Johannes Rebmann: Mtu aliyegundua mlima Kilimanjaro

Ni maajabu sana. Kulingana na machapisho mbalimbali mlima maarufu unaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 3 million iliyopita hakuna mkazi yeyote wa aliwahi kujua kuna mlima mrefu kaskazini mwa Tanganyika hata wale wakazi wenyewe hawakujua 😁.

Johannes Rebmann.

Mlima Kilimanjaro uligunduliwa na bwana Johannes rebmann ambaye alikuwa mmissionary kutoka Ujerumani mnamo 1848.

Kutokana na bwana huyo aliyekuwa na mwenzake aitwaye Johann Lidwig Krapf, habari ziliweza kusambaa maeneo mengi ya ulaya kuwa kuna mlima wenye kilele cha barafu karibu sana na ikweta. Lakini habari hizo hazikuaminika kwa watu mpaka miaka kadhaa baadae.
Mlima ulikuwepo na watu walikuwepo. Si sahihi kusema Rehbman aligundua mlima Kilimanjaro labda tuseme ni foreigner wa kwanza kuuona mlima kilimanjaro. Hizo ndiyo shortcomings za historia yetu. Utasikia Speke kagundua hiki, Livingstone kagundua kile wakati kulikuwa na wenyeji toka enzi. There is a need to rewrite our history
 
Nyie mmeshindwa kuelewa sio kwamba yeye ndo wakwanza kuona n kwamba n mzungu wakwanza kugundua n mzungu wakwanza kupanda
 
Ni maajabu sana. Kulingana na machapisho mbalimbali mlima maarufu unaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 3 million iliyopita hakuna mkazi yeyote wa aliwahi kujua kuna mlima mrefu kaskazini mwa Tanganyika hata wale wakazi wenyewe hawakujua 😁.

Johannes Rebmann.

Mlima Kilimanjaro uligunduliwa na bwana Johannes rebmann ambaye alikuwa mmissionary kutoka Ujerumani mnamo 1848.

Kutokana na bwana huyo aliyekuwa na mwenzake aitwaye Johann Lidwig Krapf, habari ziliweza kusambaa maeneo mengi ya ulaya kuwa kuna mlima wenye kilele cha barafu karibu sana na ikweta. Lakini habari hizo hazikuaminika kwa watu mpaka miaka kadhaa baadae.
Aibu kubwa sana. Upo umuhimu wa kuandaa vitabu vya historia viendane na uhalisia ulioopo. Hii habari walisoma mababu zetu kwa kutumia vitabu vya mzungu, haiwezekani tuendelee nayo. Kama watoto wanasoma hivi, itakuwa wanapotoshwa
 
hizi njemba zilituona wakuja sana unagunduaje na wenyeji wapo hapo wanaokota mpaka kuni za mlima au walipo fika ndio volcano ililipuka kuunda mlima mrefu history inaweza fanya uchukia hizi people nyeupe
 
Mlima ulikuwepo na watu walikuwepo. Si sahihi kusema Rehbman aligundua mlima Kilimanjaro labda tuseme ni foreigner wa kwanza kuuona mlima kilimanjaro. Hizo ndiyo shortcomings za historia yetu. Utasikia Speke kagundua hiki, Livingstone kagundua kile wakati kulikuwa na wenyeji toka enzi. There is a need to rewrite our history
Hili la kusema ndiye aliygundua mlima mbona ni waafrika wenyewe ndiyo wanajichanganya na kusema? Ukisoma kwenye machapisho ya watu wa Ulaya, wao wameeleza kuwa ni mtu wa Europe wa kwanza kuugundua. Ila waafrika ndiyo waliamua kuwafundisha watoto wao kuwa alikuwa mzungu. Kosa la nani?
 
Mabeberu kutoka Wikipedia wanasema hivi.
Johannes Rebmann (January 16, 1820 – October 4, 1876) was a German missionary, linguist, and explorer credited with feats including being the first European, along with his colleague Johann Ludwig Krapf, to enter Africa from the Indian Ocean coast

. In addition, he was the first European to find Kilimanjaro.[1] News of Rebmann's discovery was published in the Church Missionary Intelligencer in May 1849

Hii mada yako reference yako sijui wapi inayodai kuwa yeye ndie aliegundua mlima Kilimanjaro.
Mabeberu wa Wikipedia ni hao hapa:
626px-Daruser_2017_Editathon_-_Hapa_kazi_tu.jpg

(Dar es Salaam editathon Daruser group at Buni Innovation Hub July 2017)
 
kwahiyo mlima haukuwepo kabla ya yeye kugundua?
Swali lako si kichekesho. Kugundua ni kazi ya kiakili. Kwa hiyo, kitu kinaweza kuwepo miaka mingi lakini hakikutambuliwa bado na akili. Basi hakikugunduliwa.
Vitu vingi hugunduliwa upya kila siku; maana kila mtoto anaanza kugundua ulimwengu polepole kadri anavyokua.
Kwa jumla ni dhahiri Kilimanjaro iliwahi kutambuliwa na wenyeji muda mrefu. Rebmann aliigundua kwa utamaduni wake, kwa sababu aliandika taarifa juu yake.
Hii lugha yote ya "ugunduzi" inatumiwa mara nyingi bila kutafakari.
 
Kwaiyo mlima ulikuwa umejificha hadi ukagunduliwa ? Kulikuwa hakuna watu wanaoishi uko hahahah wa africa bana kwa kulishwa matango
 
Huo mlima uligunduliwa na Wachagga kabla babu yake Renmann hajazaliwa.
Ni maajabu sana. Kulingana na machapisho mbalimbali mlima maarufu unaokadiriwa kuwa na umri wa miaka 3 million iliyopita hakuna mkazi yeyote wa aliwahi kujua kuna mlima mrefu kaskazini mwa Tanganyika hata wale wakazi wenyewe hawakujua 😁.

Johannes Rebmann.

Mlima Kilimanjaro uligunduliwa na bwana Johannes rebmann ambaye alikuwa mmissionary kutoka Ujerumani mnamo 1848.

Kutokana na bwana huyo aliyekuwa na mwenzake aitwaye Johann Lidwig Krapf, habari ziliweza kusambaa maeneo mengi ya ulaya kuwa kuna mlima wenye kilele cha barafu karibu sana na ikweta. Lakini habari hizo hazikuaminika kwa watu mpaka miaka kadhaa baadae.
 
Yaani wenyewe Wachaga hawakuwa na macho, mxiiiiuuu, wamegundua wkt watu wapo hapo hapo.
Wachaga hawakujua kuwa ni mlima ndio maana walishindwa kuutangaza na hata umaarufu ulionao mlima huu leo ni kutokana na ugunduzi huu. Wachagga wa zamani waliamini ilikuwa ni Mungu wao anaowaletea mvua , riziki kuwaondolea mabalaa na mahonjwa akiamka asubuhi lazima.auangalie kwanza. Hivyo kwa mchagga wa kale haukuwa mlima
 
Wao hawakuita mlima waliita Mungu, hao wazungu wakaleta jina la mlima.Sasa acha tuendelee kuita Mungu tuu
 
Nchi hii ina vilaza wengi. Ona ambavyo wanashindwa kutofautisha tusentensi tudogo hivi.

".. mzungu wa kwanza.." VS "... binadamu wa kwanza.. "
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom