JK: Vyombo vya Habari visaidie kutibu majeraha ya Uchaguzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK: Vyombo vya Habari visaidie kutibu majeraha ya Uchaguzi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Nicky82, Nov 6, 2010.

 1. Nicky82

  Nicky82 JF-Expert Member

  #1
  Nov 6, 2010
  Joined: Mar 14, 2009
  Messages: 939
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wakuu,
  Nimemsikia JK akitoa kauli hii jana wakati akihutubia kwenye hafla ya kutangazwa pale Karimjee na leo kwenye sherehe ya kuapishwa pale uwanja wa uhuru.

  Na kuna mahali kwenye hotuba ya leo amesema ziko hoja za kidini zilizotolewa majukwaani na wanasiasa ambazo zimeleta mpasuko hivyo akavisihi vyombo vya habari visaidie kutibu majeraha na mpasuko huo.

  Wote tunakumbuka hizi hoja kuhusu udini na ukabila zilishikiwa bango na kufanywa mtaji wa ccm majukwaani. Sasa hii ina maana JK anakiri ule ulikuwa ni mkakati wa kampeni au na je vyombo vya habari vitawezaje kuziba ufa huu,

  Nawakilisha
  .
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Nov 6, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Mimi mpaka leo sijakielewa vizuri hicho kinachoitwa udini hasa kipo wapi!
  Uduni ninaoweza kusema kama mfano ni waraka ulioletwa hapa jamvini unaowataka watu wa dini fulani wachague viongozi wa dini fulani..basi
  Otherwise sijaona shida hiyo kuwa ni kubwa sana katika jamii ya kitanzania, ila inatumiwa tu na baadhi ya watu kujitafutia umaarufu majukwaani!
   
 3. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #3
  Nov 6, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,604
  Likes Received: 4,730
  Trophy Points: 280
  Majeraha yamesababishwa na yeye mwenyewe Kikwete, alifanya hivyo 2005 kuwajeruhi wana CCM wenzake, na mwaka huu kazitumia kumjeruhi Dr Slaa, sasa analoloma nini ? Huyu mtu ni mnafiki na elements zote za udikteta. Lakini ajuwe kuwa kipindi hiki ni kigumu kwake sana kuliko wakati wowote katika maisha yake, amekiporomosha chama chake, ameibaka demokrasia ,amevuruga uchaguzi,ametoa ahadi zisizotekelezeka, afya anazidi kudorora, mieleka kwa sana huko ikulu na zaidi sana dhamira yake inamshitaki.
   
 4. laplap

  laplap Member

  #4
  Nov 6, 2010
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tusubiri aifanye kigoma kuwa dubai
   
 5. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #5
  Nov 6, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Ivi JK ana amani ya mwili na roho following the election results?
   
 6. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #6
  Nov 6, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45


  Majeraha kayaleta yeye, sasa anavipa vyombo vya habari kazi ya kutibu majeraha? ingekuwe vyema yeye kuyatibu kwa kukubali luwa kura zilichakachuliwa.
   
Loading...