JK: Ni Marufuku kipengele cha Dini kwenye Sensa

JK: Ni Marufuku kipengele cha Dini kwenye Sensa

jamaaa kaongea pumba sana, ye amejuaje kuwa alioneshwa na Mungu katika hilo?
Halafu mwalimu nyerere alifanya aliyo yafanya kwa mtazamo na maono yake wakati ule jamani watu waache kumsakama.
Na nalojiuliza kuhusu hiki kipengele hivi kitu gani kitafuata baada ya kujua dhehebu ili ni kubwa kuzidi hili.
 
usiliangushe kanisa kiasi hichi Katika Injili za Mathayo, Marko na Luka, Yesu ameitwa mara 22 kwa jina la "Mwana wa Mungu", lakini hata mara moja yeye mwenyewe hakujiita kwa jina hilo. Katika Mathayo 27.43 tuliyonukulu hapo juu yanatajwa maneno ya wakuu wa makuhani wa Kiyahudi pamoja na waandishi na wazee waliokuwa wakimdhihaki, si maneno yake yeye Yesu. Hao walikuwa wakimzulia kuwa anadai uwana wa Mungu, na anadai kuwa ni Mfalme wa Israeli. Mara nyingi waliokuwa wakimwita Mwana wa Mungu walikuwa ama wendawazimu, wenye pepo wachafu, au askari wa Kirumi ambao tokea hapo wao ni washirikina, mapagani. Ama mwenyewe Yesu alikuwa daima akipendelea kujiita mwana wa Adamu kwa Kiebrani, lugha yake, Bin Adam, yaani ni binaadamu, mtu tu. Katika Injili jina hili la Yesu kuitwa mwana wa Adamu limetajwa yapata mara 80. Mahasimu zake wa Kiyahudi walimzulia kuwa alidai kuwa ni Mfalme wa Mayahudi ili kumchongea kwa watawala wa Kirumi, na kuwa alidai kuwa ni Mwana wa Mungu ili apate kuchusha kwa Mayahudi. Francis Young, Mwalimu wa mafunzo ya Agano Jipya katika Chuo Kikuu cha Birmingham, Uingereza, akiandika katika kitabu kinachoitwa The Myth of God Incarnate (Uwongo wa Mungu kuwa Mtu) anasema: "Isipokuwa katika Injili ya Yohana, ambako maneno ya maelezo yamewekwa kwenye mdomo wa Yesu, injili zote nyengine zinaeleza kuwa wenye kutumia maneno kama 'Mtakatifu wa Mungu', au 'Mwana wa Daudi', au 'Mwana wa Mungu' si Yesu bali wengineo. Jina pekee alilokuwa mwenyewe Yesu daima akilitumia ni 'Mwana wa Adamu'... " Yafaa pia tukumbuke kuwa katika zama za Yesu ilikuwa ni jambo lililoenea kuwabandikiza ungu viumbe vya hadithini na hata wanaadamu wa kweli kweli walio hai. Mwandishi wa kipagani Laertu alieandika kitabu kiitwacho Lives of the Philosophers (Maisha ya Mafailasufi), ameandika kuwa mafailasufi kadhaa wa kadhaa walikuwa wana wa Mungu. Plato amesimuliwa kuwa wazee wake ni miungu; hali kadhaalika Paithagoras akiaminiwa kuwa ni mwana mungu aliyekuwa mwanaadamu na mzazi wake ni mungu aitwae Hermes. Empedokles pia alidaiwa kuwa ni mungu wa milele aliyekuwa akiponyesha wagonjwa, na wafwasi wake wakimuabudu na kumsalia. Plutarch, mwandishi mwengine wa zama hizo, alikuwa anaamini kuwa bila ya shaka yo yote Alexander (Iskandar) Mkubwa ni mwana wa mungu, na Romulus, huyo anayedhaniwa kuwa ndiye baba wa Warumi, alikuwa ni Mwana wa Mars (Marrikh), mungu wa vita. Yeye akiaminiwa kuwa alipaa mbinguni katika kiwingu. Yapo maandishi ya mwaka 48 K.K. (Kabla ya Yesu) yaliyomweleza Juliasi Kaisari, Mtawala maarfu wa Warumi, kuwa ni 'mungu wa kweli, mwana wa Ares na Aphrodites, mwokozi wa wote wa maisha ya wanaadamu.' Maandishi mengine yanamtaja Agosti Kaisari, aliyerithi utawala wa Juliasi, kuwa 'Mfalme wa wafalme, Kaisari, Mwana wa Mungu, mungu Agosti, mwaangalizi wa ardhi na bahari'. Majina haya, basi, ya "mungu", "mwana wa mungu" na "Bwana" kwa kuwa yalikuwa yameenea na maarufu katika nchi za bahari ya Kati (Mediterranean) katika zama za Yesu haiwezi kukosa kuathiri mawazo ya watu ambao bado haijawavaa imani ya Mwenyezi Mungu Mmoja kama ilivyokuwa ikifunza dini ya Kiyahudi. Majina kama hayo yalikuwa yakitumiliwa ovyo na kila mtu takriban. Na hizo hadithi za watu kama hao, ikiwa ni watu wa hadithini tu si wa kweli kweli, au watu walioishi kweli kweli duniani, zimefanana mno na hizo ambazo khalafu yake zikaaminiwa na Wakristo kuwa zimemkhusu Yesu Kristo peke yake. Francis Young katika insha yake inayoitwa Mizizi Miwili au Matatanisho (Two roots or a Tangled Mass) ameandika: "Tena, hatuwezi kutupilia mbali mawazo kuwa mambo kama hayo yalitokea kwa mintarafu ya Yesu. Kwa mfano, kuna kufanana kukubwa baina ya hadithi ya Romulus, kama alivyoeleza Livy, na baadhi ya hadithi zinavyoelezwa kuwa ni za Yesu katika Injili: kuzaliwa na bikra, kutiwa mimba na mungu, maisha ya kiajabu, kutoonekana mabaki yake baada ya kufa, kutokea tena baada ya kufa na kuwatuma wafuasi wake, kumwomba kwa sala. Itakuwa ni muhali kuleta ushahidi kuwa haya yote yaliigwa tu; lakini watu walioishi wakati mmoja sana huonekana kuwa wanazua hadithi zilizoelekeana." Tukirejea kuyanukulu yaliyomo katika Biblia tunamwona Yesu mahkamani alikataa kukiri mashtaka aliyoshtakiwa kuwa yeye alidai kuwa ni Mwana wa Mungu, kama wendawazimu na mapagani walivyokuwa wakimuenezea: Kisha Kuhani Mkuu akasimama akamwambia, Hujibu neno? Hawa wanakushuhudia nini? Lakini, Yesu akanyamaza. Kuhani Mkuu akamwambia, Nakuapisha kwa Mungu aliye hai, utuambie kama wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu. Yesu lakini nawaambieni, Tangu sasa mtamwona Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija juu ya mawingu ya mbinguni.
Soma tartibu hiyo cp utaona ushahidi wa wazi kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu!Tatizo unasoma bila tohara ya Rohoni! Tofautisha Biblia Takatifu na Qaraa tukufu! Qaraa ni kukariri ukimaliza juzuu zote unapokea utukufu kwa mwanadamu na kupewa zawadi! Hivyo hata mie mgen nikitoka kula laga yangu nikiwashinda kukariri mtanizawadia ushehe na smg! Utapona tu!
 
mmemfanya nyerere ni kajimungu kenu,mtakuja kujua kuwa hana uwezo!
 
Kwa hiyo hutaki kuambiwa kuwa nyerere alikuwa na maono akiongozwa na mungu au?
 
Nimesikia leo kwenye Nukuu za hotuba za Mwalimu Nyerere (radio tanzania) akizungumzia kukiondoa kipengere hicho kwavile hatuhitaji kujenga misikiti wala makanisa. Amebainisha wazi kuwa jukumu la kujua idadi ya waumini wa kila dini ni la viongozi wa dini hizo!(Kama hauna ukakasi na rtb, jaribu kuvizia vizia kipande hicho cha hotuba kwani kimelenga kuelimisha kuhusu sensa kwa muda huu)
 
....Leo kwenye kipindi cha Tuambie kinachorushwa na TBC1 mkurugenzi wa takwimu wa Taifa ametoa kihoja fulani ambacho mimi nasema kuwa ni moja ya kauli ambazo zinamdhalilisha mwalimu Nyerere mbele ya jamii..akihojiwa kwanini kipengele cha dini kilitolewa alisema " MWALIMU NYERERE ALIONYESHWA NA MUNGU KUONDOA KIPENGELE HIKI CHA DINI KWENYE DODOSO LA SENSA" kauli kama hizi ni kauli za viongozi wasiojua kupanga hoja, huyu mama anaonekana ni dhaifu kujibu hoja za moto zilizokuwa zinarushwa hasa toka kwa waislamu.

Siku hizi umekuwa ni utaratibu wa kila mtu kumtaja Mwalimu Nyerere anapokuwa ameshindwa kusimamia hoja yake.
Mwalimu amefariki tangu mwaka 1999, sasa hii sensa ya mwaka 2012 anahusikaje kwenye kuandaa dodoso?
Mwalimu Nyerere ameondoka madarakani mwaka 1985, sensa kadhaa zimefanyika akiwa hayuko madarakani, sasa anahusishwa vipi na uandaaji wa madodoso?
 
JK hivi kuna kitu umeweza kukifanya ndani ya serikali yako kikapata muitikio wa kitaifa?una mkosi gani?mbona hupendwi hivi?au dawa uliyokuwa unapakaa ya kupendwa kichupa kimeisha..nenda ka renew mzee wangu hali ni mbaya sana kama hujui
 
Siku hizi umekuwa ni utaratibu wa kila mtu kumtaja Mwalimu Nyerere anapokuwa ameshindwa kusimamia hoja yake.
Mwalimu amefariki tangu mwaka 1999, sasa hii sensa ya mwaka 2012 anahusikaje kwenye kuandaa dodoso?
Mwalimu Nyerere ameondoka madarakani mwaka 1985, sensa kadhaa zimefanyika akiwa hayuko madarakani, sasa anahusishwa vipi na uandaaji wa madodoso?

Mwacheni Baba wa Taifa apumzike kwa amani
 
Mkuu only83 bahati mbaya sikukiona hicho kipindi lakini kama kweli amejibu hivyo hakika inadhihirisha wapo watendaji wakuu wa serekali waliopewa madaraka pasipo kustahili.

Hoja za kuondoa kipengele cha dini zipo nyingi moja kubwa sana ni kuondoa uwezekano wa kuwagawa waTanzania kwa kisingizio cha imani za dini.Ikitokea leo sensa ikafanyika kwa misingi ya dini moja wapo kati ya ukristo au uIslam ikawa na idadi kubwa zaidi masuala ya kutaka mgao wa rasilimali kwa misingi ya dini uenda ukaibuka.Ifahamike serekali ya Tanganyika haiendeshwi kwa misingi ya dini.

Jitu zima linapokuja na majibu ya mitaani bado linaachwa kuendelea na wadhifa wake !.
 
Last edited by a moderator:

Ngongo mkuu yani mimi nilibakia namwangalia yule mama nikashindwa kumuelewa, halafu kibaya zaidi hata waliokuwa pale studio hawakumrekebisha katika hili. Si sahihi kumbebesha mwalimu Nyerere uozo wetu, yani mtu unashindwa kujibu hoja unasema mwalimu Nyerere alisema. Huu ni udhaifu mkubwa, ni kweli tunaweza tukachukua yale mazuri ya mwalimu kama reference lakini na sio kama uamuzi wa mwisho.
 
Hapa kazini kuna mzee mmoja wa kiislamu kaniambia eti leo waislamu wanaandamana ili kipengele cha dini kiwekwe kwenye questionnaire za sensa mwenye uhakika juu ya hilo atujulishe.
 
Mimi ninafikiri kama kweli kajibu hivyo inamaanisha kwamba hata yeye mwenyewe hakubaliani na kitendo hicho cha kuondoa kipengele cha dini lakini ni amri tu kutoka juu yake.Lakini swali ni kwamba wapi tutapata takwimu halisi za waumini (wakristo, waislamu nk) za uhakika kama siyo ofisi za takwimu?. Kwa zama hizi za sayansi na teknolojia vitu hivi havihitaji kuwa siri.JUKUMU LA WATAALAMU NI KUTATUA MATATIZO NA SIYO KUYAKIMBIA.
 
Sory sijawaelewa vizuri mnaposema kuondolewa kwa kipengele cha udini maana yake ni sensa ya mwaka gani ilikua ni kipengere hicho?.
Ninavyojua madhehebu yote yanajua idadi ya waumini wake iweje waislamu wasijue wako wangapi?
Kwa hili ni wazi kua Uislamu hauna msingi thabiti ya kiutawala yaan wanatengana mskiti mmoja hadi mwingine wangeungana wote pamoja wangejuana idadi zao.Inashangaza kuona wanalazimisha serikali iwasaidie kuhesabiwa.
Mbona madhehebu ya Kikristo hawana tatizo kama hili? Mfano Wakatoliki kila mwaka huwa wanafanya sensa ya kuanzia Jumuia hadi Majimbo tena sidhani kama zoezi hili linawagharimu fedha yoyote kwan ni moja ya majukumu ya viongozi wa Jumuia.Waislamu wanashindwa nini kujifunza kwa wenzao?.Au kuna agenda nyinginezo wanazotaka toka serikalini,najiuliza kama uislamu unasumbua serikali hii ambayo rais na makamu wa raisi ni waislamu itakuaje pale serikali itakapokua chini ya muumini wa Kikristo?.
Sitaki kuingilila imani za watu lakini naomba watafakari maana halisi ya"Serikali haina dini ila watu wake wanadini".Ninavyofahamu dini ni taasisi huru inapaswa kua na uongozi wake na sera zake bila kuingilia majukumu ya serikali.
Wakiingiza kipengere cha udini basi utafuata Ukabila sasa sijui mwisho wake itakuaje.
 
Lengo ni kupata official data inayosema idadi ya waumini wa dini mbali mbali, jamani mbona mnakuwa na uoga ambao hata sioni msingi wake!! Kuna tatizo gani kwani hicho kipengele kikiwekwa?...swali lako la lini mara ya mwisho kilikuwapo hata mimi najiuliza.
 
Mama amesema ukweli anaoujuwa kujivua dhima la dhana nzima juu ya nani aliyeondoa dodoso hilo katika sensa. Mtu akisema kweli ni kosa siku hizi. Huyu mama ni muwajibikaji na ninavyomuelewa huwa anasema ukweli na mwaminifu kwa kazi yake.
 
Kwa kuwa jamii ya watanzania wameonyesha kutokuwa tayari kushiriki zoezi hili hivyo ni hakika serikali haitopata idadi kamili na ya uhakika na hivyo kufanya zoezi hili SI SENSA bali ni UTAFITI WA SENSA. Je wewe utashiriki zoezi hili

  • Ndio
  • Hapana
  • Sijui
 
Back
Top Bottom