Joash Onyango Ajiunga na Kenya Police FC, Umri Wake Wazua Mjadala

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,132
Reaction score
10,514
Beki mkongwe mwenye jina kubwa katika soka la Afrika Mashariki, Joash Onyango, amezua gumzo mara baada ya kujiunga rasmi na kikosi cha Kenya Police FC akitokea timu ya Dodoma Jiji ya Tanzania. Onyango, ambaye amewahi kung’ara na miamba wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba SC na Singida Black Stars, anatajwa kuwa na umri wa miaka 26, ingawa mitandaoni mashabiki wanazidi kufanya utani wakidai ana umri wake ni miaka 62.
1756617253646.jpg

Onyango mwenye miaka 26 anasifika kwa kuwa mchezaji mwenye nguvu, uzoefu mkubwa wa kimataifa na nidhamu ya kipekee katika safu ya ulinzi. Katika misimu aliyocheza nchini Tanzania, alijijengea sifa ya kuwa beki asiyeogopa changamoto, akiwazuia washambuliaji hatari na mara nyingi akitoa uongozi ndani ya uwanja.
1756617251738.jpg

Ujio wake ndani ya Kenya Police FC unatarajiwa kuimarisha safu ya ulinzi ya kikosi hicho kinachopania kupigania nafasi za juu katika Ligi Kuu ya Kenya. Mashabiki wengi wa Polisi wamesema hatua hii ni “saini ya kipekee” itakayoleta uthabiti na uzoefu kwa vijana waliopo.
 
View attachment 3459565
Onyango mwenye miaka 26 anasifika kwa kuwa mchezaji mwenye nguvu, uzoefu mkubwa wa kimataifa na nidhamu ya kipekee katika safu ya ulinzi. Katika misimu aliyocheza nchini Tanzania, alijijengea sifa ya kuwa beki asiyeogopa changamoto, akiwazuia washambuliaji hatari na mara nyingi akitoa uongozi ndani ya uwanja.
View attachment 3459566
Ujio wake ndani ya Kenya Police FC unatarajiwa kuimarisha safu ya ulinzi ya kikosi hicho kinachopania kupigania nafasi za juu katika Ligi Kuu ya Kenya. Mashabiki wengi wa Polisi wamesema hatua hii ni “saini ya kipekee” itakayoleta uthabiti na uzoefu kwa vijana waliopo.
Huyu umri wake huwa hauongezeki? Maana alijiunga Simba SC mwaka 2020 akiwa na miaka 27 iliyotajwa na ikazua mshangao kwa muonekano wake. Leo hii 2025 iwe umri wa miaka 26?? Duuh!!
 
Back
Top Bottom