JK; na mimi ujue naitwa Muhando | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JK; na mimi ujue naitwa Muhando

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Elli, Jun 3, 2010.

 1. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #1
  Jun 3, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,829
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  Jamani, naombeni mnisaidie kufikisha ujumbe huu kwa Rais wangu mpendwa kuwa kuanzia leo nimeamua kubadili Jina na kuitwa Whatever Muhando; najua baadhi yenu mtashangaa ila kuna ukweli mtupu kuwa RAHISI wetu anapendelea saaana kuwapa ulaji wale wote wenye majina ya Mikando ( plural)

  Nimeenda kwa Mchungaji wangu na amekubali nibadili jina langu la asili na kuchukua jina hilo jipya ambalo litaniwezesha kupata Ukurugenzi wowote ule toka kwa kiranja mkuu. majina ya Muhando yana sifa kuu zifuatazo: Ni majina maalumu kwa ajili ya kupata Ukurugenzi, Pili, Wana-sifa ya kuwakusanya ndugu zao wote wanaotumia majina yao bila kuulizwa na mtu; si wana sifa bwana??? kwa mfano pale kwa TaaaBaaaCaaaaa; wapo wakinda Mihando wapatao wanne, huko kwene umeme sasa watafika 20, na ndio maana nikaaamua kubadili jina na kuitwa....Muhando.

  Ikishindikana mimi kupata nafasi yoyote, naapa mwanangu wa kwanza ninayemtarajia hivi karibuni nitamuita Jina la Babu yake: Tigo Mhando. Hii itasaidia nae aingie kwenye orodha ya majina yanayo mkuna kiranja Mkuu.

  Raisi wangu, nikumbuke hata kwenye Ukurugenzi wa Always Time Cancellation ( ATCL) au kule kwenye miundo mbinu ya mabarabara baada ya kumfukuza yule mtani wangu...
   
 2. K

  Kikambala Senior Member

  #2
  Jun 3, 2010
  Joined: Jun 28, 2008
  Messages: 163
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Haaaaahaaaaaaaaaaaaa imekaa vizuri
   
 3. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #3
  Jun 3, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,829
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  Pia,
  Mwambieni nitamtafutia kiwanja cha kujenga kule Lushoto, kama kaka Beeee na Sumari/ sorry nafikiri ni kaka Asomaye, na wale wengine waliokuwa wakuu wa mkao wangu, oohh, sorry, mkoa wangu.

  Mwambie sijajikana utu wangu, Nimimi

  Shemdodo Orijino
   
 4. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #4
  Jun 4, 2010
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,276
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Yes you are Great Sinker
   
 5. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #5
  Jun 4, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,829
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  Heeeeee, heeeeee, kweli nimekubali kuwa hawajamaa ni Great Sinker/Thinker; Yote nadhani sawa hata tukiwaita Sinner oohh sorry ni Sina. Ulimi hauna mfuko/mfupa
   
 6. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #6
  Jun 4, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mbona mmeshaambiwa tena hapa kwenye thread nyingine huko nyuma kuwa Tido Mhanda (?Muhando) na huyo dada Mhando (?Muhando) hawana undugu??

  Kama watu wana sifa zinazohitajika hiyo tu ni sababu ya kutoajiriwa??

  Yaani waTanzania bwana, wakiwepo watu wa kabila moja sehemu moja ya kazi taabu, ndugu taabu, wenye majina ya kufanana taabu!!

  Grow up!!
   
 7. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #7
  Jun 4, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  wikend huondoka na vicheko vyetu walah
  hahahaha
   
 8. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #8
  Jun 4, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,829
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  Mmhh, mdau huyu kawa mkali kweli kweli, nadhani hajaelewa mada yenyewe, swala si undugu ni Majina na ndio theme ya Thread.....huyu atakuwa mjukuu wake tu, na analake jimbo/ sorry ana lake jambo
   
 9. bona

  bona JF-Expert Member

  #9
  Jun 5, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  sio massawe wote ni ndugu, au juma wote ni ndugu au mbura wote ni ndugu! ni majina tu, cha msingi ni hao watajwa wana vigezo au?
   
 10. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #10
  Jun 5, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,829
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  Heeeee heee, msumari huo.....umewachoma.

  Wapi mie sijui
   
 11. M-bongotz

  M-bongotz JF-Expert Member

  #11
  Jun 5, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,732
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Baelezeee
   
 12. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #12
  Jun 5, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,526
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Kufikiri majina yana uhusiano na vyeo ni sawa na kutofikiri kabisa . Great Thinker? Kafikirie umpa mazee.
   
 13. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #13
  Jun 5, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Mosi, Hivi kwani TANESCO waliteuana au kazi ilitangazwa ?

  Pili, ukishakubali kumpa Rais blank cheque ya kuteua, unapoteza kila sababu ya kuhoji uteuzi wake. Sanasana utaonekana kituko.
   
 14. Fisherscom

  Fisherscom JF-Expert Member

  #14
  Jun 5, 2010
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,441
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Hiyo kitu nimewahi kujiuliza sana kuhusiana na hilo jina kukutana nalo kwenye ofisi nyingi baadae nikapata jawabu kwamba kupata kazi/ajira fulani lazima kuwepo vigezo fulani vinavyoendana na kazi husika. Hivyo nikahisi kuwa wenye hayo majina Cvs zao zinawaruhusu kama ni kinyume na hilo mpwa nakupongeza kubadili jina.
   
 15. Fisherscom

  Fisherscom JF-Expert Member

  #15
  Jun 5, 2010
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,441
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 180
  Hiyo kitu nimewahi kujiuliza sana kuhusiana na hilo jina kukutana nalo kwenye ofisi nyingi baadae nikapata jawabu kwamba kupata kazi/ajira fulani lazima kuwepo vigezo fulani vinavyoendana na kazi husika. Hivyo nikahisi kuwa wenye hayo majina Cvs zao zinawaruhusu kama ni kinyume na hilo mpwa nakupongeza kubadili jina.
   
 16. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #16
  Jun 5, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,829
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  Waalaah, nakuambia haya majina yana raha yake, muulize hata yule shehe wetu wa yaya, yule muona mbali atakuambia kuwa jina lako, litakufanya usipate kazi kwa huyu Blazameni...smiling face
   
Loading...