John Heche: Wananchi wa Tarime jiandaeni, Tutavamia mgodi wa Acacia na kupora kila kitu

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,241
2,000
Mbunge wa Tarime John Heche amesema kwa kuwa imethibitika kampuni ya Acacia ni kampuni feki anawahimiza wananchi wa Tarime wajiandae kuingia mgodini kuchukua kila kitu hadi magari kwa kuwa hakuna forula ya kukamata mwizi Tarime

Amesema wananchi wa Tarime wameumizwa sana ikiwa ni pamoja na kutolipwa fidia na kuna ripoti ya waziri inasema wananchi takribani 64 wameuawa ili kuwalinda hao wezi wa Acacia

Heshima kwenu wakuu,

Mbunge wa Tarime John Heche(CHADEMA) amewaagiza Wananchi wa Tarime wajiandae akitoka bungeni ataenda Tarime kuwaongoza wavamie Mgodi wa Accacia ulioko Tarime.

Anasema Kwamba "Accacia ni Kampuni feki, ni kampuni hewa ambayo haipo na ipo Tarime na inawaharibia wananchi wa Tarime. Kuanzia leo, nawaambia wananchi wa Tarime wajiandae tuingie mle mgodini tuchukue kila kilicho chetu. Na mimi hili nalisema humu Bungeni na ntalifanyia kazi Mimi Sidanganyi. Sababu Wananchi wa Tarime wameumizwa, na kampuni ile rais amesema ni feki, na hakuna fomula ya kukamata mwizi".

Mlisema wenyewe na bunge limesema, Fomula ya kukamata mwizi ni kupambana naye. Sisi hatutaruhusu madini yatoke pale, ndege ikitua tunapiga mawe na hilo linaendelea ninaorganisation pale. Magari yao tutayakamata, Kwanza tunawadai fidia nyingi kweli kweli pale Tarime. Tunataka hayo mambo yafanyike sasa hivi.Tunazuia Mchanga huku dhahabu inaondoka, hii si sawa. Watu wengine tuna machungu na tuna maaumivu na hili. Kama mkinikamata Watanzania watajua hamko tayari kupambana Vita hii. Nataka nani atanizuia kukamata mwizi. Nataka tuone kama Polisi watanikataza kukamata Magari ya Mwizi
 
Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
206,392
2,000
Mbunge wa Tarime John Heche amesema kwa kuwa imethibitika kampuni ya Acacia ni kampuni feki anawahimiza wananchi wa Tarime wajiandae kuingia mgodini kuchukua kila kitu hadi magari kwa kuwa hakuna forula ya kukamata mwizi Tarime

Amesema wananchi wa Tarime wameumizwa sana ikiwa ni pamoja na kutolipwa fidia na kuna ripoti ya waziri inasema wananchi takribani 64 wameuawa ili kuwalinda hao wezi wa Acacia

Huu ni uchochezi sijui atayaongelea nje ya Bunge ili adakwe?
 
Prognosticator

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
40,128
2,000
Mbunge wa Tarime John Heche amesema kwa kuwa imethibitika kampuni ya Acacia ni kampuni feki anawahimiza wananchi wa Tarime wajiandae kuingia mgodini kuchukua kila kitu hadi magari kwa kuwa hakuna forula ya kukamata mwizi Tarime

Amesema wananchi wa Tarime wameumizwa sana ikiwa ni pamoja na kutolipwa fidia na kuna ripoti ya waziri inasema wananchi takribani 64 wameuawa ili kuwalinda hao wezi wa Acacia

Wakurya wakisema wanamaanisha. ACACIA kimbieni tu!
 
Ndukidi

JF-Expert Member
Jun 30, 2012
1,499
2,000
Mihemko kwenye ubora wake.
Yaani huyu ni wa ajabu hata aliyekabidhiwa hiyo ripot hakutoa hayo maamuzi.

Jamani busara itumike kwani sisi wenyewe ndio tuliojiibia

Atasababisha watu waende kumwagwa kinyesi bure...
 
darcity

JF-Expert Member
Jul 20, 2009
5,374
2,000
Hiyo siku ya trespassing awe mbele kabisa ili aongoze zoezi lake la uporaji kama Joshua Nassar
 
figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
16,721
2,000
Heshima kwenu wakuu,

Mbunge wa Tarime John Heche(CHADEMA) amewaagiza Wananchi wa Tarime wajiandae akitoka bungeni ataenda Tarime kuwaongoza wavamie Mgodi wa Accacia ulioko Tarime.

Anasema Kwamba "Accacia ni Kampuni feki, ni kampuni hewa ambayo haipo na ipo Tarime na inawaharibia wananchi wa Tarime. Kuanzia leo, nawaambia wananchi wa Tarime wajiandae tuingie mle mgodini tuchukue kila kilicho chetu. Na mimi hili nalisema humu Bungeni na ntalifanyia kazi Mimi Sidanganyi. Sababu Wananchi wa Tarime wameumizwa, na kampuni ile rais amesema ni feki, na hakuna fomula ya kukamata mwizi".

Mlisema wenyewe na bunge limesema, Fomula ya kukamata mwizi ni kupambana naye. Sisi hatutaruhusu madini yatoke pale, ndege ikitua tunapiga mawe na hilo linaendelea ninaorganisation pale. Magari yao tutayakamata, Kwanza tunawadai fidia nyingi kweli kweli pale Tarime. Tunataka hayo mambo yafanyike sasa hivi.

Tunazuia Mchanga huku dhahabu inaondoka, hii si sawa. Watu wengine tuna machungu na tuna maaumivu na hili. Kama mkinikamata Watanzania watajua hamko tayari kupambana Vita hii. Nataka nani atanizuia kukamata mwizi. Nataka tuone kama Polisi watanikataza kukamata Magari ya Mwizi
 
lukindo

JF-Expert Member
Mar 20, 2010
8,475
2,000
John Heche, angalia sana maana katika watu majasiri nchi hii hakuna anayefikia hata robo ya Ndugai. Mwenzio alipigwa bakora akazimia wewe utapitiliza hadi mauti!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom