John Bolton, Mshauri wa Trump kwenye masuala ya usalama adakwa na ujumbe huu "5,000 Troops to Colombia"

Hahahaha, je ile mustache wa Mwl nyerere na Mzee Mugabe vipi?

Sent using Jamii Forums mobile app
IMG-20170930-WA0078 (1).jpg
Huu alikuwa anauchongea tu mwenyewe! Ila akiziachia angeweza kabisa Kuchonga O
 
Naona Bado muendelezo wa vita baridi tu kiuhalisia kati ya Russia,China na USA. Kitendo cha China na Russia kutangaza wazi kumuunga mkono Maduro hakiipi nafasi ya USA kupiga hatua zaidi kuingilia mgogoro huu.

Inanikumbusha kipindi ambacho serikali ya marekani ilipoishutumu Syria juu ya matumizi ya silaha za kikemikali na kuitishia kuivamia kwa kuwa inaua raia wema wasio na hatua,

Putin aliamua kutoka hadharani na kuiunga mkono serikali ya Al Assad na kila kitu kiliishia pale na Obama alirudi nyuma hatua kadhaa.

Jicho la tatu naona Maduro akiendelea kutawala kipindi kingine tena na hawa super power countries wataishia kwenye vita baridi tu hakuna atayefanya uvamizi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Saudi Arabia nafikiri ni strategic ally wa Marekani hasa pale wanapotaka ku manipulate oil price ili kuwadhuru maadui wa marekani kama Russia,Iran n.k.pia Saudia has much to do with oil price ili ku satabilise US Dollar.Ndio maana wanaona is much better kumlea Saudia hata kama amewakosea.
Exactly the point, plus ile ni sehemu Strategic sana kiusalama: Ukimvuruga Suadi Arabia lazima yamtokee puani maana hatakuwa na kiboko cha kumpigia Mrusi tena. OPEC ni habari nyingine ndugu yangu, kama unakumbuka vizuri miaka ya 1970's Carlos The Jackal alitumiwa sana na KGB kutaka kuwavuruga OPEC hadi kuna kipindi walivamia mkutano na kuteka baadhi ya Mawaziri.

Marekani angetumia ubabe kucheza na Saudi Arabia basi lazima ingekula kwake. Sema Henry Kissinger alikuwa na akili nyingi mno akaamua kuwatenge waarabu na Mrusi. Lakini nguvu ya kimkakati ya Saudi Arabia ni kubwa sana, Urusi na ubabe wake wote anacheza kwa makini na Marekani anacheza kwa makini.
 
Daaah aiseeh kumbe,Unajua kwenye maisha ili u survive kuna muda unabidi uwe mnafiki sana tu ikibidi.ndo wanafanya hawa Marekani na Urusi.Haya manchi makubwa yanajuana vizuri sana kila mmoja anacheza kwa step.
 
Mradi Russia ipo pale Maduro atabaki kama ilivyokuwa kwa Assad wa Syria
Siyo rahisi Mrusi kucheza na Marekani kule Amerika Kusini kama anavyocheza kule Syria: Mashariki ya kati ni rahisi sana kwasababu ana washirika wenye nguvu kama Hezbollah na Iran, pia makundi yaloyokuwa yanapigana Syria yalikuwa na ajenda binafsi. Kule America ya Kusini Venezuela ana mpaka wa kilomita kama 2000 na nchi ya Colombia ambapo Marekani anatishia kupeleka vikosi.

Kama Urusi atacheza na Venezuela kama anavyofanya kule Syria basi kule Ulaya Mashariki hakutatulia kabisa na yeye analijua hilo. Vikosi vya NATO viko mlangoni kwake hivyo atacheza vizuri.

Wamarekani wajanja sana wanajua kabisa ukweli kwamba, nikicheza nje ya Urusi lazima kwangu kutakuwa vibaya. Vivyo hivyo kwa upande wa Mrusi....

Kama Urusi atacheza kule The Western Hemisphere kama anavyofanya Syria basi Marekani atakuwa ameishiwa na nguvu sana: Kitu ambacho sidhani kama ndiyo hali ilivyo.
 
Nchi yenu ikijaaliwa Oil na Gas ni "Curse", USA, EU na washirika wake watakutafutia visa vya kila aina ili wawe wanai-control wao, shetani kabisa hawa...
Sio kweli mkuu, mfno sasaiv wazungu waseme tunamtoa M7 kwa vyovyote vile mtasema ni mafuta.
 
Back
Top Bottom