JK; Nimekubali Kuwa Ben Mkapa Ni Simba Ingawa Hangurumi!

Mi sioni sababu ya kumuona mkapa lulu wakati ana kashifa kibao,mara meremeta,mara kiwila,mara EPA,wanini huyo?hupaswi kumwamini mwongo hata kama ameongea ukweli,mwizi ni mwizi tu hata kama ameiba buku,hatupaswi hum judge in positive way unles arudishe alichotuibia na akaungame kwa imani yake...mp'ya
 
yaani ndani ya ccm hakuna anayeweza kuongoza zaidi ya Mkapa? Basi ccm kwishney. Nalog off
 
lakini pamoja na udhaifu wake uncle ben ni kichwa bwana, aliweza kabisa kwa muda mfupi kuuweka uchumi wa JMT kwenye mstari. Kama isingekuwa hawa wahuni tulionao hivi sasa kwenye madaraka hivi sasa JMT tungekuwa tunaongoza kwa uchumi mzuri EAC. Huyu JK ni sawa na ule usemi wa mtoto akililia wembe mpe.

usihalalishe!hakuchaguliwa kuwa raic ili aanzishe ANBEN
 
Nilishawahi kusema huyu mk.wer.e atakuja kumpigia magoti tu mzee Mkapa, sasa taratibu naona anarudi kwenye mstari, angekuwa anakili akakumbuka toka mwanzo mambo yasingekuwa kama ilivyosasa tatizo anashauriwa na watu kibao mwisho anashindwa kujua astick kwenye ushauri upi. Pole sana JK
 
Baada ya wanamtandao kumfitinisha Kikwete na Mzee Benjamin Mkapa mwaka 2005 huku wakipandikiza chuki dhidi ya Mkapa kwa madai kuwa alikuwa hamtaki Kikwete chuki ambazo zimewahi hata kuandikwa na magazeti nchini , ikiwa ni mwaka wa sita akiwa madarakani rais Jakaya Kikwete amewaambia wasaidizi wake Mkapa ni simba ingawa haungurumi kwa maana ya kutopenda kujionyeshajionyesha. Kubadili mtazamo kwa Kikwete dhidi ya Mkapa ndiyo kunaelezwa kuwa ndiyo kiini cha mzee Ben Mkapa kurejea kwa kasi kwenye ulingo wa siasa za kitaifa, na siyo hivyo tu lakini pia inaelezwa tayari Kikwete ameanza kuandaa mkakati wa kuhakikisha Mkapa anakuwa Mwenyekiti wa CCM kwa mara nyingine tena ili kumaliza makundi hasimu ndani ya chama hiko lakini pia ili kuivusha salama CCM kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Kikwete akimaliza muda wake anahama nchi hii!
 
......hapa penye red nimepapenda kwa sababu ndio ukweli na utasimama daima;
Jisome hapo penye rangi.
Ni nani kakuambia kuna aliyemakini aliyependa Kikwete aongoze nchi hii. Ni nani aliyekwambia Kikwete na kundi lake waliandika bluu book dhidi ya Mkapa walikuwa hawana chuki. Si unaona na yeye anavyoweweseka kufikiri Lowasa anamwandikia.
Angekuwa hana chuki, kwanini wengine aliwapiga chini na wengine kuwapuuza waliukuwa washauri wa Mkapa, Mwinyi na Nyerere ktk masuala ya uchumi?

Mambo yamwemuwia magumu. Amejaribu kutaka nchi ijiendee yenyewe [natural progression] inamgomea, sasa anatafuta mtu wa kumsaidia. Mzigo huo anataka kumpa Mkapa kiaina.

CCM imeanguka, hawawezi kuisimamisha tena. Wakitumia nguvu wataendelea kumwaga damu, na damu iliyomwagika kamwe haijawahi kupata UBUBU.
 
Baada ya wanamtandao kumfitinisha Kikwete na Mzee Benjamin Mkapa mwaka 2005 huku wakipandikiza chuki dhidi ya Mkapa kwa madai kuwa alikuwa hamtaki Kikwete chuki ambazo zimewahi hata kuandikwa na magazeti nchini , ikiwa ni mwaka wa sita akiwa madarakani rais Jakaya Kikwete amewaambia wasaidizi wake Mkapa ni simba ingawa haungurumi kwa maana ya kutopenda kujionyeshajionyesha. Kubadili mtazamo kwa Kikwete dhidi ya Mkapa ndiyo kunaelezwa kuwa ndiyo kiini cha mzee Ben Mkapa kurejea kwa kasi kwenye ulingo wa siasa za kitaifa, na siyo hivyo tu lakini pia inaelezwa tayari Kikwete ameanza kuandaa mkakati wa kuhakikisha Mkapa anakuwa Mwenyekiti wa CCM kwa mara nyingine tena ili kumaliza makundi hasimu ndani ya chama hiko lakini pia ili kuivusha salama CCM kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

good LORD....what??!!
 
Sasa hi habari ina mchango gani katka kutatua kero za umma wa watanzania?
 
Kwa maana hiyo Kikwete ni mtu wa fitna na visasi kama Mkapa alimchukia basi leo hii asingekuwa Rais haswa kwa kutumia katiba kwa jinsi ilivyo ingewezekana kumtupilia mbali...
 
..mmeshasahau alivyojimilikisha Kiwira??

..bila shaka ufisadi una tafsiri nyingi na tata.
 
Ben ni Simba kwako wewe ulieleta thread hii,hivi wengine huwa mnakunywa maji ya kusafishia masaburi? Aibu gani unajionyesha we ndugu,ufisadi aloufanya unatuambia ni simba mnyama au simba jina?huji kama kuna Kiwira,unajua alichukua nani,maana huko si kununua kwa bei hiyo,Magorfa ya kariakoo kwa kivuli cha mkewe Anna ambayo yalikuwa yanapangwa wakati wako Ikulu unayajua? sitaki kukumbuka zaidi maana ni kinyaa,labda kama unamaanisha ni simba jina basi nisamehewe lakini kama unamlinganisha na simba mnyama basi aende porini japo nako huko wanapakiwa kwenda ulaya,ila kama unaoanisha nguvu za simba mnyama na nguvu za kiungozi,basi sitaki hata kusikia unanibipi unisamehe,maana kwang fisadi ni fisadi tu.
 
Back
Top Bottom