John Heche: Wananchi wa Tarime jiandaeni, Tutavamia mgodi wa Acacia na kupora kila kitu

Kusema ukweli Jamaa Yupo Sahihi... Kama kweli mumedhamiria kuzuia inakuwaje Mnazuia Mchanga ila Ndege kutua Kule Mgodini na Kuchukua dhahabu mnaruhusu? Tena na kampuni hiyo hiyo mnayosema haijasajiliwa halafu bado inaruhusiwa kuendelea na Uchimbaji na kufanya shughuli ilihali haina legal Identification.

Kwani Acacia wao wanahusiaka na Mchanga Tu.....

He is right... Naanza kumuelewa Zitto Kabwe kuwa Kila Rais aliyewahi kuiongoza Nchi hii alishaunda Tume ya Madini katika Kipindi chake Lakini Hakuna Kinachoendelea utadhani wanaongoza Nchi Tofauti...

Fuatilia Kuanzia MKapa Tume Iliundwa, Mwinyi Tume Ilundwa, Kikwete Tume Iliundwa na Leo Hii Tume Zimeundwa.. Ni Mahitimisho ya Tume Zote hizo?

This is entrance strategy ya Viongozi wetu au...
Matumbo ndio shida anapozwa account ikituna anatulia na nfio itakavyokua trust me.
 
John Heche, angalia sana maana katika watu majasiri nchi hii hakuna anayefikia hata robo ya Ndugai. Mwenzio alipigwa bakora akazimia wewe utapitiliza hadi mauti!
Ndugai ndiye aliyemtia mtu mikwaju akazimia
 
Mpaka uwe na gb kubwa ndio utamwelewa Heche. Ana maanisha hv, inakuwaje ACACIA KAMA NI WEZI HAWAKAMATWI?? Sasa kama ni wezi turuhusu tuwakamate. Mkituzuia ina maana mnawasingizia!!
Pia amemaanisha kama ACACIA ni wezi kwanini serikali iwaache waendelee kufanya shughuli za uchimbaji wakati hawajasajiriwa kisheria?
 
Shamba lililo kwenye chanzo cha maji?yeye kama kiongozi alitakiwa awe mfano awe mstari wa mbele kulinda mazingira ina maana angeshinda uchaguzi akawa waziri mkuu,si misitu yetu angeigeuza mkaa.
Nani kakwambia unajua vlchanzo kilikua karibu Kwa mita ngapi? Na he kwanini asingepelekwa Kwa vyombo vya sheria? Je huo ndio ustaarabu wa serikari Kwa wazawa na wazalendo wa nchi hii? Ccm you should think and act out side the box.
 
Leo ndio nimegundua Huyu heche ni bogus kabisa upinzani una safari ndefu Sana kwa kuwa na wabunge wa namna him.
Wewe ndio bogus usie weza kufikiria vizuri umesha ambiwa ni kampuni hewa lkn.mpaka sasa serikari yako IPO tu aijachukua hatua yeyote acacia bado wanaendelea kuchimba madini, bado wanaendelea kuingiza na kutoa ndege. Kama Wewe sio bogus tumeambiwa hao ni wezi so uiambie serikari yako ikawazuie wasiendelee kufanya shuguli zao pale.
 
Kwanini Spika anamwacha Heche anaropoka tu asimtoe nje ili Magufuli amshughulikie.Kwani si alishamwambia
 
Heshima kwenu wakuu,

Mbunge wa Tarime John Heche(CHADEMA) amewaagiza Wananchi wa Tarime wajiandae akitoka bungeni ataenda Tarime kuwaongoza wavamie Mgodi wa Accacia ulioko Tarime.

Anasema Kwamba "Accacia ni Kampuni feki, ni kampuni hewa ambayo haipo na ipo Tarime na inawaharibia wananchi wa Tarime. Kuanzia leo, nawaambia wananchi wa Tarime wajiandae tuingie mle mgodini tuchukue kila kilicho chetu. Na mimi hili nalisema humu Bungeni na ntalifanyia kazi Mimi Sidanganyi. Sababu Wananchi wa Tarime wameumizwa, na kampuni ile rais amesema ni feki, na hakuna fomula ya kukamata mwizi".

Mlisema wenyewe na bunge limesema, Fomula ya kukamata mwizi ni kupambana naye. Sisi hatutaruhusu madini yatoke pale, ndege ikitua tunapiga mawe na hilo linaendelea ninaorganisation pale. Magari yao tutayakamata, Kwanza tunawadai fidia nyingi kweli kweli pale Tarime. Tunataka hayo mambo yafanyike sasa hivi.

Tunazuia Mchanga huku dhahabu inaondoka, hii si sawa. Watu wengine tuna machungu na tuna maaumivu na hili. Kama mkinikamata Watanzania watajua hamko tayari kupambana Vita hii. Nataka nani atanizuia kukamata mwizi. Nataka tuone kama Polisi watanikataza kukamata Magari ya Mwizi
Heche acha hizo huo ni ukurupukaji, tulia chunguza thibitisha chukua hatua
 
Hawa ndo wale viongozi wanaopatikana kwa bahati mbaya.... Unahamasisha uharibifu!! Ndo maana hata maandamano yanazuiliwa, maana kiongozi mwenye busara huwezi tamka hivyo!!
 
wakati mwingine hawa jamaa akili zao ni za hovyo kweli
kabisa heche ameona suluhu kuu ni kuvamia mgodi?
hapo ndipo harakati zao zote zinapooneka si kitu
UPUUZI HUU
Hujamwelewa wewe Lumumba, serikali si inadai kuwa hawana leseni na hawajasajiriwa?? Maanake hawa ni wezi na wanatakiwa wakamatwe?? Akili za Lumumba bwana
 
Back
Top Bottom