Tanzania.
 
Wengi wanasukumwa na wivu. Msomeni Pombe vizuri ... ...... ... good move.
 
Tungekuwa na magufuli wengi ingesaidia sana. Kila wizara anafanya frsh.
 
Mimi natamani sana Mwakyembe awe president then huyu bwana Magufuli apewe u pm(PRIME MINISTER)..Hapo nchi itasonga mbele..kila wizara itakuwa safi na madudu yote tupa kule
 
Huyu asipewe wizara tena apewe uwaziri mkuu..unajua waziri mkuu ndio kiranja wa mawaziri wote na ndio mtendaji mkuu wa serikali..Mimi sitaki awe rais kuna maeneo yatakuwa yanakwama kulingana na katiba..ila mpeni u pm nakwambia wizara zote na madudu yote yataondoka..habari za twiga kupanda ndege zitakuwa historia...
 
...anaijua vizuri ccm,wapo ambao hawaoni taabu kuua yeyote anayeonekana kufunika ndoto zao...
 
Ukikaa chini na utafakari kwa makini utaona kila kitu katika nchi yetu kimesambaratika.Sekta muhimu katika kujenga maendeleo rasilimali watu imetupwa mbali. Elimu, afya, uvuvi, kilimo, nyumba na makazi, umiliki wa mali na ardhi vyote vinawaneemesha wanaoitwa wawekezaji. Raia wa Tanzania ameonekana si chochote si lolote, wakazi wa vijijini hadhi zao zimebadilika, kimsingi wanaonekana ni wapuuzi ambao ubinadamu wao unafananishwa na wanyama. Wanaonekana si watu wanaostahili kuishi nyumba nzuri, kunywa maji safi wala kupata huduma nzuri za afya, wameonekana na watu wa daraja la mwisho hivyo kufanya asilimia kubwa ya watanzania wanaounda kundi hili kuonekana wanaishi kwa fadhila tu ya watu 'wawekezaji au watu wenye masilahi na wawekezaji.

Nikiangalia kushoto na kulia sioni mtu mwenye nia na lengo la dhati la kututoa katika hili. Ndani ya CCM simuoni, huko UKAWA nako ndo kabisa na wapi sijui, kwa akina Dovutwa wote waliobaki wasakatonge wenye kuamini katika "wawekezaji"..

Mtu pekee ninayemuona kuwa anaweza kuwa "Musa" wetu na kututoa hapa tulipo ni John Pombe Magufuli. Angalau katika viongozi wa nchi hii hatishwi na wawekezaji na mwenye uthubutu wa kuwakemea na hata kuwashughulikia wanapopindihs utaratibu, pia Magufuli ndiye kiongozi pekee aliyepo katika serikali yetu ambaye kwanza hutambua kazi yake kwa mujibu wa sheria na huamua kuitekeleza pasipo kupepesa macho. Ana uwezo wa kusema ukweli hata kumwambia Rais mbele ya hadhara. Alishfanya hivyo kwa rais aliyestaafu Benjamin Mkapa na alishawahi kumwambia Rais wetu Kikwete umuhimu wa kufuata utaratibu na sheria na kuacha kusikiliza watu wenye fitina, uongo, umbea na uzandiki.

Bila kujali itikadi, kwa kuifikiria zaidi Tanzania, Tanzania ipi katika hali mbaya kiuongozi, nchi imepoteza muelekeo, watanzania tumedharau na tumeacha kufuata utaratibu, tumejenga utamaduni wa njia za mkato na nani ana nani wa kumlinda. Kila mtu anavunja sheria, kuhujumu nchi na kumuonea anayeweza kumuonea kwa nafasi yake na kwa nguvu yake.

Uongozi wa Magufuli umeonesha hauna kujuana, kupendelana, kuoneana haya wala aibu, ni uongozi wenye kuchapa kazi kwa kufuata sheria na uongozi wenye kuonesha kila kitu kina maana na bora kwa watanzania, hata uvuvi wa samaki.

Umefika muda kwetu watanzania tuamue kuondoka katika hali hii, tutafuta kiongozi ambaye hata kwa macho hatuna mashaka nae, kiongozi ambaye mioyoni mwetu tutakuwa na imani naye na tutakuwa kwatu kuwa nyuma yake kumfuta hata kama njia takayotumia itakuwa na miiba ilhali itatuchoma kiasi lakini tutafika kule tunapotaka kwenda kuliko ilivyo hivi sasa ambapo tumekuwa tunazunguka mduara pasipo kwenda popote badala yake tunaishia kupata kizunguzungu tu
 
Mzee wa visasi asiyependa challenge si wapinzani wake woye ndani nanje ya chama wataishia jela
 
Back
Top Bottom