JKCI yapata mtambo wa kisasa utakaopima 95% maradhi ya moyo

esther mashiker

JF-Expert Member
May 29, 2018
616
552
1114238


TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imepokea msaada wa mashine ya kisasa yenye uwezo wa kupima hadi asilimia 95 ya maradhi yote ya moyo. Mashine hiyo inayofahamika kwa jina la Echo Cardiograph imetolewa na Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (SACH), Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya JKCI, Profesa Mohammed Janabi ameeleza.

Kwa mujibu wa Prof Janabi, mashine hiyo yenye thamani ya Sh. milioni 150, inahamishika na kurahisisha utoaji huduma wa vipimo hata nje ya Taasisi hiyo. Katika haa ya kupokea mashine hiyo jana Ijumaa, Profesa Janabi alisema,kati ya watoto milioni mbili wanaozaliwa kila mwaka, 14,000 hugundulika kuwa na matatizo mbalimbali ya moyo huku wengi wao wakipoteza maisha kutobainika mapema na kupatiwa matibabu. "Kwa sasa watoto 512 wako katika orodha kusubiri kufanyiwa upasuaji wa moyo.

Kifaa hiki kitatusaidia kugundua mapema tatizo la moyo kwa mtoto lakini pia kumpima mama mjamzito kugundua tatizo la moyo kwa mtoto aliye tumboni ili kama anatatizo hilo iwe rahisi kumshauri ajifungue kwa njia gani na pia kupanga matibabu kwa mtoto," alisema.

Viongozi wa Taasisi ya SACH kutoka Canada na wengine kutoka Israel wameitembelea JKCI kuona namna ambavyo madaktari wao wanafanya kazi ya kutoa mafunzo pamoja na kutoa msaada huo. Katika ujumbe huo pia wapo madaktari ambao watafanya matibabu kwa watoto wenye matatizo ya moyo ikiwa ni pamoja na kufanya upasuaji kwa watoto.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya JKCI, Profesa William Mahalu, alishukuru kwa kuwasaidia JKCI mashine hiyo na kuahidi ktoa ushirikiano kwani uhusiano wa Israel na Tanzania umewawezesha wataalamu wanaofanya upasuaji sasa JKCI kwa msaada wa Israel kupitia mafunzo wanayotoa.
 
Hela ya kurudia uchaguzi kwenye kata moja tu kuchagua diwani ingetosha kununua hicho kifaa ila tunasubiri misaada!!

No wonder wanaenda kutibiwa ulaya ila huwa najiuliza huwa wanajisikiaje kurudi kama mizigo ila hali walisafiri wakiwa ni abiria wa daraja la business class!!
 
Hela ya kurudia uchaguzi kwenye kata moja tu kuchagua diwani ingetosha kununua hicho kifaa ila tunasubiri misaada!!

No wonder wanaenda kutibiwa ulaya ila huwa najiuliza huwa wanajisikiaje kurudi kama mizigo ila hali walisafiri wakiwa ni abiria wa daraja la business class!!
Kupewa bure , lakini vipimo bei juu
 
Tunashukuru kwa huo msaada wa Echo Machine kutoka kwa hao waisraeli ....ila mtoa mada huo sio mtambo ni mashine ya kawaida sana...kwani hapa Tanzania zipo hivyo usikuze mambo.
Mwenye education background ya Janabi naomba atusaidie jukwaani kama hatajali.
 
Kwa hiyo aina ya tatizo la moyo lina influence ni njia gani mama atumie wakati wa kujifungua sio....aiseee Mungu atusaidie sana na aina hii ya Maprofesa ...itakua amenukuliwa vibaya
 
Jakaya Kikwete alikuwa na lengo zuri sana na nchi hii hawa wachunga ng'ombe wanatupeleka kuzimu.
 
Watakuwa wanekosea thamani ya hiyo mashine kama bei ni hiyo tulipaswa kuwanayo kila hospitali hapa nchini.
 
Mashine kutoka "izrael" !

Kuna majeruhi alikataa kupakizwa kwenye ambulance ya msalaba mwekundu, sasa kwa hii mashine ndugu zetu waislam wanasemaje
 
Tunashukuru kwa huo msaada wa Echo Machine kutoka kwa hao waisraeli ....ila mtoa mada huo sio mtambo ni mashine ya kawaida sana...kwani hapa Tanzania zipo hivyo usikuze mambo....
Mwenye education background ya Janabi naomba atusaidie jukwaani kama hatajali....

Yoote sawa ila hapo kwenye education back ground ya Dr Janabi wewe elimu yako ni sawa na chekechea kwake
 
Back
Top Bottom