JK: Ni Marufuku kipengele cha Dini kwenye Sensa

JK: Ni Marufuku kipengele cha Dini kwenye Sensa

Lengo ni kupata official data inayosema idadi ya waumini wa dini mbali mbali, jamani mbona mnakuwa na uoga ambao hata sioni msingi wake!! Kuna tatizo gani kwani hicho kipengele kikiwekwa?...swali lako la lini mara ya mwisho kilikuwapo hata mimi najiuliza.
Hizo official data zitakua na manufaa gani kwa jamii hali mgawanyo wa rasilimali na huduma za jamii hautegemei udini?.Wewe undadhani hao jamaa wataishia kujijua wapo wangapi,wanamambo mengi nahisi wanataka kudai ila bas tu usilolijua ni usiku wa giza.
Ninavyofahamu hata kwa watu wanaofanya research,data collection huwezi kukusanya data tu ilmradi,lazima zihusiane na project husika.
Hivyo kutaja tu Waislamu ni X% na Wakristo ni X% ya watanzania wote haiwezi kusaidia lolote kwan serikali haifanyi kazi kwa kuzingatia magroup hayo.Na si dhani kama Waislamu wataridhika tu kusikia wapo wangapi maswali mengine yatafuata ambayo hayatakua na majibu baadaye
.
Fikiria Wasukuma,Wahaya,Wachaga,Wapare,Wagogo n.k nao wakidai wajijue ni wangapi nini hatima yake?

 
hivi kipengele cha dini ina manufaa kwa waislam tu?
Au tukisema dini tunamaanisha uislam?
Unajua ukilalamika sana ni dalili ya inferiority complex
 
Soma tartibu hiyo cp utaona ushahidi wa wazi kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu!Tatizo unasoma bila tohara ya Rohoni! Tofautisha Biblia Takatifu na Qaraa tukufu! Qaraa ni kukariri ukimaliza juzuu zote unapokea utukufu kwa mwanadamu na kupewa zawadi! Hivyo hata mie mgen nikitoka kula laga yangu nikiwashinda kukariri mtanizawadia ushehe na smg! Utapona tu!

mwadhama umebaki kufakamia divai ya damu ya Yesu hata kondoo unawasahau , unachokiandika hukijui tena

mwiba mwengine huu

Utumiaji ovyo ovyo maneno hayo matakatifu kama "Mungu" au ya kufuru kama "mwana wa Mungu" yaliyotumiwa na waandishi wa Biblia yaonyesha wazi vipi imani na agano la Ibrahimu na Manabii wengine walilofungamana kwalo na Mwenyezi Mungu lilivyopotoshwa.

Mayahudi ambao kumshirikisha Mwenyezi Mungu na cho chote ni mwiko walishawishiwa na watawala wao na makafiri waliokuwa wakikaa nao kutumia lugha na maneno ya kikafiri bila ya wenyewe kutambua.

Sisi tunaona vipi hii leo tulivyoharibiwa hata Kiswahili chetu na watawala ambao mila na dini zao ni mbali na yetu. Tunaona vipi maneno kama "Halali na Haramu" yalivyopotoshwa hata imekuwa yanatumiwa kuwa ni kilichoruhusiwa au kukatazwa na serikali au chama kinachotawala, wala sio kama ilivyo asli kuwa alichohalalisha na kuharimisha Mwenyezi Mungu.

Tunasikia inasemwa kuna pombe ya "halali", yaani inayoruhusiwa na serikali. Tunasikia kuna majumba au mashamba yaliyopokonywa (kughusubiwa) na serikali yanaambiwa ati "yametaifishwa" kihalali. Na ilhali hapana unyan'ganyi, au wizi wa halali. Yote ni haramu.

Hata hili neno "sharia" limepotoshwa pia. Sharia ni sharia ya Kiislamu tu. Ya Serikali ni "Kanuni" si sharia. Sharia ni ya Mwenyezi Mungu.

Makosa anayoyafanya mcheza mpira (faul) sasa yanaitwa: Dhambi. Badala ya Nguzo Tano za Uislamu watoto wetu wanafunzwa "Nguzo tano za ujamaa".

Ni namna hivyo basi waandishi wa Biblia wa Kiyahudi ambao walikuwa wakimuamini Mwenyezi Mungu mmoja waliikoroga lugha yao kwa kuwa maneno ya kikafiri ya watawala wao wa kipagani wa Kirumi na jirani zao mapagani wa Kigiriki, wa Kimisri na wengineo waliokuwa katika pande zile za mashariki ya Bahari ya Kati (Mediterranean Sea) yaliwaathiri hata wao wakawa wanayatumia kama jambo la dasturi.

Tuliyokwisha kuyanukulu ni maneno ya kutokana na sehemu ya Biblia iitwayo Agano la Kale, yaani ile sehemu iliyoandikwa kueleza mambo ya Manabii waliokuwa kabla ya Yesu. Hebu tuangalie sasa yaliyosemwa na Agano Jipya lilioandikwa baada ya Yesu. Luka anatusimulia katika Injili yake alivyohubiri Yesu:



Bali wapendeni adui zenu, tendeni mema, na kukopesha msitumaini kupata malipo, na thawabu yenu itakuwa nyingi; nanyi mtakuwa wana wa Aliye juu, kwa kuwa yeye ni mwema kwa wasiomshukuru na waovu.

Luka 6.35
​

Hapo twaona Yesu anawaambia wafwasi wake kuwa katika malipo ya watendao mema na kuwapenda maadui zao ni kuwa watakuwa "wana wa Aliye juu" yaani Mwenyezi Mungu. Katika Injili ya Mathayo Yesu anasema:

Heri wapatanishi;


Maana hao wataitwa wana wa Mungu.
Mathayo 5.9
​

Ni wazi kwa maneno haya kuwa Yesu hakujiona yeye kuwa ni "mwana wa Mungu" kwa maana ya namna ya peke yake kama linavyofundisha Kanisa.

Kwa mujibu wa Biblia wote watendao mema, wapatanishi, wanaokopesha bila ya kutaraji kulipwa n.k. ni "wana wa Mungu".

Hiyo ndiyo lugha ya Kibiblia, ndiyo lugha iliyokuwa ikitumiwa wakati huo. Nasi tutakuwa wajinga tukimsikia mtangazaji wa redio au T.V. kwenye uwanja wa futboli akisema: "Kafanya dhambi" kwa kuwa mchezaji kaugusa mpira kwa mkono, nasi tukaamini kuwa yule mtu kweli kafanya dhambi tunayoijua sisi, yaani kamkosa Mwenyezi Mungu na hivyo anastahiki kutiwa katika jahannam! Haya yanadhihirika wazi katika hadithi hii inayosimuliwa katika Injili ya Yohana.

Mayahudi walipotaka kumpiga mawe Yesu aliwauliza kwa vitendo gani vyema alivyowaonyesha ndio wanampiga?


Wayahudi wakamjibu, Kwa ajili ya kazi njema hatukupigi kwa mawe; bali kwa kukufuru, na kwa sababu wewe uliye mwanadamu wajifanya mwenyewe u Mungu. Yesu akawajibu, Je! haikuandikwa katika torati yenu ya kwamba, Mimi nimesema, Ninyi miungu?
Ikiwa aliwaita miungu wale waliojiliwa na neno la Mungu; (na maandiko hayawezi kutanguka); je! yeye ambaye Baba alimtakasa, akamtuma ulimwenguni, ninyi mnamwambia, Unakufuru; kwa sababu nalisema, Mimi ni Mwana wa Mungu?
Yohana 10.33-36
​

Kwa mujibu wa kauli hiyo iliyoelezwa na Yohana tunafahamu kuwa Yesu anawaambia Mayahudi kuwa ikiwa katika vitabu vyao watu wema wote wameitwa "wana wa Mungu" pana ajabu gani basi kuwa Mtume wa Mungu aliyetakasika akaitwa vile vile ni "mwana wa Mungu" kwa maana hiyo ya jumla jamala. Na haya yanawekwa wazi na maneno aliyoyanukulu huyo huyo Yohana kuwa Yesu akimwambia Mariamu Magdalene:



Lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, Ninapaa kwenda kwa Baba yangu naye ni Baba yenu, kwa Mungu wangu naye ni Mungu wenu.

Yohana 20.17
​

Hata Paulo naye amesema katika barua yake aliyowapelekea Warumi:



Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.

Warumi 8.14
​

Yohana na Paulo ndio wakubwa wa kumfanya Yesu ni Mungu, au mwana wa Mungu, lakini hata wao wametoa ushahidi wa kutosha kuwa huo "uwanamngu" wa Yesu ndio ule ule kama walio nao wote walio wema.

Mwandishi wa Kimarekani maarufu, Upton Sinclair, akiandika katika kitabu chake A Personal Jesus (Yesu Mtu) amesema:



"Na ili asidhani mtu ye yote kuwa kwa kumuita Mungu kuwa ni Baba yake, Yesu akijitangaza kuwa yeye ni Mwana wa Mungu, yafaa ibainishwe wazi ya kuwa vile vile alimwita Mungu 'Baba yenu.' Aliyasema hayo mara kumi na nane katika Agano Jipya: 'Baba yenu wa mbinguni anajua,' na kadhaalika. Alikusudia ya kuwa sote sisi ni wana wa Mungu, na yeye (Yesu) ni mmoja wao."


​
http://www.quranitukufu.net/Biblia/MWANA.htm#_top

 
....Leo kwenye kipindi cha Tuambie kinachorushwa na TBC1 mkurugenzi wa takwimu wa Taifa ametoa kihoja fulani ambacho mimi nasema kuwa ni moja ya kauli ambazo zinamdhalilisha mwalimu Nyerere mbele ya jamii..akihojiwa kwanini kipengele cha dini kilitolewa alisema " MWALIMU NYERERE ALIONYESHWA NA MUNGU KUONDOA KIPENGELE HIKI CHA DINI KWENYE DODOSO LA SENSA" kauli kama hizi ni kauli za viongozi wasiojua kupanga hoja, huyu mama anaonekana ni dhaifu kujibu hoja za moto zilizokuwa zinarushwa hasa toka kwa waislamu.

...Kwanza kusema kuwa Mwalimu Nyerere ndio alitoa kipengele cha dini si kweli, huu ni upotoshaji mkubwa, kwa kusema hivyo ina maana kuwa Mwalimu Nyerere alikitoa kipengele cha dini kwasababu ya fikra zake na muono wake. Huu ni upotoshaji. Pili, hizi kauli za kusema kila kitu mwalimu Nyerere alionyeshwa na MUNGU ni hoja dhaifu na zinazotoka midomoni mwa watawala wanaotaka kufukia udhaifu wao kupitia migongoni mwa Mwl Nyerere.

kwa hiyo wewe unataka kiwekwe au........ushabiki mwingne bhana hovyoooooooooooooo
 
Mimi ninafikiri kama kweli kajibu hivyo inamaanisha kwamba hata yeye mwenyewe hakubaliani na kitendo hicho cha kuondoa kipengele cha dini lakini ni amri tu kutoka juu yake.Lakini swali ni kwamba wapi tutapata takwimu halisi za waumini (wakristo, waislamu nk) za uhakika kama siyo ofisi za takwimu?. Kwa zama hizi za sayansi na teknolojia vitu hivi havihitaji kuwa siri.JUKUMU LA WATAALAMU NI KUTATUA MATATIZO NA SIYO KUYAKIMBIA.

umeshaambiwa nchi haina dini(secular state) sasa hizo takwimu za nini....tujadili mambo ya msingi tusishabikie mambo ya kutugawa
 
kwa hiyo wewe unataka kiwekwe au........ushabiki mwingne bhana hovyoooooooooooooo

Jaribu kusoma kwanza post vyema mkuu Baro. Mimi nimesema kusema kuwa Mwl Nyerere alionyeshwa na MUNGU kufuta kipengele cha dini ni moja ya mifano mingi ya viongozi wetu dhaifu wanaotaka kutumia kichaka cha udhaifu wao wa kufanya mambo kupitia hoja kuwa Mwl Nyerere alionyeshwa. Mimi kipengele cha dini kuwepo au kutokuwepo haina maana kwangu. Hoja hapa ni kuwa ni haki kweli kusema Mwl Nyerere ndio alionyeshwa na MUNGU kufuta kipengele cha dini?
 
JK hivi kuna kitu umeweza kukifanya ndani ya serikali yako kikapata muitikio wa kitaifa?una mkosi gani?mbona hupendwi hivi?au dawa uliyokuwa unapakaa ya kupendwa kichupa kimeisha..nenda ka renew mzee wangu hali ni mbaya sana kama hujui

udhalilishaji
 
Mkuu only83 bahati mbaya sikukiona hicho kipindi lakini kama kweli amejibu hivyo hakika inadhihirisha wapo watendaji wakuu wa serekali waliopewa madaraka pasipo kustahili.
....Jitu zima linapokuja na majibu ya mitaani bado linaachwa kuendelea na wadhifa wake !.
Kweli kama ingekuwa "nchi za watu" huyu mama leo ndio ungekuwa mwisho wake wa kukanyaga ofisi.
Ni mwajiriwa wa chombo cha serikali ambayo ni sekula chombo kinachowakilisha watu wa dini zote, iweje aje kutuambia Waislamu kuwa Mungu alikuwa akizungumza na Nyerere wakati hii inakinzana na imani yetu, kwa sababu katika imani yetu baada ya Wahy kukoma kushushwa kutoka mbinguni HAKUNA BINADAMU awezaye kuzungumza na Mungu! huyo atakayezungumza naye ni Shetani anayemdanganya kuwa niMungu, si Mungu!
Vipi kuhusu Wapagani nao ambao ni sehemu ya wakazi wa nchi hii na wanalipia kodi ya kuiendesha hii taasisi?
Anachotuambia ni kuwa hii nchi si ya kisekula! ina dini na dini ya nchi ni ile aliyokuwa akiifuata Nyerere! kunani Tanzania?!
 
kuna mambo ya Nyerere ya kufuatwa na yakuachwa..
Hli ni la kulitupilia mbali..

Yule mama aliongea pumba.
 
Lengo ni kupata official data inayosema idadi ya waumini wa dini mbali mbali, jamani mbona mnakuwa na uoga ambao hata sioni msingi wake!! Kuna tatizo gani kwani hicho kipengele kikiwekwa?...swali lako la lini mara ya mwisho kilikuwapo hata mimi najiuliza.

umenena vyema mkuu.
 
Jaribu kusoma kwanza post vyema mkuu Baro. Mimi nimesema kusema kuwa Mwl Nyerere alionyeshwa na MUNGU kufuta kipengele cha dini ni moja ya mifano mingi ya viongozi wetu dhaifu wanaotaka kutumia kichaka cha udhaifu wao wa kufanya mambo kupitia hoja kuwa Mwl Nyerere alionyeshwa. Mimi kipengele cha dini kuwepo au kutokuwepo haina maana kwangu. Hoja hapa ni kuwa ni haki kweli kusema Mwl Nyerere ndio alionyeshwa na MUNGU kufuta kipengele cha dini?

mkuu, ONLY 83.nimekusoma mimi nafikiri hili suala la dini mwalimu alifanya vizuri kutoliweka kwani kwa hali inavyoonekana lingeleta madhara makubwa hapo baadae nafikiri alikuwa anamuono mzuri....ni kweli kuna watu wanashindwa kujibu hoja na kumsingizia mwalimu nyerere hii ni kutokana na upeo wao mdogo wa kuchambua mambo na kuwasilisha kwa jamii
 
Hizo official data zitakua na manufaa gani kwa jamii hali mgawanyo wa rasilimali na huduma za jamii hautegemei udini?.Wewe undadhani hao jamaa wataishia kujijua wapo wangapi,wanamambo mengi nahisi wanataka kudai ila bas tu usilolijua ni usiku wa giza.
Ninavyofahamu hata kwa watu wanaofanya research,data collection huwezi kukusanya data tu ilmradi,lazima zihusiane na project husika.
Hivyo kutaja tu Waislamu ni X% na Wakristo ni X% ya watanzania wote haiwezi kusaidia lolote kwan serikali haifanyi kazi kwa kuzingatia magroup hayo.Na si dhani kama Waislamu wataridhika tu kusikia wapo wangapi maswali mengine yatafuata ambayo hayatakua na majibu baadaye
.
Fikiria Wasukuma,Wahaya,Wachaga,Wapare,Wagogo n.k nao wakidai wajijue ni wangapi nini hatima yake?


Sasa hivi kuna data zinatolea kuwa Waislamu ni 35%, Wakristo 50% na wapagani 15% kuna kitu gani kinadaiwa na hao Waislamu au Wakristo kwenye mgawanyo wa rasilimali? Huoni kuwa kama kuna haja ya kuwa na data hizo kwa mwaka huu wa sensa? as long as serikali iko makini na opne na sheria ziko kuwa hii si serikali ya kidini na mganwanyo wa rasilimali hauko kidini then hamna tatizo. Problem tuliyo nayo ni kuwa serikali ya CCM, huwa inatumia haya makundi ya kidini ku influence matokeo ya uchaguzi, kumbuka pale Waislamu walipoaminishwa kuwa CDM ni ya Wakatoliki, Kumbuka CUF ilipofanywa ni chama cha Kiislamu na kigaidi. Unakumbuka swala la Kadhi lilikuwapo katika ilani ya CCM, then likatolewa, unadhani ni kwanini Kadhi ameruhusiwa kimya kimya?? Hayo ndio ya kupiga vita!!! Lakini hili la kupata data sio tatizo.
 
umeshaambiwa nchi haina dini(secular state) sasa hizo takwimu za nini....tujadili mambo ya msingi tusishabikie mambo ya kutugawa

mbona marekani isiyo na dini wanajua idadi ya raia wao kwa dini zao, hata ukitaka kujua jimbo lenye wayahudi wengi au waislam wengi unajua?
Kwanini tuwe na hofu zisizo na msingi.
Tunachotaka ni takwimu halisi zisizo na mashaka, sio kila dini itoe takwimu zake.
Kwanini tbc na tanapa walitoa takwimu za idadi wa watu kwa dini zao, wamezipata wapi ikiwa serekali haina takwimu hizo?
Sioni tatizo la kipengele hicho na nashangaa na watu wanaotumia nguvu nyingi kukipinga.
 
mbona ziko nyingi anza na hizi tu kwanza baadaye ndiyo utakuja na za sensa

mimi siwezi kufanya neno mwenyewe; kama nisikiavyo ndivyo nihukumuvyo; na hukumu yangu ni ya haki, kwa sababu siyatafuti mapenzi yangu mimi, bali mapenzi yake aliyenipeleka.
yohana 5.30

yohana 20:17,

yesu alimwambia mariam magdalene awaambie wafuasi zake: "yesu akawaambia, usinishike, kwa maana sijapaa kwenda kwa baba

lakini enenda kwa ndugu zangu ukawaambie, ninapaa kwenda

kwa baba yangu naye ni baba yenu,

kwa mungu wangu naye ni mungu wenu.


toa ayat inayokataza sensa kwa waislamu tujadili, mzee wa kupotosha mada.
 
Back
Top Bottom