FRANC THE GREAT
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 5,416
- 7,828
Habari!
Serikali ya Marekani chini ya rais Donald Trump imemshitaki mshauri mkuu wa zamani wa usalama wa taifa, John Bolton, ili kuzuia kuchapishwa kwa kitabu chake kipya kinachohusu wakati wake alipokuwa katika ikulu ya White House.
John Bolton.
Kitabu hicho kilichopewa jina "The Room Where It Happened", kilipangwa kutolewa mnamo 23 Juni lakini kulingana na malalamiko ya kesi hiyo, kitabu hicho kina "taarifa za kiusalama".
Kesi hiyo inafuatia siku moja baada ya Rais Donald Trump kusema kuwa Bolton atakuwa akivunja sheria ikiwa kitabu hicho kitachapishwa.
Kwa mujibu wa Baraza la Usalama la Kitaifa la ikulu ya White House (NSC), kitabu hicho kina vifungu kadhaa ambavyo vina taarifa nyeti za kiusalama za taifa.
Kuchapishwa kwa kitabu hicho "kunaweza kusababisha madhara yasiyoweza kutabirika, kwa sababu kuwekwa wazi kwa taarifa za kiusalama zilizomo ndani ya kitabu hicho kunaweza kuleta uharibifu mkubwa kwa usalama wa kitaifa", kulingana na shitaka.
Charles Cooper ambaye ni wakili wa Bolton amesema kuwa "wanafuatilia kwa ukaribu" kesi hiyo na majibu yatatolewa hapo baadaye.
[Reuters]