JKT na Uzalendo; Uzalendo kwa Nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JKT na Uzalendo; Uzalendo kwa Nani?

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by Nyota Ndogo, Sep 1, 2011.

 1. Nyota Ndogo

  Nyota Ndogo Senior Member

  #1
  Sep 1, 2011
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 152
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kuna mazungumzo mengi kuhusu kurejeshwa kwa mafunzo ya JKT na mara nyingi yamekuwa yakipigiwa debe na Television ya Chama Cha Mapinduzi kila uchao.

  ukiwasikiliza watetezi wa hoja ya kurejea kwa JKT na wanapropaganda wengi wengine wanajenga hoja kwamba vijana wengi wamekosa uzalendo. kwamba vijana wengi si wabunifu tena na wanashinda vijiweni.

  wana hoja. labda. ni kweli kwamba vijana wengi sasa wa vijijini na mijini wanashinda vijiweni. mbaya zaidi hata wale walio vijijini wanadanganyika kuwa neema iko mijini na matokeo yake wimbi kubwa la vijana kukimbilia mijini linazidi kuongezeka kila leo. lakini tusisahau kuwa kwa wale walioko vijijini wanayasikia maneno ya wakuu wa nchi...kwamba serikali haiwezi kuiamuru mvua inyeshe. kwa hiyo wale wenzangu na mimi walioko shamba wanaoamini katika kilimo imekula kwao. inabidi waje mijini. kwa hawa wa mijini na hasa waliopita skuli wao waliambiwa wataandaliwa ajira milioni moja. sijui ni wangapi hata sasa wana hizo ajira? nani atuthibitishie?

  kinachonishangaza hapa ni hii dhana kwamba vijana wamekosa uzalendo. najiuliza kivipi? kwani uzalendo ni nini?

  kwa mujibu wa kamusi yangu hapa, uzalendo ni ile tabia au hali ya mtu kuiunga mkono nchi yake kwa moyo na nguvu zake zote kiasi cha kuwa tayari kuitetea.

  Maswali:

  1. wanaotuhumiwa kwa rushwa kubwa kubwa kama kagoda, dowans, na richmond? ni vijana? hawakupita jkt?
  2. wanaotuhumiwa kusafirisha wanyamapori kwenye ndege ni vijana? hawakupita jkt?
  3. wanaotuhumiwa kuuza dawa za kulevya leo ni vijana? hawakupita jkt?
  4. wanaolalamikiwa kuiingiza nchi katika mikataba mibovu ya madini ni vijana? hawakupita jkt?
  kuna maswali mengi ya kujiuliza, lakini tuanze na hayo manne.

  kwamba vijana sasa tunalaumiwa na hawa wazee waliopita jkt kwamba hatuna uzalendo, wakati wenyewe hawana hata harufu ya uzalendo.

  why?

  Nadhani ni siasa. Kwamba vijana tumechoka na kauli-mbiu za kila mwaka, miaka 50 baada ya uhuru bado tunaishi kwa kaulimbiu zisizokuwa na msaada kwetu.


  Matokeo ya uchaguzi uliopita pia ni moja ya vichochezi vya suala hili kupigiwa debe. kwamba vijana wengi wameongoka kifikira. na kwa vitendo walikipinga waziwazi chama cha mapinduzi katika uchaguzi uliopita. na sasa ili kuwadhibiti vijana, ccm sasa wanakuja na mavi ya kale. ati JKT. kwamba wakawajaze vijana na fikra mgando za ccm.

  Too late:

  it will never work. kwa waliosoma physics wanajua Hooke's Law. Elastic material ikishavuka elasticity, basi inakuwa inaingia katika region tofauti kabisa inayoitwa deformation ambako huwa haiwezi tena kurejea katika original shape.

  Vijana tumeshavuka Elastic Limit. Tuko kwenye Deformation point.

  Kama motives za kurejea kwa JKT una lengo la kutujengea uzalendo kwa CCM....waanzilishi wa mpango huo mmefulia na hautafanikiwa. Kwa mara nyengine tena mmemshauri vibaya mkuu wa kaya.

  Vinginenyo mtuambie............

  kwa wizi huu, kwa rushwa hizi na hujuma hizi zinazofanywa na wazee walioko serikalini na waliopita JKT miaka hiyo, manataka kutufundisha uzalendo, nauliza hivi..........


  Uzalendo kwa Nani?
   
 2. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #2
  Sep 2, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Mkuu uko sahihi kabisa! ni dalili/matokeo ya watu wanaotapatapa eti kuhamasisha kurudishwa jkt kwa kigezo cha uzalendo miongoni mwa vjana
   
 3. Halfcaste

  Halfcaste JF-Expert Member

  #3
  Sep 2, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 973
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Mkuu big up,

  Hivi wewe na mimi tuna share ubongo,swala hili nimekuwa nikilifafanua kwa watu wengi tangu mwezi wa sita 2011, hata wik ilopita. JKT has nothing to do in imparting the so called "uzalendo". Vijana tulioajiriwa hivi majuzi kazini,tunaitwa vijana dot com kwamba hatujui uzalendo, tunataka laptops, modems, magari wakati huo huo wazee wanaiba hela za serikali hapa Ofisini.Tunaambiwa hatujapita JKT kufundishwa ukakamavu, upuuuuuuzi mtupu!

  Msitudanganye sie vijana hatuna tatizo, tatizo ni ninyi Wazee mlotutangulia kwa kivuli cha JKT ukakamavu, na si JKT maadili ya Taifa na uzalendo.
   
 4. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #4
  Sep 2, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,011
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Hakika nakuambia JKT kwa mujibu wa sheria haiwezi kurudi.
   
 5. T

  Tata JF-Expert Member

  #5
  Sep 2, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,730
  Likes Received: 646
  Trophy Points: 280
  Mimi ni mmoja wa wale waliopitia JKT na hili suala la uzalendo bado huwa nashindwa kuelewa nini maana yake kwa muktadha wa wale wanaoshabikia kurejeshwa kwake. Sikuwahi hata siku moja kukalishwa chini kufundishwa somo lenye kichwa cha UZALENDO kwa muda wote niliokuwa jeshini na nina uhakika wengi wa maafande waliokuwa wasimamizi wetu walikuwa hawajui huyo mdudu anayeitwa UZALENDO anafananaje.

  Labda kama wanamaanisha ule utamaduni wa kijeshi wa kukubali kila anachosema mtu aliyekuzidi cheo (yaani afande) bila kuhoji wala kupinga. Nakumbuka tulifundishwa utamaduni wa kujibu NDIO AFANDE hata kwa mambo ya kipuuzi kabisa ambayo hata watu wasiokuwa na uelewa hawawezi kukubaliana nayo. Kwa ufupi utamaduni wa kijeshi unazuia watu kuhoji masuala yanayoathiri maisha yao na kugoma jeshini ni kosa kubwa sana la jinai. Utamaduni mwingine wa kipuuzi kabisa uliokuwa kwenye jeshi letu ni ule wa kupinga mabadiliko na kuendeleza mambo yaleyale (status quo) bila kuhoji mantiki ya mambo yaliyopo. Ndio maana kwata ya kijeshi imebaki ileile miaka yote bila mabadiliko yoyote tangu kuundwa kwa utaratibu wa kijeshi wakati wa vita ya kwanza ya dunia.

  Wahubiri wa kurudushwa kwa JKT wanatishwa na kizazi cha vijana wa sasa ambacho hakijaathiriwa na huu utamaduni wa kijinga wa NDIO AFANDE. Utamaduni huu kwa kiasi kikubwa umechangia jamii yetu ya wasomi kuwa ama washiriki au mashuhuda wa ufisadi unaofanywa na wakubwa zao kazini (maafande) bila kuwa na ujasiri wa kuhoji wala kubadilisha hali. Wanajua kizazi hiki zhha sasa kina uwezo mkubwa wa kubadilisha muelekeo wa jamii nzima na kwamba mabadiliko ya kweli yakitokea wao hawatakuwa salama tena.
   
 6. H

  HEMA Member

  #6
  Sep 2, 2011
  Joined: Oct 13, 2010
  Messages: 17
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  JKT inatakiwa kutumika kuzalisha raslimali mfano kilimo na ujenzi wa miundombinu, na inatakiwa walipwe kama posho kila mwezi kwa ajili ya kujikimu. Issue sio uzalendo ni kutenegeneza ajira kwa vijana na kuongeza uzalishaji. Ni kweli wengi waliopita JKT ndio mafisadi.
   
 7. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #7
  Sep 2, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hakuna haja ya JKT kwa sababu hata wanajeshi walioko si wazalendo kabisa. Haiwezekani wahindi, wachina, waarabu na wazungu wanavuna rasilimali wao wanaangalia tu, uzalendo gani juzi wafanyabiashara wamegoma kuuza mafuta kwa sababu serikali imetoa kodi kwa wananchi wake? huu ni usaliti wa hali ya juu.

  Hakuana cha JKT wala jeshi haiwezekani hata kidogo wageni wanakuja na kupiga hela hapa sisi tunafundishana uzalendo wa ka kazi gani.

  hii ni njama ya watu/kikundi funa kwa mgongo wa JKT kupiga hela kama ilivyo kwa kilimo kwanza.

  Haiwezekani, nimempigia mbunge wangu simu na kama hii ikipita basi naenda kumpinga jimboni kwa nguvu zote.
   
 8. Hassani

  Hassani JF-Expert Member

  #8
  Sep 2, 2011
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 267
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Kama ukipitia jeshini unakuwa mzalendo basi maofisa wa JWTZ wasingejilimbikizia mali kwa kuwaibia askari wadogo stahiki zao,Kama ukipitia jeshini unakuwa mzalendo basi police wakubwa wasingekuwa wanachukua rushwa toka kwa wafanyabiashara wakubwa wa magendo,askari wa JWTZ wasingekuwa wanajihusisha na ujambazi (refer tukio la ubungo mataa),askari magereza wasingekuwa wanachukua rushwa toka kwa wafungwa.
   
 9. Halfcaste

  Halfcaste JF-Expert Member

  #9
  Sep 2, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 973
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Wisely!!Kitu tunachohitaji hapa nikuandaa Syllabus inayoitwa ''Uzalendo na Maadili ya Mtanzania''kufundishwa kuanzia Primary hadi Verisity huku tukiweka vipengele hivo kwenye Katiba Mpya, Maadili na Miiko yetu kama Watanzania.Ukifisadi Katiba ieleze wazi huyo mtu nafanywaje,full stop!!
  Kwani Wachina,wamefikaje walipo.......????Otherwise nchi itabaki Mifupa,na mifupa hiyo itakwibwa tu!!
   
 10. Halfcaste

  Halfcaste JF-Expert Member

  #10
  Sep 2, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 973
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Bravo kwa mwanzisha topic,inawezekana isipate wachangiaji wengi hii tabia ya Watanzania kuchangia' topic pendwa' ambazo utamu wake ni wa muda tu.Topic ni nzuri kwani niyakuijenga Tanzania tunayotaka.
   
 11. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #11
  Sep 2, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,991
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Tatizo ni mfumo uliopo ni mbovu,achilia mbali JKT.
   
 12. nditolo

  nditolo JF-Expert Member

  #12
  Sep 2, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 1,335
  Likes Received: 300
  Trophy Points: 180
  Msekwa ni miongoni mwa watu ambao either walipitia jkt au walianzisha jkt, lowassa chenge, msabaha, mkono,mramba, lukuvi na wengine wengi ambao nikiwataja wote nitajaza ukurasa je ni wazalendo? hao ndo wezi wakubwa, wafanya mikataba feki hao ndio walio wamilikisha wageni mali za watanzania, wamewapa madaraka wageni akina manji, rostam yaani kifupi ndio waliotufikisha hapa tulipo. Staki hata kuwasikia.
   
 13. m

  mtolewa Senior Member

  #13
  Sep 2, 2011
  Joined: Jan 18, 2011
  Messages: 197
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  mbona JKT imeshaanziswa?JKT=JESHI LA KUIKOMBOA TANZANIA chini ya brigedia general K.E.Msemakweli na mimi nimepita kwenye usaili wa kujiunga na jeshi hilo intake ya pili.
   
 14. n

  nyantella JF-Expert Member

  #14
  Sep 2, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 890
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  ...wazee wanaiba pesa ofisini ili wawanunulie watoto wao mobile phones za bei mbaya, laptops, modems,magari, pesa za kunywea, za kuhonga....and the song goes on!!!. one thing huwa najiuliza hivi vijana wa tanzania hawatazeeka? au siku zimeganda?

  If you can, please suggest a better way ya kuunganisha vijana woote, wasomi, wasiosoma, watoto wa wakulima, watoto wa mafisadi, wakike na wa kiume waipende nchi yao na ndio utakua mwisho wa wizi na ufisadi. JKT iliweza kuwaunganisha vijana wote kwa wakati huo, je kwa mtazamo wako nini kifanyike kuwaunganisha vijana wa leo? maana kwa vyovyote vile, life goes on and nchi zote zina duniani zina vijana na wazee!!
   
 15. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #15
  Jan 10, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu mara nyingi huwa nikipiga story na Watu wazima wenye umri wa miaka 45 na kuendelea huwa wanasupport sana ishu ya kurejesha mafunzo ya JKT kwa vijana kwa hoja kwamba yanawajengea Ukakamavu, Uadilifu na Uzalendo.

  Binafsi nimekuwa nikiwapinga tena kwa hoja kwamba Ukakamavu, Uadilifu na Uzalendo ingawa vinawezwa vikachongwa na kuchomweka akili mwa Mwanadamu lakini huwezi kuvitenganisha na other inherence behaviors. Huwa hata nawatolea mifano ya Viongozi wetu wa Serikali yetu ya leo ambao sehemu yao kubwa ni wale waliopata mafunzo ya JKT ujanani (Mfano JK, Utouh, Luhanjo, Lowassa, Luhanjo, Jairo, Mramba, Yona, nk) na kuwauliza Je watu hao ni Wakakamavu, Waadilifu na Wazalendo leo hii?

  Siamini katika hoja ya kurudisha mafunzo ya JKT kwa Vijana kwa ajili ya kuwajengea Ukakamavu, Uadilifu na Uzalendo maana uzoefu tulionao leo hii ni kwamba Viongozi na Watendaji wa Serikali wa leo, wengi walipata mafunzo hayo lakini leo hii si Wakakamavu, Waadilifu wala Wazalendo tena. Badala yake wamekuwa Mabwenyenye, Wabadhirifu, Wabinafsi, Waongo na Wasaliti kwa Watanzania.
   
 16. F

  FUSO JF-Expert Member

  #16
  Jan 10, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,855
  Likes Received: 2,331
  Trophy Points: 280
  kaka yaani unaanza kumsema Rais wako ajaye wa 2015 mpaka 2025 kwamba ni legelege na si mzalendo (mdokozi) aka mwizi - sisi hatumo hili la kwako ndugu.

  mimi nilipita JKT mwaka mmoja (OP Multi -Party) pale Makutupora ndio maana sijawahi iba hata thumni ya umma, ni mwadilifu na mzalendo numberi one.
   
 17. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #17
  Jan 10, 2012
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,749
  Likes Received: 545
  Trophy Points: 280
  Hao uliowataja ni exceptional to the general rule.
   
 18. B

  Baba Collins JF-Expert Member

  #18
  Jan 10, 2012
  Joined: Sep 24, 2011
  Messages: 498
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Naunga mkomo hoja,tutaongeza majambazi na wala si ukakamavu na uzalendo.
   
 19. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #19
  Jan 10, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ungetutajia kwa majina (Japo kwa uchache) hao ambao siyo exceptional to the general rule Mkuu ili tuwachambue na kuona kama kweli JKT iliwajengea Ukakamavu, Uadilifu na Uzalendo!

   
 20. D

  Dawa ya Mjinga JF-Expert Member

  #20
  Jan 10, 2012
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 382
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mimi simo na ninanawa kabisa mikono yangu ili damu yenu mnaotaka kirejesha JKT ya mujibu wa sheria, isidaiwe kesho ahera mikononi mwangu. JKT ni Jeshi la Kuhujumu Uchumi. Kama kujenga limetujengea taifa la wezi. Kama wengine wanadai kuwa ni waadilifu kwa ajili ya JKT, ni mafunzo yapi ya JKT ambayo yamewajengea huo uaminifu?
  Ukweli usiopingika, hakuna (narudia) hakuna aliyepita JKT bila kuwe mdokozi na au mwizi kabisa. Ukibisha, tueleze, ulifanyaje pale ulipoamka asubuhi ukakuta kombati yako imetambaa na asubuhi hiyo kuna ukaguzi?
  Hayo tisa, kumi tujue kuwa kizazi cha sasa si cha kale. Mnajionea wenyewe vijana wanavyofanya migomo kila uchao vyuoni. Kwa sasa unawamudu kirahisi hata kwa kuwaruhusu kufanya maandamano kwani baada ya siku moja tu wamechoka. Sasa mnaenda kuwapa ukakamavu na kuwafundisha matumizi ya silaha za kivita. Mimi simo. Damu yenu na iwe juu ya vichwa vyenu wenyewe.

  Kama kuna hela ya kuchezea huko JKT bora ipelekwe bodi ya mikopo ya Elimu ya Juu, vijana hao wasome bila purukushani zisizo za lazima. Pia wako vijana ambao wako tayari kujitolea huko JKT, kwanini kuwataka hawa wa lazima? Mwisho JKT ilivyokithiri unyanyasaji wa kijinsia, janga la kihitoria litatokea kwenye maambukizi ya gonjwa la kisasa la ukimwi. Mwenye masikio na asikie ukweli huu.
   
Loading...