Heparin
JF-Expert Member
- Sep 24, 2021
- 440
- 3,211
Kwenye YouTube Channel, kila unapopata hits YouTube inakulipa pesa. Wakafungua YouTube acc ya chama, ina followers laki 4 kumbe ana imiliki yeye na kijana mmoja. Kila wiki wanalipwa zaidi ya Tsh. Milioni 3. Tumeyakuta hayo ofisini.
Unamiliki YouTube channel ya chama, unalipwa wewe, leo tumekata mirija ya ufisadi unaanza kupiga kelele huko? Na waende wanako enda. Hatuwezi kuwa na chama cha aina hii.
Wamechukua YouTube channel yetu wamekimbia nayo, wamechukua acc ya X wamekimbia nayo kwa kisingizio kwamba walitumia credentials zao kufungua acc hizo. Wameamua kuungana na dola, tutashughulika nao.
John Heche
Mei 16, 2025 kwenye Uzinduzi wa CHADEMA Family, Kata ya Bulyanhulu, Jimbo la Msalala, Chadema Familia ina wanachama hai 250.
Pia soma CHADEMA: Akaunti zetu za chama za YouTube na X (Twitter) zimedukuliwa
Majibu ya John Mrema - John Mrema: Madai ya kuwa nimekimbia na YouTube na X za CHADEMA si kweli, sikuwa hata na Password ya hiyo Mitandao