JK; Nimekubali Kuwa Ben Mkapa Ni Simba Ingawa Hangurumi!

Adolf Mark

Member
Nov 4, 2011
50
26
Baada ya wanamtandao kumfitinisha Kikwete na Mzee Benjamin Mkapa mwaka 2005 huku wakipandikiza chuki dhidi ya Mkapa kwa madai kuwa alikuwa hamtaki Kikwete chuki ambazo zimewahi hata kuandikwa na magazeti nchini , ikiwa ni mwaka wa sita akiwa madarakani rais Jakaya Kikwete amewaambia wasaidizi wake Mkapa ni simba ingawa haungurumi kwa maana ya kutopenda kujionyeshajionyesha. Kubadili mtazamo kwa Kikwete dhidi ya Mkapa ndiyo kunaelezwa kuwa ndiyo kiini cha mzee Ben Mkapa kurejea kwa kasi kwenye ulingo wa siasa za kitaifa, na siyo hivyo tu lakini pia inaelezwa tayari Kikwete ameanza kuandaa mkakati wa kuhakikisha Mkapa anakuwa Mwenyekiti wa CCM kwa mara nyingine tena ili kumaliza makundi hasimu ndani ya chama hiko lakini pia ili kuivusha salama CCM kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
 
lakini pamoja na udhaifu wake uncle ben ni kichwa bwana, aliweza kabisa kwa muda mfupi kuuweka uchumi wa JMT kwenye mstari. Kama isingekuwa hawa wahuni tulionao hivi sasa kwenye madaraka hivi sasa JMT tungekuwa tunaongoza kwa uchumi mzuri EAC. Huyu JK ni sawa na ule usemi wa mtoto akililia wembe mpe.
 
Kwenye huo mkutano nani alitajwa kama swala anayewindwa na simba huyo?
 
Nilidhani mkapa wa maana, lakini alipojipeleka kwenye kauchaguzi ka Igunga ndipo wengi walipomtoa maanani. Ilibidi magamba wafanye kazi ya ziada usiku wa kuhesabu kura kuhahikisha ushindi kwao hata kama ni kwa kuiba ili mstaafu asiaibike. Shame on him....
Pale hakika alijishushia heshima kubwa aliyokuwa nayo mbele ya jamii ya watanzania. Kwenda kwake Igunga kulisababisha vurugu nyingi kuongezeka kwani magamba walikuwa wakihaha kuhakikisha walau mkapa hatarudi kwa aibu. Matokeo yake tunafahamu... vifo vya raia 4 waliosadikiwa kuuawa na wanamagamba.
Mkapa muuaji. Kufanya biashara ikulu, kujiuzia mali ya umma kwa bei chee ni uuaji wa kwanza mkubwa aliowafanyia watanzania.
Rais mstaafu aliye na heshima mbele ya jamii yetu Watanzania sasa, ingawa alichemsha wakati wa uongozi wake, ni mzee ruksa tu.
Labda mzee Ruksa tu ampigie debe mgombea urais wa magamba 2015, ili walau asikilizwe.
 
Baada ya wanamtandao kumfitinisha Kikwete na Mzee Benjamin Mkapa mwaka 2005 huku wakipandikiza chuki dhidi ya Mkapa kwa madai kuwa alikuwa hamtaki Kikwete chuki ambazo zimewahi hata kuandikwa na magazeti nchini , ikiwa ni mwaka wa sita akiwa madarakani rais Jakaya Kikwete amewaambia wasaidizi wake Mkapa ni simba ingawa haungurumi kwa maana ya kutopenda kujionyeshajionyesha. Kubadili mtazamo kwa Kikwete dhidi ya Mkapa ndiyo kunaelezwa kuwa ndiyo kiini cha mzee Ben Mkapa kurejea kwa kasi kwenye ulingo wa siasa za kitaifa, na siyo hivyo tu lakini pia inaelezwa tayari Kikwete ameanza kuandaa mkakati wa kuhakikisha Mkapa anakuwa Mwenyekiti wa CCM kwa mara nyingine tena ili kumaliza makundi hasimu ndani ya chama hiko lakini pia ili kuivusha salama CCM kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Jisome hapo penye rangi.
Ni nani kakuambia kuna aliyemakini aliyependa Kikwete aongoze nchi hii. Ni nani aliyekwambia Kikwete na kundi lake waliandika bluu book dhidi ya Mkapa walikuwa hawana chuki. Si unaona na yeye anavyoweweseka kufikiri Lowasa anamwandikia.
Angekuwa hana chuki, kwanini wengine aliwapiga chini na wengine kuwapuuza waliukuwa washauri wa Mkapa, Mwinyi na Nyerere ktk masuala ya uchumi?

Mambo yamwemuwia magumu. Amejaribu kutaka nchi ijiendee yenyewe [natural progression] inamgomea, sasa anatafuta mtu wa kumsaidia. Mzigo huo anataka kumpa Mkapa kiaina.

CCM imeanguka, hawawezi kuisimamisha tena. Wakitumia nguvu wataendelea kumwaga damu, na damu iliyomwagika kamwe haijawahi kupata UBUBU.
 
lakini pamoja na udhaifu wake uncle ben ni kichwa bwana, aliweza kabisa kwa muda mfupi kuuweka uchumi wa JMT kwenye mstari. Kama isingekuwa hawa wahuni tulionao hivi sasa kwenye madaraka hivi sasa JMT tungekuwa tunaongoza kwa uchumi mzuri EAC. Huyu JK ni sawa na ule usemi wa mtoto akililia wembe mpe.

Ben,hana jipya kama ni wizi katuibia sana, 2015 anguko pale pale,labda mwl nyerere afufuka
 
Back
Top Bottom