kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 9,000
- 17,909
Jarida la National Interest: Huenda John Bolton akatimuliwa na Trump
Mei 15, 2019 14:20 UTC
Jarida moja la nchini Marekani limeandika kuwa, huenda John Bolton, Mshauri wa Usalama wa Taifa wa nchi hiyo akapigwa kalamu nyekundu.
Jarida la The National Interest limewanukuu viongozi wawili wa Marekani wakisema kuwa, hatua ya kupenda makuu ya John Bolton, Mshauri wa Usalama wa Taifa wa nchi hiyo hasa kutokana na njama zake chafu zilizofeli dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Venezuela na Korea Kaskazini, imemuweka katika safu ya watu ambao huenda wakatimuliwa kutoka White House.
Likimnukuu afisa mmoja wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani jarida hilo limeandika kuwa, kwa sasa Mike Pompeo, Waziri wa Mambo ya Nje anafanya jitihada kubwa zenye lengo la kulinda nafasi yake, lakini Bolton ni mwenye kuchukiwa na wizara hiyo kutokana na kupenda kwake sana uchochezi.
Hayo yanajiri katika hali ambayo siku chache zilizopita, gazeti la Washington Post liliripoti kwamba, Rais Donald Trump wa nchi hiyo ana wasi wasi mkubwa kutokana na hatua za uingiliaji za John Bolton katika masuala ya ndani ya Venezuela ambapo alisema kuwa, Mshauri huyo wa Usalama wa Taifa anaisukuma Marekani kuelekea katika vita na nchi hiyo ya Amerika ya Latini.
Aidha baadhi ya vyombo vya habari nchi Marekani vimewanukuu maafisa wa kitengo cha ushauri ndani ya ikulu ya White House wakisema kuwa, Trump anaonekana kutofurahishwa na stratijia za Bolton kuhusu Venezuela. Ama kuhusiana na tofauti iliopo kati ya timu ya Trump juu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, baadhi ya weledi wa masuala ya kisiasa wanaamini kwamba, licha ya kuwepo timu yenye siasa kali na yenye chuki ya hali ya juu dhidi ya Iran katika uga wa siasa za kigeni za Marekani ikiongozwa na John Bolton mwenye kupenda kujitanua, lakini binafsi Trump hana nia ya kuingia vitani na Iran ya Kiislamu.
Tags
MAREKANI