Jana Tumeshuhudia tena Raisi wetu akipewa Degree ya Heshima baada ya ile ya Chuo Kikuu cha Dodoma. Safari hii ameibukia Chuo Kikuu cha Tiba Muhimbili.
Hivi hizi Degree za Heshima zitamsaidia nini kuongoza nchi. Ukifikiri sana hapa inaonekana kuwa ni usanii na uswahili wa Raisi wetu kupenda sifa kuliko kufanya kazi.
Kwa nini asifanye kazi ili Watanzania wamtunukie Degree ya Heshima kwa kazi nzuri alizofanya. Kwa sasa Watanzania wengi wanaishi kwa shida, bila kupata mahitaji yao ya lazima. Gharama za Maisha zimepanda mno.
Tunafikiri Raisi wetu angeshughulikia kero za Watanzania badala ya kila siku kupanda kwenye majukwaa kupewa Degree za Heshima na Ma- Profesa wanaotaka sifa kutoka kwake.
Raisi wetu Degree za Heshima nzuri zipo kwa Watanzania kama utawatumikia vyema. Lakini kama utaendelea na usanii huu, Watanzania hawatakuheshimu kwa kuwa na hizo Degree za Heshima za Wasomi wanaotaka sifa kutoka kwako.
Huyo anayempa hiyo degree, yeye mwenyewe mbona naskiaga hana degree yoyote?
Hii ya Kikwete ya jana nasikia kaiomba mwenyewe. Hajafanya lolote la maana kustahili tuzo ya udaktari katika uganga. Angalau Nyerere alifanya mengi kuhusu ukombozi wa Afrika na aliupa changamoto kubwa ulimwengu wa magharibi kuhusu uhusiano wake na nchi zisizoendelea. Wazungu walipenda mawazo yake na kumtunuku. Mkwere ni bogus.Hivi Nyerere alipata kupokea hizi shahada ngapi vile? Tena alikuwa anapanda pipa kwa fedha zetu kwenda kuzipokea hizo shahada!
Hivi Nyerere alipata kupokea hizi shahada ngapi vile? Tena alikuwa anapanda pipa kwa fedha zetu kwenda kuzipokea hizo shahada!
Wakuu,
Mmesikia nyingine kali hiyo, eti Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili Mzee Alli Hassani Mwinyi ametunuku rais Kikwete digrii ya heshima ya udaktari wa afya ya jamii wakati wa mahafali ya nne ya chuo hicho. Mnaionaje hii kasi ya wazee kukabidhiana hizo digrii??? Alianza Mzee Mkapa pale UDOM na sasa Mzee Mwinyi nae amejibu mapigo. Sijui nani atafuata kumtunuku JK digrii nyingine manake wazee wa aina hiyo bado wengi sana!!
Chanzo cha Habari: Tanzania Daima, tarehe 12 Desemba 2010.