Serikali ianzishe elimu ya uelewa wa mambo yaani Intellectual Education Certificate (IEC) kwa watu wote wanaoongea na vyombo vya habari

Pascal Ndege

JF-Expert Member
Nov 24, 2012
2,977
1,897
Katika Maisha ya sasa huwezi kujizuia kusikiliza vyombo vya habari. Endapo ukiwa na mishemhe za kawaida unaweza ukawa hospital au public transport basi utakutana na taarifa za habari na vipindi mbalimbli vya Radio au TV.
Zamani kabisa vyombo vya habari vilikuwa strict sana. Vipindi vingi vilirecordiwa na kupigwa baadae.

Baada ya mfumuko wa vyombo vya habari naamaanisha uwepo wa vyombo vingi vya habari. Ufuatliaji umekuwa mdogo sana.

Kwasasa serikali imekaa mkao wakujihami na vyombo vya habari hivi. Mtangazaji akiikosea serikali au kutukana anachukuliwa hatua Mara Moja.

Vyombo vingi vya habari viliwahi kufungiwa na kupewa faini kulipa na maonyo makali. Yote hayo serikali imefanikiwa sana sana.

Kuna angle flani Mimi naona vyombo vya habari vinafanya vibaya sana ni kwenye maswala ya taaluma.

Kuna siku nilikuwa kwenye mwendokasi mwandishi wa habari kutoka kwenye Radio Moja nikashangaa hajui muundo wa Bunge la Tanzania. Kibaya zaidi anapotosha bila kujali anasikilizwa na mamillioni ya watu.

Waandishi wengine hawajui muundo wa mataifa mbalimbali, Siasa za nchi nyingine, history, biology na mambo mbali mbali.

Lakini cha kushangaza waandishi pamoja na wageni wao studio wamekuwa wakiongea vitu vya ajabu bila wasiwasi na bila kuchuliwa hatua yoyote.

Si hao tu hata wanasiasa kwenye majukwaa na bungeni wamekuwa wakiongea vitu ambavyo walipaswa kuvijua lakini hawakijui.

Mimi napendekeza kuwepo na certificate ya uwelewa wa mambo. Ukitaka kuingia kwenye kazi ambayo itakukutanisha na vyombo vya habari basi lazima uwe na hiki cheti.

Muundo wa hii elimu kuwepo na maswali ya kuchagua kama 2000 katika lugha ya kiswahili ambapo mtahiniwa atapambana kuifanya hiyo mtihani akifaulu ndio atapata nafasi ya kuongea na vyombo vya habari.

Hii itasaidia uelewa wa mambo. Kwahiyo kama mwandishi wa habari atakosea basi cheti chake kitafutwa na kulazimika kufanya mitihani tena.
 
Ni kweli kabisa. Majuzi nilimsikia kiongozi wa ccm huko mwanza akisema "acha waarabu waje tuoe mabinti zao"!
Yaani akili ni tope hadi utosini!
 
Back
Top Bottom